Jumanne, 12 Januari 2016

UTUMWA WA HIARI



UTUMWA WA HIARI



Katika hali ambayo watu wengi hawapendi kuishi wala kusikia ni hali hii inaitwa UTUMWA kwani ndani ya hali hii inaambata na mateso ya nafsi na wakati mwingi ina ambatana na mateso ya mwili, kiukweli unapozungumzia utumwa lazima uendane sambamba kufanya jambo nje ya hiari binafsi (matakwa binafsi) lakini katika dunia ya sasa  kuna utumwa wa kupenda au utumwa wa hiari binafsi na wakati mwingine utumwa uendana sana na majonzi hasa katika moyo.

Hili neno UTUMWA alina rafiki katika dunia, na kama ukiamua kuanzisha maandamano ya kuondokana na utumwa wa nafsi basi bila shaka utapata wafuasi wengi na hasa tabaka la chini.
Kwa jinsi watu wanavyolichukia hili neno watu wangekuwa na uwezo wa kuliondoa neno hili katika kamusi basi wangeliondoa maana neno linachefua moyo! Kwakua alipendezi kutamkwa wala maana yake bali linaonekana kama JANGA.

Adui mkuwa wa utumwa ni uhuru, kwani palipo na uhuru basi hapo hakuna utumwa na palipo na utumwa basi hapo hakuna uhuru hawa ni maadui ambao hawawezi kukaa sehemu moja na kuamua jambo hilo kwa kushirikiana kama timu.

Kuna mambo mengine mtu anaweza akaona ni ya kawaida kwakuwa watu wengi wanafanya na kwa mtazamo wa kawaida unaweza kuona kama yanafaida katika maisha ya watu wanavyoishi kutokana na hali ya kuzoelea kwa watu wafanyao mambo hayo au kutokana na tafsiri inayotolewa na macho yako.

Utumwa wa hiari ni hali ya mtu kujikuta kufanya jambo yeye binafsi kutokana kushindwa kufanya tofauti na hali iliyopo na akili yake ikiona kuwa hakuna njia ila inabidi nikubaliane na hali hii kwa maana wakati mwingine unaweza kujikuta katika hali mbaya zaidi kwa kushindwa kufanya jambo unalopaswa kufanya.

Huu ni utumwa ambao unajikuta wewe binafsi unatengeneza nafasi katika kukamilisha swala au jambo unalolifanya kila siku au kila wakati, na huu ni utekwa katika upande wa akili na mwili unakuta unafanya kwakujua lakini hauna njia mbadala nyingine ya kufanya tofauti na vile unavyopaswa kufanya. Wakati mwingine utumwa huu unaweza kufanya hata bila ya kusimamiwa na mtu na wakati mwingine unaweza kufanya kwa shinikizo au kusimamiwa na mtu ila katika hali ya kupenda.

Huu ni utumwa ambao wewe binafsi ndio unajua kwanini nafanya hivi na sio mtu aliye karibu yako au mwenye nafasi yeyote katika maisha yako, kwakua kile unachokiamini wewe na namna unavyopenda uwezi kuamini kama kuna mtu mwingine anaweza kukuelewa kama unavyoelewa/unavyoamini.

Huu ni utumwa ambao hauwezi kuchoka katika kuenenda katika mtindo maisha ambao umeuchagua pasipo kukata tamaa bali ni katika kuridhisha akili yako na mwili wako, wakati mwingine unawezajua kuwa kitu hiki au jambo hili mwisho linaweza kuniweka katika hali ngumu lakini bado utakuwa ukiendelea kufanya hivyo maana katika kufanya hivyo ndio uleta burudiko la nafsi yako.

Kwakua huu ni utumwa unaohusisha hiari yako hivyo inakuwa sio kitu rahisi tu kwa wewe kuwaza tofauti na hasa katika hali unayostahili kuwa nayo, wakati mwingi unakuwa katika giza japo unajikuta una hali ya kupenda pasipo kujua hasa maana yake nini na kujua faida yake au matokeo yake katika jambo ambalo unalolitaka kulifanya.

Na ukumbuke kuwa utumwa wa hiari unazaliwa pale tu akili inapokosa kutawala jambo Fulani katika mwenendo mzima wa maisha yako, jambo hilo linaweza kuwa la siri au wazi lakini linakuwa lina nguvu hata kushindwa kuzuiwa na akili au mwili wako, utumwa huu unakupa nguvu hasa unapotambua hakuna mtu anayekuona hivyo unakuwa huru kutumia uhuru wako.

Hakuna nguvu ya kweli inayoweza kuzaliwa hapa ikiwa tu tayari utumwa wa hiari utakuwa ukisababisha giza kuzidi kuchukua nafasi katika maisha yako, na mwisho utakapojitokeza unaweza ukaweka wazi yale yote yaliyo uteka mwili wako na akili yako.

Imeandaliwa na:

Cothey Nelson…………………………………………………………0764 018535

UTUMWA NI TESO LA NAFSI

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni