Ijumaa, 4 Juni 2021

UHITAJI WANGU!

 


WEWE UNAJUA UHITAJI/MAHITAJI YAKO NA MUNGU ANAJUA
UTATUZI WA MAHITAJI YAKO

 

Ni vitu viwili vinavyokamilisha kitu kimoja chenye sura inayoleta maana kamili.

Binadamu kutambua mahitaji yake ni ishara ya kuwa hai ( kuishi ) maana ni maiti tu ambayo haina uhitaji bali watu ndio watakao iamulia nini kifanyike au kisifanyike!

Kama hela au shilingi isipokuwa na pande mbili ni vigumu tu kusomeka hama kuwa kitu kinacholeta thamani kamilifu, na hali kadhalika unapokuwa na uhitaji pasipo kujua utatuzi wake ni mateso! Sawa na samaki kuwa nchi kavu akiangahika kuingia au kurudi majini.

Raha ya swali ni kupata jibu inapotokea jibu alijapatikana linakuwa kikwazo katika akili ya mtu na hali hiyo uweza kubadilisha hata mfumo wa mwili, uweza kujikuta mtu anaumwa pasipo kujua anaumwa nini?

Moja ya kitu kinachoweza kukupelekea kukosa utulivu wa akili ni pale unapokuwa na mahitaji na kushindwa kujua utatuzi wake wa hayo mahitaji.

Ni sifa ya binadamu kujiamini na kuamini uwezo ambao Mungu amempa hivyo upenda sana kutumia akili yake katika mambo yake anayoyafanya katika uwezo wake wote na pindi anapokosa utatuzi wa jibu analolitaka uweza kujikuta moyo wake uko chini na ishara ya kupoteza matumaini pasipo kujua akili  inapokosa majibu, Mungu anamajibu sahihi.

Ni ngumu sana kuamini utatuzi sahihi unatokana na Mungu hasa kwa binadamu au mtu aliyeenda shule angalau akapata shahada ya kwanza, mtu huyu mpaka aweke utatuzi wa jambo lake kwa Mungu basi vitabu vilivyo katika akili yake vimesha chanika sana.

Binadamu wengi wanamweka Mungu katika utatuzi wa pili ( plan B ) na sio mtoa mwelekeo katika kupata ufumbuzi wa yale yanayo kukuta au kukabili.

Na nafasi ya Mungu kwa mwanadam inabidi iwe ya kwanza na sio ya pili kwakua yeye anaijua kesho hata kabla ujaifikia leo!

Maana ni yeye Mungu aliyekupa akili na kukupa neema zake ya kukupa kiwango cha elimu ulichonacho, hivyo nafasi yake isichukuliwe na vitu alivyo vifanya yeye. ( maana Mungu ni Mungu mwenye wivu ).

-          Anataka nafasi yake ibaki kuwa yake!

Mungu anataka ujuzi na maarifa uliyoyapata vitumike katika muongozo wake na sio vyenyewe vifanye nje ya muongozo wake.

Kuna raha na furaha ya kweli pindi unapotambua na kuamini kufanya Mungu ndio mtatuzi wako mkuu, maana yeye alipui wakati mwingine anaweza kufanya nje ya wewe lakini linakuwa ni suruhisho la kudumu na lililobora katika maisha yako.

INAITWA SIKU! BARIKIWA

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson…………………………………………………………………………………….0764 018535

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni