Unapozungumzia Kumtegemea
Mungu! Hii ni zaidi ya mtoto anavyo mtegemea mzazi au mlezi wake,
Kwani mzazi anaweza
kuwa makini sana kumwangalia mtoto wake lakini asiweze kumpa uzima hama afya
pindi anapoumwa! Lakini Mungu anaweza kufanya hivyo vyote.
Karibu!
Kuna kusema mimi
namtegemea Mungu na Mungu kusema huyu
ananitegemea mimi! Hizi ni kauli mbili ambazo zimebeba ukamilifu wa jambo
husika.
Japo kwa kiasi kikubwa
maarifa uliyonayo kuhusu Mungu ndio yanaweza kukupa nguvu ya kusema ya mimi na
mtegemea Mungu au lah!
Hatuwezi sema
tunamtegemea kwasababu watu wanasema tunamtegemea au wanamtegemea Mungu bali ni
dhamira yako iliyobeba uhalisia ndiyo yenye nguvu ya kuonyesha kuwa wewe unamtegemea
Mungu au lah!
Zipo tafsiri nyingi
nzuri tu zinazoelezea nini maana ya kumtegemea Mungu lakini mimi ningesema hivi
kwa kifupi kumtegemea Mungu ni Mungu kuishi katika akili yako!
Ubora wa utendaji wa
watu wengi utambulishwa na utendaji mzuri unaotokana na akili ya mtu hivyo
hivyo utendaji mbovu/mbaya wa mtu utambulisha matumizi yasiyo sahihi ya akili
ya mtu.
Tukienda mbali kidogo
tunaweza kufananisha akili katika maisha ya mwanadamu ni sawa uskani katika
gari na endapo ukaweza kuutawala uskani vizuri basi gari litaenda katika
mwelekeo mzuri nje hapo unaweza kusababisha
matatizo katika uendeshaji wako.
Ni kweli kuna mambo
unahitaji kutumia akili za kawaida tu na yakaenda lakini sio kila jambo linakuwa
na majibu kutokana na akili uliozaliwa nazo.
Kama kweli unatamani
kuliona tabasamu la Mungu basi hakikisha akili yako inaishi katika kauli ya
Mungu.
Maisha ya kumtegemea
Mungu ndio maisha ambayo Mungu anayatarajia kuona tunaishi humo.
Makutano yetu na Mungu
yanakuwa ni rahisi ni pale tu tunapoamua maisha ya kumtegemea maana hapo tutapata
majibu ya maswali yetu na kupata nguvu mpya kila itwayo leo.
Kama kweli unadhamira
ya dhati ya kutoka katika hali ya manung’uniko au lawama ni pale tu akili yako
ijifunze na kuishi kwenye kauli ya Mungu.
Lazima uone kwa fahari
ya Mungu kwake inakuwa kubwa pindi unaizoesha akili yako kumtegemea Mungu.
Ni muhimu utambue kuwa
hakuna namna moja ya kumtegemea Mungu bali ni namna anavyojifunua katika akili
yako na kukupa namna ya kuishi sawa na maongezi yake.
Kuishi uku ukimtegemea
Mungu sio maisha ya mateso bali ni maisha ya kuishi kwa ajili ya faida ya
Mungu.
Maisha ya kumtegemea
Mungu ni maisha ya kuongezeka nguvu hata nguvu, maarifa hata maarifa na kuweza
kuwa bora kwa wakati uliopo na ujao.
Unapokubali kuishi
maisha ya kumtegemea Mungu unapata neema ya kuwaona watu na kuwathamini kama
Mungu anavyowaona kwa kuwa unakuwa na akili yake basi hapo unakuwa na akili
yake.
INAITWA SIKU! BARIKIWA
Imeandaliwa na:
Cothey Nelson…………………………………………………………0764 018535