Jumanne, 19 Aprili 2016

NGUVU YA HAZINA



NGUVU YA HAZINA

Unaweza kuona mtu upenda kuchelewa katika mambo mbalimbali, unaweza usijue kwanini mtu anachelewa? mathalani Ukiona mtu ananunua bidhaa alafu anasema chenji ibaki ukouko hakuna shida,ukabaki na maswali kichwani?  Au Unaweza kuona mtu anaangusha kinywaji alafu anakiacha na kwenda kuchukua kingine, unaweza kuwa na maswali mengi pamoja na majibu yako binafsi unaweza kuona mtu huyu ajaona alichododosha au aibu hama anajiona?

Sikatai Ana B yanaweza kuwa majibu lakini kuna uwezekani kuwa NGUVU YA HAZINA, kwa kiasi kikubwa inawezakana kuwa siyo yeye bali NGUVU YA HAZINA inampa ujasiri wa kufanya kile anachokifanya pasipo kuogopa huku akiamini kuwa kile anachofanya ndicho anachotakiwa kukifanya na sio kingine ambacho wengine wanaona kuwa ni sahihi.

Unaweza kuona mtu anasumbua mtaa, anachosha watu, anaboa watu analeta maswali katika kichwani mwa watu lakini kubwa kumbe inaweza kuwa ni nguvu ya hazina inayomsukuma kufanya kile anachokifanya na kuona ni sawa watu kumuongelea kwakua yeye anazo fedha na wengine hawana(maskini) hivyo wacha wamuongelee yeye azidi kupeta, kwa kawaida mtu wa namna hii upenda sana kupigiwa magoti na kumuona kuwa yeye anastahili sana kuliko asiye hadhi yake!

Ukitaka kupata shida kutana na mtu mwenye hazina yenye nguvu alafu hazina inamwendesha au inamtaalakisha au inamsukuma kufanya mambo………….unaweza ona ni bora ukutane na simba akakutafuna basi historia ya maisha yako ikaishia hapo kuliko kuishi na mtu wa namna hii inakuwa ni zaidi ya mateso.

►Asante karibu………………………….!!!

Tunafahamu kuwa hazina ikiwa njema bila shaka maisha yanakuwa njema! Na furaha itokanayo na utoshelevu utazani kumbikumbi wakati wa mvua basi bila shaka inaweza kuchomoza furaha inayoambata na uwepo wa fedha.

Bila shaka namna unavyoishi kwa kiasi kikubwa uweza kuamliwa na hazina uliyonayo ukiona mtu huyu anapanda katika gari lake na huyu anapanda daladala hapo kunatokana na utofauti wa uchumi kati ya mtu husika na kwa kiasi kikubwa kinachoamliwa hapo sio kupenda bali hazina ya mtu.
HAZINA ni usalama wa mtu katika kumudu mahitaji yake, hivyo ukubwa wa hazina ndio ukubwa wa kuimarika kwake. Na bila shaka kila mtu upenda kuona hazina ikiongezeka na sio ikipungua.

Upaswi kupatashida kuumia kuwa matumizi yamekuwa mengi bali ni vizuri kutambua kuwa shida yote unayopata kwa kiasi kubwa ni kutokana na hazina kutotosheleza mahitaji husika. Hivyo ni vizuri usipange safari ya kutoka kawe kwenda gongo la mboto (700) wakati nauli yako ni kutoka kawe kwenda kariakoo tu (400).

Mathayo 7:24 Basi kila asikiaye hayo maneno yangu, na kuyafanya, atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba;

Mathayo 7:25 mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, isianguke; kwa maana misingi yake imewekwa juu ya mwamba.

Nazungumzia hazina ambayo ambayo haijawaitokea ikakupoteza au kukuacha bali hii hazina inaweza kukupa fedha, uzima, nguvu na maarifa na yote ambayo dunia haiwezi kukupa kwakua yenyewe imebeba ukamilisho.

Hii hazina ndio asili na ustawi wa hazina zote maana inakuwa imeshikwa na Mungu mwenyewe na hakuna hawezaye kuharibu.

Mathayo 6:20 bali jiwekeeni hazina mbinguni, kusikoharibika kitu kwa nondo wala kutu, wala wevi hawavunji wala hawaibi;

Imeandaliwa na:

Cothey Nelson……………………………………………0764 018535

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni