Jumanne, 28 Novemba 2017

NGUVU YA KUJITAMBUA.






Uweza wa kufanya mambo na ujasiri unaozaliwa/ kutokana na kujitambua.

Kuna kujitambua kunako zaliwa na vitu vingi mathalani kujitambua kunakotokana na mila na desturi katika jamii husika kujua majukumu yake na kuyatekeleza, mara nyingi utegemea miaka ( rika na umiliki) pamoja na nafasi ya mtu katika ukoo na hata jamii husika.

Pia mtu uweza kujitambua hama kuanza kujitambua kutokana na elimu ( rasmi au isiyo rasmi) au baada ya kupata ushauri kutoka kwa wataalamu au wazee wenye hekima.

Ni ukweli usiopingika kuwa uhuru mkamilifu unakuja baada ya kujitambua na bila shaka kuonewa na kuteseka kunakuwa ni maisha yako baada ya kuishi maisha ya kutojitambua au kukubali kuishi maisha ya kutojitambua. 

Maisha ya kutojitambua hayana tofauti sana na maisha ya utumwa japo kwa kiasi kikubwa inaweza kuwa ni zaidi ya utumwa, kwani njia rahisi ya kuchukua haki ya mtu mfanye tu asijitambue.

Wagalatia 4: 1 Lakini nasema ya kuwa mrithi, wakati wote awapo mtoto, hana tofauti na mtumwa,  angawa ni bwana wa yote;
                       2 bali yu chini ya mawakili na watunzaji, hata wakati uliokwisha kuamriwa na baba.

  Kujitambua kwa namna zote ( mila na desturi, elimu n.k) vinakikomo chake na kwa kiasi kikubwa haviwezi kukupa maisha uliyokusudiwa kuishi mathalani unaweza kuwa mtu fulani kama vile msomi mwenye daraja la juu sana katika masomo yako na zaidi ukawa unajitambua kutokana na elimu uliyonayo , unajipenda , unajielewa lakini maisha yakaenda pasipo kuona yale uliyotegemea mfano. 

Ukosefu wa kazi unayotaka hivyo ukajitahidi kuvumilia kutokana na masharti magumu yakupata kazi unayoitaka lakini mwisho ukakubali aibu ya mwili ( rushwa ya ngono) ili maisha yaendelee.
Pia inawezekana ulipata kazi kwa neema tu ya Mungu ( kwa uhalali) lakini ghafla pakatokea na mtikisiko kazini kuwa bila ya kutoa rushwa ( kwa ujumla ) kibarua kitaota nyasi! Hama kujiingiza katika mfumo fulani.

Karibu……………………!!

Nguvu ya kujitambua kunakotokana na Neno la Mungu!

Ø  Unaweza kushangaa kuona mtu anaogelea katika bahari kama samaki badala ya kuzama.

Ø  Unaweza kushangaa mtu anakula vizuri na kuishi vizuri na zaidi kunawiri wakati ulitegemea ameze vidonge afe kwa kile kilicho mkuta.

Ø  Unaweza kushangaa pia mtu uliyetegemea asuse kula na aondoke lakini ukakuta anajiachia zaidi na kupafurahia na huku akila kwa nafasi.

Kujitambua huku ni zaidi ya kulalia/kumiliki madini ( almasi/ tanzanite n.k) maana ubora unaotokana na hali hii hakuna mfano wake.

Unapojitambua kutokana na hali hii hapo ndipo unaanza kuishi maisha aliyokusudia ( maisha uliyotakiwa/ unayotakiwa kuyaishi ) na unapoliishi kusudi la Mungu kwa ukamilifu unakuwa Mungu duniani ( Mungu kuishi kupitia wewe) na udhihirisho wa Mungu unakuwa juu yako.

Kama kweli unataka kujitambua wewe ni nani basi liruhusu neno la Mungu linalokaa ndani yako likutambulishe. Na sio biblia inayokaa chumbani hama sebuleni pasipo kuwa kiongozi wa maisha yako bali kuwa moja ya pambo la nyumba na zaidi sana wakutambue kuwa wewe ni mkristo.

