Moja ya kitu kinacho kutambulisha kuwa wewe ni mtu huru ni uwezo wa kufanya maamuzi na kuyasimamia hayo maamuzi sawa na utashi wako!
Na kwa maisha ya kawaida kama binadamu uwa unaongozwa na maamuzi maana kila kitu kina bebwa na maamuzi, ili kufanya hiki na kuacha hiki kinategemea maamuzi ya moyo wako,
Maamuzi ni hali ya kukataa hali fulani na kukubaliana na hali fulani ( kukataa na kukubali )!
Japo yote uitwa ni maamuzi lakini kuna maamuzi ya hiari na yasiyo ya hiari, na maamuzi yanaweza kuweka makao katika akili yako hayo ni maamuzi uliyoyafanya kwa utashi wako na ukaona matunda yake kwakuwa ni maamuzi ya kusifia nafsi yako au kulaumu nafsi yako na sio mtu mwingine mathalani wewe ni binti uliye jitunza akatokea kijana mtanashati akakutongoza nawe kwa utashi wako ukamkubali lakini asikwambia kama ameathirika na UKIMWI baada kuingia maisha ya ndoa ukaamua kujikuta umeambikizwa.
Yote juu ya yote jua kila maamuzi yoyote utakavyo yafanya lazima ujue yana mchango mkubwa katika hatima yako kuifikia au kutoifikia hama kuijenga au kuibomoa.
Hivyo mtu anayeipenda hatima yake utamuona umakini anaoutumia katika kufanya maamuzi uwa amui tu kwa sababu anajisikia kuamua.
Hivyo hauwezi kuwa makini na hatima yako pasipo kuwa makini katika maamuzi unayoamua kila siku.
Wakati mwingine mtu wa namna hii uweza kuhatarisha maisha yake lakini kipindi hicho unamuona anahatarisha maisha yake lakini hapo inawezekana analitumikia/kuishi hatima yake.
Pindi utakapo tembea katika maamuzi sahihi au vigumu sana kuona watu kama kizuizi katika kuitumikia hatima yako iliyowekwa na Mungu.
Ukishindwa kusimamia maamuzi sahihi ni ngumu kuitumikia ndoto/hatima yako.
Kumbuka pindi unapochukua hatua ya hatua ya kuitumikia kuna maisha ya wengi watapona: matasa wanaweza kupakata, wajane wanaweza kupa tumaini jipya na hata yatima wakapata faraja ya kweli ya kudumu lakini hayo yote yanajengwa na umakini katika maamuzi yako.
Ni muhimu ujue ustawi wako uko pale utakapolitumikia/kuishi katika hatima yako, hivyo penda sana kuishi hatima yako kwa kuzingatia hatima yako.
Na ni vizuri hata pale utakapoicha dunia ni vizuri uwe ndani ya hatima yako kuliko uwe nje hatima maana usipoitumikia hatima yako unaweza kupoteza maana ya wewe kuwepo duniani na hata kukupelekea kukosa mbingu.
Unapoamua kuitumikia hatima yako hauhitaji kujiona au kujifananisha na watu wengine maana inaweza kupelekea kujiona mnyonge au uko zaidi yao pasipo kutambua kila mtu utembea katika njia yake, hakuna haja ya mashindano.
Unapoitumikia hatima yako ndio furaha ya Mungu lakini hauwezi kuitumikia hatima yako kama haujawa na usahihi katika maamuzi yako.
Lazima utambue/uone kuna muonekano bora wa maisha kikamilifu nje ya kusimamia hatima yako au ndoto yako!
Uwezi kuwa salama au kuyafurahia maisha kikamilifu nje ya kuisimamia hatima yako!
Kwakuwa unapoitumikia hatima furaha ya bwana inakuwa kama chemichem isiyo kauka katika moyo wako hivyo nguvu zako zinakuwa nyingi.
INAITWA SIKU! BARIKIWA
Imeandaliwa na:
Cothey Nelson……………………………………………….……….0764 018535