NINI TATIZO?
Unaweza kukuta mtu anasema leo sijisikii kusema na mtu! au Leo sijisikii kula chochote na huku haumwi au
mabadiliko ya kibiolojia! hama Leo nataka niwe pekee yangu! au Leo sijisikii
kupokea simu ya mtu yeyote wala kuingia katika mitandao ya kijamii!mh! Leo
sitaki utani kabisa na mtu yeyote! Yaaani leo naomba mniache tu! Kwa kweli leo
siku yangu haikuwa vizuri kabisa! Na mwingine ataenda mbali kidogo atahitaji
dawa ya kutuliza maumivu ya kichwa! Na mwingine atasema Jamani leo mniombee tu
maana moyo wangu siuelewielewi kabisa! Swali langu kwako ni dogo tu JE! TATIZO NINI?
Unaweza kukuta mtu anatoa sababu ya kuvunja ahadi ya kukutana”samahani
leo sijisikii vizuri kabisa” hata kama ni uongo atasema tu kwa sababu kuna kitu
kime mvuruga ndani ya kichwa chake…mwingine atashindwa ata kwenda kazini na
kutoa dharura ambayo haijaokoka maadamu apate tu aone mahali gani nitapata
AMANI iliyotoweka ndani maana jambo hili silo la kawaida kwangu! Narudia tena
nasema TATIZO NINI?
Unaweza kukuta mtu amekuwa bubu ghafla inawezekana mara tu
baada ya kupokea simu au ya kutoka uko aliko toka na pindi utakapoanza
kumuongelesha mdomo unaweza kuwa mzito na machozi yakatoa majibu yanaelezea
hisia za moyo tafsiri ambayo ni ngumu kuielewa maana ni zaidi ya siri! Nauliza
tena TATIZO NINI?
Unaweza kukuta mtu amefika chumbani kwake kajitupa ndani hanamaelezo
kabisa ule ucheshi wake umepotea kabisa, lile tabasamu alipo tena na anaweza
kujitaidi kukupa karatasi ikielezea yale aliyojibiwa na akapelekea kuamuru
mwili wake kutoa maji yapitayo machoni! Nauliza kwa mara ya mwisho TATIZO NI
NINI?
Ni kweli hali hii inaweza kukuta katika mambo mbalimbali
ikapelekea kuwa na sura ambayo wewe mwenyewe kama ungajiangalia kwenye kioo
ungejichukia sana….. inaweza kuwa ni tatizo la kifamilia au binafsi au jamaa
ambao moyo wako ulimpa nafasi katika maisha yako kuwa ni rafiki yako hivyo
lolote baya lililo mpata yeye wewe linakugusa kwa asilimia zote.
Karibu tuzungumze?
HIVI MNAPO AMUA KUVUNJA MAUSIANO YA KIMAPENZI NANI ALAUMIWE
AU NANI NI CHANZO?
Je! Ni ninyi wenyewe? Shetani? Mungu? Ni nani wa kulaumiwa au
hakuna wa kulaumiwa basi kama hakuna wa kulaumiwa sio vibaya mnaweza kupendana
katika mwendelezo! Possible answer!
Wakati mwingine imekuwa ngumu kujua nani ni tatizo kwakua
kila mtu atavutia kwake na kusema yule ni chanzo kwakua aliniambia mimi hivi!
Na mwingine atasema yeye ndio chanzo kwakua yeye alinijibu hivi! Basi tukaamua
hivi……..na maisha yanaendelea ni kweli hata kama msinge amua hivyo bado maisha
yange endelea maadam uhai ungalipo.
pindi mnapoingia
katika ulimwengu huu mnakuwa mnaishi dunia nyingine inaitwa dunia ya wapendano
na hapo mnaunganisha hisia zenu kwa ukali usio na maelezo ya kueleweka ila
wenyewe mnaelewa sana kuliko maelezo.
Unaweza kuona mtu ana kuwa na huyu baadae anasema huyu anifai
au moyo wangu ahujaridhika kabisa na baada ya kupumzika kwa kitambo kidogo
anarudia tena na bado anasema bado moyo wangu haujapata tulizo lake! Hapa TATIZO
NI NANI? Unaweza kusema bado sio tatizo
langu ila linaweza kuwa ni hisia zangu au la mtu mwingine.
Haya ni maisha ambayo hakuna mwanadamu anapenda kuishi maisha
ya namna hii leo yuko na huyu na kesho yuko na yule na hata kufikia mtu mpaka
anaoa au kuolewa mapaka anaanza kuwafananisha mtu aliye naye na mtu aliyewai
kumjua mwanzoni.
Sikatai tatizo linaweza kuwa kwa mtu mwingine au kwako lakini
lazima uchukue muda wa kutafakari sana kile unachokita katika akili yako ni
kweli kipo na je! Hicho kinatengenezwa nawe au kinatengezwa na wengine na wewe
unakitumia tu.
Ni muhimu kujiuliza kuwa kile kinachosemwa ni kweli kipo na
kina uhusiano wa kweli na hayo mahusiano au kuna utofauti mkubwa na unajua kila
hali inategemea na mtu husika.
Ninachoamini mimi kuwa UKIJUA KWELI UTAKUWA SALAMA NA
UTASABABISHA USALAMA KWA WENGINE!
Ni kweli hauwezi kuwaambia watu kitu ambacho wewe ukijui
vizuri, kumlaumu mtu sio jambo jema ni bora ujitambue wewe binafsi kuweza
kumudu mwili wako na ukiweka ustawi wa kudumu katika maisha yako na sio STAREHE
ISIYO NA TIJA.
Katika hili uhitaji kuona Mungu akupendi au watu wanataka
kukuchezea tu akili yako bali ni vizuri utambue USALAMA WAKO UNATEGEMEA UBORA
WA AKILI YAKO!
Imeandaliwa na:
Cothey Nelson………………………………………………………0764 018535
TUNZA THAMANI YAKO!