Jumanne, 17 Mei 2016

UTULIVU KATIKA UTATUZI



UTULIVU KATIKA UTATUZI




Hakuna jambo linaloleta furaha sana kama utatuzi katika jambo lililokusumbua! hasa lililochukua  muda mrefu, pindi unapofikia hatua ya kutatua jambo fulani na hatimae kutokuwa kizuizi tena au mzigo katika moyo wako basi hapo bila shaka unaweza kusikia raha katika hisia zako.

Ni shauku ya kila mtu pindi jambo linapotokea na hasa jambo ambalo litasumbua akili yake ni kulipatia ufumbuzi wa mapema sana na pindi jambo hilo linaposhindwa kutatuliwa kwa mapema uweza kuagharishwa na kupewa siku nyingine katika utatuzi wake  na si ajabu jambo hilo likawa la muda mrefu kutokana na kukosa ufumbuzi mapema.

Kuna sababu mbalimbali zinazo sababisha jambo kuchukua muda mrefu katika kutatuliwa:
i)                    Haina ya jambo lenyewe
ii)                  Kutojua mwanzo/dalili zake
iii)                Kutokuwa makini pindi jambo hilo linapoanza

Katika dunia inaamnika kuwa katika utulivu bila shaka jambo jema au mawazo ya busara yatazaliwa hapo na kipindi kingine mtu anapokosa jibu la haraka ataomba nafasi apumzike kwanza ( utulivu) ndipo aje na wazo lingine lenye tija au la msaada wa uhakika.

Mwanzo 1:2 Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji

Tunaona hata Mungu katika uumbaji kabla ajaanza kazi yake kwanza Roho yake ilitulia katika vilindi vya maji na mpangilio wa vitu vikaanza kufanyika na hatimae ikatokea dunia tunayoishi sasa.

Hivyo tunaamini katika utulivu mambo mema yanaweza kuzaliwa hapo na tija au manufaa katika katika jamii yako na wewe binafsi, lakini niseme utulivu peke yake haiwezi kuwa wa maana sana zaidi kama kinachoendelea ndani yako hakina msingi mzuri, ndomana unaweza kumuacha mtu atumie muda wake vizuri katika utulivu lakini mwisho wake usione maana ya kumpa muda wa mtu katika utulivu maana kile kitu kilichotoka hapo akina mchango wa kujenga zaidi ya kuharibu.

Pamoja na hayo yote bado na amini sana katika utulivu kuna uwezekano wa kutoka kitu chema kama ndani yako kutakuwa na mambo haya yamezingatiwa:
i)                    Uondoe maslahi binafsi

• hasa katika maamuzi yanayohusisha kundi/ jamii kwa ujumla.

• usitake kuonekana kuwa wewe ndio ulifanya

•usitake kuwa wa kwanza wa wewe kufaidi matunda yake
                                                                                                              
•usitake heshima ya haraka

•usipende kuona baadhi ya watu waki haibika

Hata mtu akiwa na uwezo mkubwa kiasi gani lakini sio wakati wote anaweza kuwaza katika utulivu na kutoa kitu chema, anaweza kupatia baadhi ya mambo na mengine akatoa mawazo yaliyobeba maslai yake.

Utulivu usio na Mungu ndani yake jambo linapofanikiwa katika kuleta utatuzi wa jambo fulani basi bila shaka majivuno na kujiona fahari itakuwa ndani yake na kuona bila yeye jambo hilo lisingefanyike.

Utulivu uliombeba Mungu kamwe hakuna jambo linaloshindikana hapo labda ukatai kufuata njia ambayo atakuambia uifuate:

2 Samweli 16:23 Na shauri lake Ahithofeli, alilokuwa akilitoa siku zile, lilikuwa kama mtu aulizapo kwa neno la Mungu; ndivyo yalivyokuwa mashauri yote ya Ahithofeli, kwa Daudi, na kwa Absalom

Imeandaliwa na:

Cothey Nelson…………………………………0764 018535