Jumanne, 5 Januari 2016

ACHA NIUTE USIKU KUWA GIZA



ACHA NIUITE USIKU KUWA GIZA


 Ni jambo la kawaida tu pindi inapokuwa usiku basi watu hupenda kusema habari za usiku au usiku mwema…… wakiwa wanaenda sawa na majira yaliyopo, hali kadhalika pindi inapokuwa mchana watu usema mchana mwema au habari za mchana, imekuwa ni kitu kimoja kizuri sana katika utamaduni wa kusalimiana hasa waafrika,japo salamu ya mchana imekuwa ikitumika sana kuliko ya usiku kutokana na wingi wa watu unaokutana mchana kuliko usiku!

Ni vizuri kuita usiku kuwa ni usiku ili uweze kuishi kulingana na hali iliyopo hasa mwanga unakuwa hafifu hivyo unahitaji kuwa makini katika mwenendo wako katika usiku huo na pia katika mchana lazima ukubali kuwa huu ni mchana yanipasa nitembee katika hali stahiki nikijua kuwa huu ni mchana kila mtu nirahisi kuniona kwahiyo lazima nitembee katika hali iliyo sawa kulinganisha na wakati.

Na ndomana watu wengi katika ulimwengu wa sasa hasa huu wa utandawazi wamekuwa wakitembea na kuvaa mavazi yanayo ashiria huu ni usiku na mchana (tunahita maendeleo) na pindi ukavaa mavazi ya usiku wakati wa mchana bila shaka unaweza kuibua maswali kwa jamii inayokuzunguka, kwakua jamii inategemea kila vazi linawakati wake na jamii ya sasa imekwenda mbali kidogo kusema pia kila hali ya hewa inamavazi yake mathalani majira ya joto, masika,baridi n.k kila hali inapotokea ina aina ya mavazi yake stahiki ambayo kama binadamu anapaswa kuvaa pasipo kuchanganya!

Na unaweza kushangaza watu pindi utakapoanza kuita usiku kuwa ni mchana hata kama kunataa zenye uwezo mkubwa ambao mwanga wake unafanana kuwa kama mchana lakini ukweli utabaki kuwa huu ni usiku ila taa zilizopo zina mwanga mkali sana.

Acha niuite usiku kuwa giza nini maana yake!
Nipende kusema kuwa usipokubali hali uliyonayo ni ngumu tu kuvuka sehemu nyingine iliyo hatua bora katika maisha yako!

Wako watu walikuwa wanaumwa sana na wakati mwingine magonjwa ya aibu mtu anaona hawezi hata kumwambia rafiki yake anabaki kutumia madawa katika duka la dawa kununua dawa za kutuliza maumivu hawezi kwenda hospitali wala kutafuta suluhuu ya tatizo linalo mkabili kwa kuogopa kuwa ataweza kuchekwa au heshima yake itapungua katika familia au katika jamii inayomzunguka.

Wako wanawake na wanaume wanajua kuwa hawana uwezo wa kuzaa kabisa kutokana na ushahidi wa kimadaktari lakini pindi wanapokuwa wamepata wenzi wao wanakuwa sio wa wazi katika kueleza hali zao za kiafya na matokeo yake wamekuwa wakileta shida katika jamii zao na hata kupelekea ndoa zao kuwa na wakati mgumu sana tofauti na hali sahihi inayotakiwa kuwepo katika ndoa.

Wako na wanafunzi wamekuwa na matokeo mabaya katika hali ya mwanzo kabisa katika masomo yao lakini wamekuwa sio wa kweli pindi wanapoulizwa na ndugu zao au walezi wao na kukuta kusema tofauti na hali ilivyo na mwisho hali ikawa mbaya sana na hata kupelekea kufeli katika masomo yake.

Wako watu wengine wamekuwa wakisema Mungu pekee yake anajua na ndiye ataye jibu na kunipa haja ya moyo wangu lakini wakati mwingi imekuwa ni vigumu tu kuwa Mungu kushuka kwako kwa namna unavyofikiri anaweza akamtumia mtu naye akawa jibu katika swali lako linalo kukabili.

Usipokubali na kutambua kasoro zako ipo siku itakuweka katika mazingira magumu sana na hata kukupelekea kujuta kwanini ukuwa wazi toka mapema na hatimae yakakufikisha mahali ulipo sasa ambapo kiukweli ukupatarajia.

Pindi unapokubali tatizo sio kwamba unataka likae na wewe milele bali njia sahihi katika kulitambua marefu yake na mapana yake ili iwe rahisi kutoka pale ulipo kwakua utajua chanzo chake  na utafanya akili yako ifanye kazi katika hali ya utulivu na kupata jibu sahihi na ikawa suluhu ya kudumu!

Na hali ya kukubali jambo kuwa limekukuta sio ishara ya kuonyesha Mungu ameshindwa kuliepusha lisikupate hapana kunawakati mwingine Mungu anataka wewe uwe ushuhuda kwa wengine waone jinsi ulivyoteseka na hatimae ukaibuka kuwa mshindi.

Imeandaliwa na:

Cothey Nelson…………………………………………..0764 018535

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni