Moja ya vitu vya msingi sana vya kuzingatia ili ufike unakotakiwa kufika ni kuto poteza mwelekeo, ingawa mara nyingine unaweza kuupoteza kwa kujua hama kutojua!
Unapo poteza mwelekeo uweza kusababisha hali ya kuchelewa kufika katika safari yako hama kutofika kabisa! Na muhimu kujua atutimizi ndoto zetu kwakuwa tuna akili nyingi bali kwa kufuata maelekezo yaliyo sahihi.
Baadhi ya vitu vinavyoweza sababisha kupoteza mwelekeo ni ugumu wa safari unao onekana kwenye akili au hali ya kushiba ukasahau njaa.
Mara nyingi mtu anapolianza jambo au safari ( mwenye akili njema) anakuwa ana matarajio fulani au ana matarajio au analengo fulani lakini mambo yote haya yanaweza kutimia tu kama hutopoteza mwelekeo.
Ni muhimu kutambua ufanisi wa jambo utegemea sana umakini ulionao katika kufuata mwelekeo sahihi.
Ishara kubwa ya kupenda kule unakotaka kwenda/ unakotakiwa kwenda uwa aishii katika kupania na maandalizi ya kutisha bali ubwebwa na umakini pamoja na utayari wa kufuata mwelekeo unaotakiwa.
Kuendelea kudumu katika mwelekeo ulio sahihi bila shaka kuna gharama/ kujigharimu kwingi na hata kuchoka au kuishiwa hivyo kukubali hali hizi zote ni ishara ya kutokuwa tayari kupoteza mwelekeo na kuipenda ndoto yako.
Watu wengi wamekuwa wakitamani mambo mazuri na ya maana katika maisha yao pasipo kutia bidii au kujikita katika mwelekeo sahihi wa kumfikisha katika ndoto yake .
Muhimu kuliko yote kufuata mwelekeo kwa moyo wote hilo ni jambo sahihi na lina husisha mtu binafsi wala alinakufahamiana sana wala kujuana (atanionaje au watanionaje?- uwa wanakuona kama unavyojiona)
Unapokua makini katika mwelekeo wako inapelekea hatua bora katika maisha yako kwa kuwa neema ya uwezesho inakuwa juu ya maisha yako.
Nini maana ya kupoteza/ kutopoteza mwelekeo?
- Ni muhimu kujua kupoteza mwelekeo sio kutofanya kitu sahihi, unawezafanya kitu sahihi kabisa lakini ukawa umepoteza mwelekeo (wrong direction).
Mathalani mtu anaweza akaamua kulima mpunga ( kilimo cha biashara) baada ya kuvuna magunia ya kutosha akaanza kuwasaidia wahitaji baada ya kuingiwa na huruma mwisho bidhaa zikaisha na mtaji ukafa.
Hivyo unaweza kufanya jambo sahihi kabisa lakini ikatokea ukapoteza mwelekeo basi usishangae kuona hicho kitu kikafa au kikienda mwendo wa taratibu sana.
Kutopoteza mwelekeo hauishii kufanya kitu/ jambo sahihi tu bali inahusisha katika namna sahihi + wakati sahihi + watu sahihi.
Hali hii sio lazima pawepo na mlipuko bali ni namna nguvu ya ndani inavyoweza kukuwezesha kuendelea katika mwelekeo sahihi wenye kukupa mpenyo.
Kujua na kufuata mwelekeo sahihi hii ni kwa faida yako na vizazi vyako!
INAITWA SIKU! BARIKIWA
Imeandaliwa na:
Cothey Nelson………………………………………………………0764 018535
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni