Neno “ utumwa “ ni neno lisilovutia kulisikia masikioni mwa mtu, kutokana na uhalisia ulivyo wa mtu anayeishi maisha ya utumwa, kwa asilimia kubwa unaishi maisha usiyoyapenda kwahiyo furaha ya kweli inakuwa adimu katika maisha hayo! Kwa kifupi unalazimika kuishi hivyo sawa na matakwa ya mtu mwingine.
Hivyo tunakubaliana kabisa moja ya teso la utumwa ni kutoishi maisha yake au kuishi vile upendeleavyo bali unaishi kwa matakwa ya mwingine tena bila ridhaa yako.
Ni maisha yaliyobeba hali ya ukatiri na kutojaliwa! Unaishi kwa sababu unapumua na wala si kwa sababu unafurahia maisha.
Pindi unapokuta mtu anaishi maisha haya ( utumwa ) kuwaza kujiua ni kitu kinawezekana tu na utoshangaa kumkuta mtu kajiua, kwa maana utumwa wa akili unaweza kufanana na mtu aliye zezeta kwa maana kwa kiasi kikubwa mtu uishi nje ya utashi wake.
Hapa duniani kuna utumwa wa aina nyingi mathalani kuna utumwa wa pesa,ngono,kazi,akili na mengine mengi.
Lakini ningependa kuangalia UTUMWA WA AKILI,
Hii ni hali ya mtu kushindwa kuitawala akili yake na kujikuta kufanya mambo ambayo kwa uhalisia ayapendi.
Ni maisha ambayo mtu anaishi baada akili yake kukosa jibu liletalo amani litakalo ondoa shida hiyo inayomkabili, utakuta mtu anakubali kufanya jambo moyo,akili na hisia azitaki lakini imemlazimu maana hana namna nyingine.
Akili yako inaweza kushikiliwa na mtu mwengine kutokana na ridhaa yako au nje ya ridhaa yako ikakupelekea kufanya mambo kwasababu tu imekulazimu mbali na hapo maisha yako yatakuwa vinginevyo.
Utumwa wa akili ni mambo yote ambayo akili yako yanakusukuma kutenda nje na utashi wako ili mradi tu maisha yako yawe salama au yaendelee.
Ni vile akili yako imeshikiliwa na vitu vingi vinavyofanya akili yako isiwe na maamuzi yake.
Mbali na hapo kuna utumwa wa akili unaoupenda ( hata pasipo kujua kuwa huu ni utumwa ) ambao unaweza ona uko sawa tu kwa namna ulivyo kwakuwa hauna madhara ya moja kwa moja katika maisha yako ya sasa mathalani akili yako inakupa msukumo wa kupenda kula vitu vyenye mafuta na sukari nyingi pasipo kuwa na tabia ya kunywa maji ya kutosha wala kufanya mazoezi madhara yake utayaona baadae! Hata utumiaji wa madawa ya kulevya unaweza mdogo mdogo lakini baadae ukishakolea hautasita kuuza hata nyumba ili uendelee kutumia madawa ya kulevya.
Na kwa utumwa usioupenda unaweza kujikuta wewe unagombanisha watu kila inapoitwa leo la huyu unalipeleka kwa yule na yule unalipeleka kwa wale ili mradi tu wasielewane.
Kiujumla utumwa wa akili hauna matokeo mazuri katika maisha yako haijalishi unaupenda au haupendi mambo yote unayo yafanya ayatatoa mwelekeo sahihi /bora katika maisha yako.
Njia za kukuwezesha kuondokana na utumwa wa akili;
i) Ongeza maarifa juu ya kitu kinachokutatiza katika akili yako ( hali ya kutafuta ufumbuzi ) na kushindwa kupata mwelekeo na unaweza kuongeza maarifa kutokana na kujisomea vitabu au matumizi sahihi ya mitandao na hata katika watu unaowaamini wanaoweza kukushauri na hatimaye kutoka katika hilo tatizo au hiyo hali.
ii) Anza kufanya tofauti na akili yako ilivyo kamatwa, kama unajua akili yako imejaa uchonganishi basi anza kujenga tabia ya kusema vizuri kwa waliokuuzi na wasiokuuzi.
iii) Mshirikishe Mungu katika hali inayokusumbua akili yako! Yeye aweza kubadilisha na kufanya tena yale yote yaliyoshindikana kwa wanadamu,
INAITWA SIKU! BARIKIWA
Imeandaliwa na:
Cothey Nelson…………………………………………………………..0764 018535
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni