UNAONA NINI?
Moja ya milango mitano
ya fahamu ambayo mwanadamu uitumia
katika shughuli za kila siku ni JICHO(MACHO) ambayo kazi yake kubwa ni kuona
japo inakazi nyingine kama njia mojawapo ya mwili katika kutoa taka mwili na kazi
nyingine nyingi!
Katika maisha ya
mwanadmu utendaji wake mkubwa umebebwa na KUONA jambo au tukio unaweza kukuta
huyu ameacha mwenzi wake, hawaongei tena, hawashirikiani tena, na hata kuwa
hawapendani tena inaweza kuwa ni matokeo baada ya mtu kuona kitu akikifanya mwenzake na hatimae mwingine akaamua kuchukua maamuzi
ya kuwa mbali naye!
Kuona jambo au tukio
huu ni ushahidi ambao unapewa nafasi kubwa katika himaya ya mahakama, pindi
unaposema ushahidi wangu ninao utoa ni ushahidi unaotokana na kuona mwenyewe na
sio kusimuliwa na mtu basi bila shaka huo ushahidi unakuwa na uzito wa kipekee
kuliko ushahidi wa kusikia.
Katika uwanja mzima wa
KUONA kuna kuona kwa macho
kunakohusishwa na ufahamu wa mtu na uko ndiko jikoni kwa mtu katika kuchukua
maamuzi ya haraka au ya muda, bila shaka ufahamu wako ndio unaoamua utendaji
wako mara baada ya kuona japo kuna wakati hisia uweza kuchukua nafasi na
hatimae watu wakashangaa hata wewe umeamua jambo hilikwakua sio kawaida yako.
Ni wazi kabisa vile
unavyo ona ndivyo unaweza kujiamini na kuchukua hatua katika jambo husika, wako
watu wamekuwa wakiamua jambo baada ya kuona kitu fulani kikitendeka au kutokana
namna anavyoamini, alivyoona kwa wengine alivyoshaurika au shawishika binafsi.
Yako mambo mengi
yanawatokea watu ni kutokana na vile wanavyoona na hatimae kuamini mathalani
mtu anaweza kuingia ulingoni katika mashindano ngumi baada ya kumuona mpinzani
wake anaweza kuona kuona kuwa nafasi ya kushindwa hipo kubwa kuliko ya
kushinda……..na baadhi yao wanaweza kuathirika na kumbukumbu ya mpinzani wake kuwa
katika mapambano yake hajawai kushindwa au kashindwa pambano moja na kama
alishawai kushindwa basi aliyemshinda ameshakufa hivyo huna hata wakupata mbinu
zitakazo kukuwezesha katika kupigana na mtu huyo.
Wako wengine wanapoitwa
kwenye usaili wanapoingia mahali pa usaili anaweza kujiona hapo yeye astahili
hivyo hata ujasiri wa kujibu maswali wote unapotea kama sio kuisha kabisa na
uwezekano uweza kuwa mkubwa wa yeye kukosa kazi kuliko kupata kazi, sio hilo tu
bali wako hata wanafunzi wanapojiandaa na mitihani uwa uweza kuona mimi hapa
katika somo hili mimi siwezi kupita hivyo hata maandalizi yake yanakuwa sio
yaliyo ubeba umakini na bidii sana kwani uamini hapa kushindwa ni haki yangu.
Mbali hilo kuna jambo
ambalo ni la hatari sana hasa kwa wagonjwa wengi katika nguvu ya kuona uwa
kinacho wa maliza ugonjwa sio ugonjwa bali ni namna wanavyouelewa huo ugonjwa
na hatimae KUONA kuwa huu ni ugonjwa hatari sana hivyo wakati wowote kuna
mahali pana nihita tu iwe isiwe.
Hakuna kitu kibaya kama
kuona vibaya kwani uwezi kufika salama kama unaona jambo katika mtazamo tofauti
na vile ulivyopaswa kuona mathalani mtu
anaweza kumwitaji mwenzi wa maisha anaweza kuwa na maswali mengi hivi mimi
nitaweza kweli? Hivi anaingilika? Akinikataa itakuwaje? Hivi huyu simcharuko kweli?
Hivi atanipenda kweli mimi? Hivi ndugu zake watanikubali kweli? Mtu huyu uweza
kushtukia yule anayempenda kaolewa au kaoa pasipo kupata jibu sahihi katika
akili zake.
Niseme kunanguvu kubwa
katika KUONA vyema kwa katika kuona vyema unaweza kubadili hali isio faa ika
faa inategemea na mtazamo wako kwa kiasi kikubwa:
Mtazame ezekieli,
Ezekieli 37:3
Akaniambia, Mwanadamu, je! Mifupa hii yaweza kuishi? Nami nikajibu, Ee Bwana MUNGU, wajua wewe.
Muhimu kutambua Mungu yuko kwa ajili ya
kukung’arisha na wala sio kukuabisha hakuna zito atakalo liruhusu litakalo
kukushinda wewe kwa maana aibu yako itakuwa aibu yake kama ukiwa wake!
Imeandaliwa na:
Cothey
Nelson…………………………………0764 018535
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni