Ijumaa, 18 Juni 2021

IACHE ZIADA IWE ZIADA!

 


 Ni vizuri ziada ije kama ziada ili cha msingi kiweze kupata nafasi yake kama cha msingi, maana ukiweka ziada katika nafasi ya msingi ni uhakika kabisa haiwezi kutoshea na uimara wa kukaa hapo unakuwa ni mdogo.

Naam kila kitu kikae katika nafasi yake uwa kuna kuwa na raha fulani ambayo haiwezi kutokea kwa vitu vinapokuwa tofauti na hali hiyo.

Ni muhimu kuacha moja iwe moja ili mbili iwe mbili kuliko kuifanya moja kuwa mbili itasababisha kupoteza sifa ya mbili kuishi kama mbili.

Uwa kila kitu Mungu anachosema uwa ana maana kubwa na sio anajaribu au anabahatisha.

Mungu alisema “ iwe Nuru………………………………ikawa Nuru” Mwanzo 1:3

Ndo mana tusema mchana kwasababu nuru ipo ikitoweka atuwezi kusema mchana tena bali tutaita/kusema ni usiku.

Mungu kama mchora ramani ya dunia na mbingu kwa kujua iki kikae hapa na kwa sababu gani?  na kile kikae pale kitasaidia kitu fulani uwa anapofanya hivyo anakuwa na maana kubwa sana.

Mathalani mtu aliyetengeneza gari na kuweka matairi chini sio juu alikuwa na maana yake mbali na hilo pia ndani ya gari kuna maelekezo yanayopatikana katika “ dash body “ au gari kukosa utulivu kuna mngurumo usio kuwa sawa au mwendo wake kutokuwa sawa kama utakuwa mtulivu utagundua hata baadhi ya matatizo utayaona pale kwenye “dash body”  na kama unaipenda gari yako utaifanyia service pindi unapo ona utofauti kwenye gari lako basi hivyuo utafanya lidumu kwa muda mrefu.

Karibu sana!

Tunapozungumzia ziada, ni vitu ambavyo havina uhusiano wa karibu na uhai wako bali ni vitu vinavyo changamsha nafsi yako pamoja na vionjo vya mwili wako.

Mathayo 6:25-33

25 Kwa sababu hiyo nawaambieni, Msisumbukie maisha yenu, mle nini au mnywe nini; wala miili yenu, mvae nini. Maisha je! Si zaidi ya chakula, na mwili zaidi ya mavazi?

 26 Waangalieni ndege wa angani, ya kwamba hawapandi, wala hawavuni, wala hawakusanyi ghalani; na Baba yenu wa mbinguni huwalisha hao. Ninyi je! Si bora kupita hao?

 27 Ni yupi kwenu ambaye akijisumbua aweza kujiongeza kimo chake hata mkono mmoja?

 28 Na mavazi, ya nini kuyasumbukia? fikirini maua ya mashamba, jinsi yameavyo; hayafanyi kazi, wala hayasokoti

 29 nami nawaambia, ya kwamba hata Sulemani katika fahari yake yote hakuvikwa vizuri kama mojawapo la hayo.

 30 Basi, ikiwa Mungu huyavika hivi majani ya kondeni, yaliyopo leo, na kesho hutupwa kalibuni, je! Hatazidi sana kuwavika ninyi, enyi wa imani haba?

 31 Msisumbuke, basi, mkisema, Tule nini? Au Tunywe nini? Au Tuvae nini?

 32 Kwa maana hayo yote Mataifa huyatafuta; kwa sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote.

 33 Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.

 

mungu anaposema nitafuteni mimi hana maana sasa ushinde kanisani unasoma biblia tuuu na kuomba BALI kuishi kwa kufuata maelekezo yake kwanza kabla ujaamua jambo lolote.

 

Elimu- amesema mkamate sana elimu, japo kiimsingi sio elimu ya kimfumo wa dunia lakini inasaidia katika kuendesha maisha ya kila siku.

Mithali 4:13 Mkamate sana elimu, usimwache aende zake; Mshike, maana yeye ni uzima wako.

 

Kazi- amesema asiyefanya kazi asile

2 Wathesalonike 3:10 Kwa kuwa hata wakati ule tulipokuwapo kwenu tuliwaagiza neno hili, kwamba ikiwa mtu hataki kufanya kazi, basi, asile chakula.

 

kufanya mambo yote ni muhimu sana kwasababu ni agizo la Mungu mwenyewe.

Tatizo linaanza pale unapotanguliza ziada na kuacha cha kwanza. Ni sawasawa na mtu kujali sana matunda pasipo kuutunza mti ili uendelee kukuletea matunda!

 

Wakati mwingine ili uache ziada na kufanya cha kwanza unahitaji ujasiri,kujitoa mwanga ( maamuzi sahihi ) na usipende kujifunza baada ya kukosea kuna gharama ya marekebisho ( mimba, ugonjwa, kutengwa na familia n.k )

Kiukweli ziada inapendwa kuliko kitu kinachosababisha ziada, ni sawasawa na tunda na mti, tunda linaweza kuvutia sana kuliko mti lakini tambua kama hauta utunza mti ujue hautakula matunda siku zote.

Pindi utakapo fanya ziada kuwa ziada hakika utaifurahi hiyo ziada na wala haitakuendesha na hata kupoteza mwelekeo sahihi wa maisha yako.

Na kamwe usikubali nafsi yako au watu wa kushawishi kuwa kuipata ziada unaweza kuipata vitu vyote pasipo wasiwasi.

Mungu ameweka kila kitu kwa utaratibu wake fuata maelekezo yake ufurahishe moyo wa Mungu na yeye atakufurahisha kwa kukupatia mema yake.

Pindi utakapofanya ziada kuwa ni kitu cha msingi kwako hapo uharibifu unakuwa ni maisha yako.

 

INAITWA SIKU! BARIKIWA

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson………………………………………………………0764 018535

 

Ijumaa, 4 Juni 2021

UHITAJI WANGU!

 


WEWE UNAJUA UHITAJI/MAHITAJI YAKO NA MUNGU ANAJUA
UTATUZI WA MAHITAJI YAKO

 

Ni vitu viwili vinavyokamilisha kitu kimoja chenye sura inayoleta maana kamili.

Binadamu kutambua mahitaji yake ni ishara ya kuwa hai ( kuishi ) maana ni maiti tu ambayo haina uhitaji bali watu ndio watakao iamulia nini kifanyike au kisifanyike!

Kama hela au shilingi isipokuwa na pande mbili ni vigumu tu kusomeka hama kuwa kitu kinacholeta thamani kamilifu, na hali kadhalika unapokuwa na uhitaji pasipo kujua utatuzi wake ni mateso! Sawa na samaki kuwa nchi kavu akiangahika kuingia au kurudi majini.

Raha ya swali ni kupata jibu inapotokea jibu alijapatikana linakuwa kikwazo katika akili ya mtu na hali hiyo uweza kubadilisha hata mfumo wa mwili, uweza kujikuta mtu anaumwa pasipo kujua anaumwa nini?

Moja ya kitu kinachoweza kukupelekea kukosa utulivu wa akili ni pale unapokuwa na mahitaji na kushindwa kujua utatuzi wake wa hayo mahitaji.

Ni sifa ya binadamu kujiamini na kuamini uwezo ambao Mungu amempa hivyo upenda sana kutumia akili yake katika mambo yake anayoyafanya katika uwezo wake wote na pindi anapokosa utatuzi wa jibu analolitaka uweza kujikuta moyo wake uko chini na ishara ya kupoteza matumaini pasipo kujua akili  inapokosa majibu, Mungu anamajibu sahihi.

Ni ngumu sana kuamini utatuzi sahihi unatokana na Mungu hasa kwa binadamu au mtu aliyeenda shule angalau akapata shahada ya kwanza, mtu huyu mpaka aweke utatuzi wa jambo lake kwa Mungu basi vitabu vilivyo katika akili yake vimesha chanika sana.

Binadamu wengi wanamweka Mungu katika utatuzi wa pili ( plan B ) na sio mtoa mwelekeo katika kupata ufumbuzi wa yale yanayo kukuta au kukabili.

Na nafasi ya Mungu kwa mwanadam inabidi iwe ya kwanza na sio ya pili kwakua yeye anaijua kesho hata kabla ujaifikia leo!

Maana ni yeye Mungu aliyekupa akili na kukupa neema zake ya kukupa kiwango cha elimu ulichonacho, hivyo nafasi yake isichukuliwe na vitu alivyo vifanya yeye. ( maana Mungu ni Mungu mwenye wivu ).

-          Anataka nafasi yake ibaki kuwa yake!

Mungu anataka ujuzi na maarifa uliyoyapata vitumike katika muongozo wake na sio vyenyewe vifanye nje ya muongozo wake.

Kuna raha na furaha ya kweli pindi unapotambua na kuamini kufanya Mungu ndio mtatuzi wako mkuu, maana yeye alipui wakati mwingine anaweza kufanya nje ya wewe lakini linakuwa ni suruhisho la kudumu na lililobora katika maisha yako.

INAITWA SIKU! BARIKIWA

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson…………………………………………………………………………………….0764 018535