Huu ni utambulisho usiochuja bali unaongezeka siku kwa siku ( utambulisho unaotokana na Neno la Mungu).

INAITWA SIKU! BARIKIWA.

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson……………………………………………..0764 018535

Jumanne, 14 Novemba 2017

USIPOTEZE MWELEKEO ( USIJISAHAU)






Moja ya vitu vya msingi sana vya kuzingatia ili ufike unakotakiwa kufika ni kuto poteza mwelekeo, ingawa mara nyingine unaweza kuupoteza kwa kujua hama kutojua!

Unapo poteza mwelekeo uweza kusababisha hali ya kuchelewa kufika katika safari yako hama kutofika kabisa! Na muhimu kujua atutimizi ndoto zetu kwakuwa tuna akili nyingi bali kwa kufuata maelekezo yaliyo sahihi.

Baadhi ya vitu vinavyoweza sababisha  kupoteza mwelekeo ni ugumu wa safari  unao onekana kwenye akili au hali ya kushiba ukasahau njaa.

Mara nyingi mtu anapolianza jambo au safari ( mwenye akili njema) anakuwa ana matarajio fulani au ana matarajio au analengo fulani lakini mambo yote haya yanaweza kutimia tu kama hutopoteza mwelekeo.

Ni muhimu kutambua ufanisi wa jambo utegemea sana umakini ulionao katika kufuata mwelekeo sahihi.

Ishara kubwa ya kupenda kule unakotaka kwenda/ unakotakiwa kwenda uwa aishii katika kupania na maandalizi ya kutisha bali ubwebwa na umakini pamoja na utayari wa kufuata mwelekeo unaotakiwa.

Kuendelea kudumu katika mwelekeo ulio sahihi bila shaka kuna gharama/ kujigharimu kwingi na hata kuchoka au kuishiwa hivyo kukubali hali hizi zote ni ishara ya kutokuwa tayari kupoteza mwelekeo na kuipenda ndoto yako.

Watu wengi wamekuwa wakitamani mambo mazuri na ya maana katika maisha yao pasipo kutia bidii au kujikita katika mwelekeo sahihi wa kumfikisha katika ndoto yake .

Muhimu kuliko yote kufuata mwelekeo kwa moyo wote hilo ni jambo sahihi na lina husisha mtu binafsi wala alinakufahamiana sana wala kujuana (atanionaje au watanionaje?- uwa wanakuona kama unavyojiona) 

Unapokua makini katika mwelekeo wako inapelekea hatua bora katika maisha yako kwa kuwa neema ya uwezesho inakuwa juu ya maisha yako.

Nini maana ya kupoteza/ kutopoteza mwelekeo?

-          Ni muhimu kujua kupoteza mwelekeo sio kutofanya kitu sahihi, unawezafanya kitu sahihi kabisa lakini ukawa umepoteza mwelekeo (wrong direction).

Mathalani mtu anaweza akaamua kulima mpunga ( kilimo cha biashara) baada ya kuvuna magunia ya kutosha akaanza kuwasaidia wahitaji  baada ya kuingiwa na huruma mwisho bidhaa zikaisha na mtaji ukafa.

Hivyo unaweza kufanya jambo sahihi kabisa lakini ikatokea ukapoteza mwelekeo basi usishangae kuona hicho kitu kikafa au kikienda mwendo wa taratibu sana.

Kutopoteza mwelekeo hauishii kufanya kitu/ jambo sahihi tu bali inahusisha katika namna sahihi + wakati sahihi + watu sahihi.

Hali hii sio lazima pawepo na mlipuko bali ni namna nguvu ya ndani inavyoweza kukuwezesha kuendelea katika mwelekeo sahihi wenye kukupa mpenyo.

Kujua na kufuata mwelekeo sahihi hii ni kwa faida yako na vizazi vyako!

INAITWA SIKU! BARIKIWA

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson………………………………………………………0764 018535