UTULIVU KATIKA UTATUZI
Hakuna jambo linaloleta
furaha sana kama utatuzi katika jambo lililokusumbua! hasa lililochukua muda mrefu, pindi unapofikia hatua ya kutatua jambo
fulani na hatimae kutokuwa kizuizi tena au mzigo katika moyo wako basi hapo
bila shaka unaweza kusikia raha katika hisia zako.
Ni shauku ya kila mtu
pindi jambo linapotokea na hasa jambo ambalo litasumbua akili yake ni kulipatia
ufumbuzi wa mapema sana na pindi jambo hilo linaposhindwa kutatuliwa kwa mapema
uweza kuagharishwa na kupewa siku nyingine katika utatuzi wake na si ajabu jambo hilo likawa la muda mrefu
kutokana na kukosa ufumbuzi mapema.
Kuna sababu mbalimbali
zinazo sababisha jambo kuchukua muda mrefu katika kutatuliwa:
i)
Haina ya jambo lenyewe
ii)
Kutojua mwanzo/dalili zake
iii)
Kutokuwa makini pindi jambo hilo
linapoanza
Katika dunia inaamnika
kuwa katika utulivu bila shaka jambo jema au mawazo ya busara yatazaliwa hapo
na kipindi kingine mtu anapokosa jibu la haraka ataomba nafasi apumzike kwanza
( utulivu) ndipo aje na wazo lingine lenye tija au la msaada wa uhakika.
Mwanzo
1:2 Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi
vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji
Tunaona hata Mungu
katika uumbaji kabla ajaanza kazi yake kwanza Roho yake ilitulia katika vilindi
vya maji na mpangilio wa vitu vikaanza kufanyika na hatimae ikatokea dunia
tunayoishi sasa.
Hivyo tunaamini katika
utulivu mambo mema yanaweza kuzaliwa hapo na tija au manufaa katika katika
jamii yako na wewe binafsi, lakini niseme utulivu peke yake haiwezi kuwa wa
maana sana zaidi kama kinachoendelea ndani yako hakina msingi mzuri, ndomana
unaweza kumuacha mtu atumie muda wake vizuri katika utulivu lakini mwisho wake
usione maana ya kumpa muda wa mtu katika utulivu maana kile kitu kilichotoka hapo
akina mchango wa kujenga zaidi ya kuharibu.
Pamoja na hayo yote
bado na amini sana katika utulivu kuna uwezekano wa kutoka kitu chema kama
ndani yako kutakuwa na mambo haya yamezingatiwa:
i)
Uondoe maslahi binafsi
• hasa katika maamuzi yanayohusisha kundi/
jamii kwa ujumla.
• usitake kuonekana kuwa wewe ndio
ulifanya
•usitake kuwa wa kwanza
wa wewe kufaidi matunda yake
•usitake heshima ya haraka
•usipende kuona baadhi ya watu waki
haibika
Hata mtu akiwa na uwezo
mkubwa kiasi gani lakini sio wakati wote anaweza kuwaza katika utulivu na kutoa
kitu chema, anaweza kupatia baadhi ya mambo na mengine akatoa mawazo yaliyobeba
maslai yake.
Utulivu usio na Mungu
ndani yake jambo linapofanikiwa katika kuleta utatuzi wa jambo fulani basi bila
shaka majivuno na kujiona fahari itakuwa ndani yake na kuona bila yeye jambo
hilo lisingefanyike.
Utulivu uliombeba Mungu
kamwe hakuna jambo linaloshindikana hapo labda ukatai kufuata njia ambayo
atakuambia uifuate:
2
Samweli 16:23 Na shauri lake Ahithofeli, alilokuwa akilitoa siku zile, lilikuwa
kama mtu aulizapo kwa neno la Mungu; ndivyo yalivyokuwa mashauri yote ya
Ahithofeli, kwa Daudi, na kwa Absalom
Imeandaliwa na:
Cothey
Nelson…………………………………0764 018535
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni