Jumanne, 6 Oktoba 2020

SEHEMU SALAMA!

 



 

Sehemu salama ni hitaji la kila binadamu mwenye kujielewa na kujithamini, ni kama fedha isivyokuwa na adui bali kila mmoja uhitaji kwa matumizi yake binafsi sawa na halmashauri ya ulimwengu wa fikra zake.

Wakati mwingine ni ngumu kutambua hapa ni sehemu salama au si salama kwa muonekano tu, kwani kuna mahali panaweza kuonekana kuwa ni sehemu salama kwa macho lakini usalama unaonekana hapo kinaweza kuwa ni kichaka cha kuficha uharibifu.

Ni kweli kuna sehemu panawezeka kuonekana kuwa hapo usalama ulizaliwa hapo kutoka na ulinzi mkali na mitambo ya kutosha iliyopo! Lakini uharibu wa siku moja unaweza ukaharibu hiyo sifa ya sehemu hiyo.

Usalama mbali na sehemu/eneo husika pia unaweza kuhuamishia kwa mtu,ukafikiri ninapokaa au kuongea naye siri zako basi maisha yangu yatakuwa salama hali hiyo inaweza kuwa kwa kitambo tu baadae anaweza asiwe salama kwako bali akatumia nafasi hiyo kukuharibu kabisa.

Katika hali ya dunia inavyoaminika na kusema sehemu hii ni salamu au mtu huyu ni salama hali hii inazidi kupungua kutokana na matokeo yasiyotegemea kutokea na kuzidi kuushangaza ulimwenguni,yale ambayo ukutegemea kutokea sasa yanatokea na kuwa ni mambo ya kawaida.

Mathalani wapo waliweka imani kubwa kwa wazazi wao wakitegemea kwao hapo ni sehemu salama lakini mwisho wakatolewa kafara.

Sasa sehemu salama utaipata wapi? Utaijuaje? Ili uweze kuwa salama isiyokuwa na maswali yoyote!

Ili upate usalama wa kudumu na wa uhakika ni lazima urudi kwa yeye aliye asili ya vyote vinavyoonekana na visivyoonekana “ SIR GOD “

Mbali na usalama huu hakuna mahali pengine penye usalama wa kudumu, kwa maana usalama mwingine utengenezwa na akili za wanadamu au mazingira yanayokushawishi kusema sehemu hii ni salama lakini hali hizo zinaweza kubadilika na kuleta maafa.

Ninao ushuhuda wa mtu aliyefikiri kuwa sehemu hii ni salama kwake au kwa mtu ukafikiri kuna usalama kwake lakini baadae akakengeuka kabisa na kusababisha majeraha makubwa ndani ya moyo wa mtu lakini sijawai kuona kwa mtu aliyemfanya Mungu kuwa ni sehemu salama kwake alafu Mungu akawa si sehemu salama kwake.

Ukimfanya Mungu kuwa ni salama kwako naye atakuletea salama yake katika kila jambo na kamwe hawezi kukudhuru kwa kuwa teso la moyo wako ndio teso lake.

“ Nitakuwa pamoja nawe taabuni”

Mfanye Mungu kuwa salama yako hauwezi juta, atakufanya uyafurahie maisha yako kwa maana ni yeye alikutambua kabla ujatokea duniani na kizuri zaidi anampango mwema juu yako.

Hautaji kuchoka katika usalama wako na Mungu bali wewe kubali kufuata maelekezo yake naye atakupa usalama wake na kuzidi katika maisha yako.

“ msikilize uwe salama ndani yake “

INAITWA SIKU! BARIKIWA

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson……………………………………………………0764 018535

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni