Sauti ya Mungu, uwa inabaki kuwa ni sauti yake iliyojaa ukamilifu wa utimilifu wa ahadi zake au yale anayo yasema, lakini kazi inakuwa kwetu kuendelea kuisikia sauti ya Mungu au kuishi ndani ya sauti yake!
Ni vizuri usiishie kusikia tu bali penda kuishi ndani ya sauti yake Mungu.
Waenda kanisani wengi upenda kusikia sauti ya Mungu kama sio kutoka ndani yake basi itoke kwa mtu anayemuamini.
Ni kweli unaweza kusikia sauti ya Mungu na ukatoka katika hali fulani kama sio jambo fulani lakini usiendelee kuishi katika hiyo sauti japo unaweza kuwa muudhuriaji mzuri wa vipindi kanisani hata mchungaji akakupenda sana, mathalani wana Israel walipofika bahari ya sham na kukosa mwelekeo hapo waliisikia sauti ya Mungu kutoka kwa Musa na kupitia katika bahari sham lakini wengi wao baada ya kuvuka hile bahari awakuendelea kuisikiliza/kuifuata kama sio kuiamini sauti ya Mungu.
Na ndio maana sio wote walioweza kuingia nchi ya kanani,
Lazima utambue lengo la Mungu/tamanio la Mungu ni uishi katika sauti yake zaidi sana maisha yako yatawaliwe na sauti yake.
Ni muhimu uishi katika sauti yake ili uweze kuyaishi maisha uliyokusudiwa na sio ya neema tu.
Ni vizuri kutambua kuishi ndani ya sauti ya Mungu haya ni maamuzi ya mtu yaliyo tayari kubeba gharama zitokanazo na maamuzi aliyoyachukua.
Naam kuishi katika sauti yake ni sawa na samaki kuishi majini yaani maisha yaliyo tengenezwa na Mungu wewe uishi humo.
Na jambo lisilopingika usipoishi katika sauti ya Mungu basi utaishi katika sauti ya dunia na dunia itakutesa japo utakuwa unaenda kanisani.
Moja ya kigezo cha kuonyesha unampenda Mungu ni kukubali kuishi katika sauti yake NO MATTER WHAT! Haijalishi nini kinaendelea katika maisha yako.
Kukubali kuishi kwa sauti ya Mungu ni kukubali kuyateketeza maisha na kuwa majivu ili yaweze kuwa manukato kwa Mungu.
Ili uwe na imani thabiti juu ya Mungu na isiyo na shaka kamwe ni muhimu ujifunze kuishi katika sauti ya Mungu.
Nje ya kuishi katika sauti ya Mungu sahau kuishi katika maisha ya ushindi wa kishindo.
Unahitaji kuishi katika sauti yake ili mahali penye giza pawe na nuru, mahali ambapo wengi wanakimbia basi uwepo wako unaweza fanya jangwa kuwa sehemu yenye rutuba ambapo watu wengi watatamani kuwa hapo.
Maana ya wewe kuwepo hapo inakuja mara tu ya wewe kudumu katika sauti ya Mungu maana hapo utafanyika kuwa majibu katika maswali ya wengi.
Usikubali kizuizi chochote kikizuie kuishi katika sauti ya Mungui haijalishi urafiki,mahusiano au chochote bali jua wewe kuishi humo vyote vitarudi vyenye utukufu zaidi vilivyobeba hatima njema katika maisha yako.
Usiogope kutoeleweka na watu wako karibu hama kuachwa kwa watu uliowategemea pindi unapochukua maamuzi ya kuishi katika sauti ya Mungu, Mungu anaweza kukuondolea watu/vitu visivyo stahili ili vije vyenye vya kukufaha zaidi.
Usalama wako unaimarishwa pindi utakapoishi ndani ya sauti yake!
INAITWA SIKU! BARIKIWA
Imeandaliwa na:
Cothey Nelson………………………………………………………………….0764 018535
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni