Ijumaa, 28 Januari 2022

KUMTEGEMEA MUNGU

 



Unapozungumzia Kumtegemea Mungu! Hii ni zaidi ya mtoto anavyo mtegemea mzazi au mlezi wake,

Kwani mzazi anaweza kuwa makini sana kumwangalia mtoto wake lakini asiweze kumpa uzima hama afya pindi anapoumwa! Lakini Mungu anaweza kufanya hivyo vyote.

Karibu!

Kuna kusema mimi namtegemea Mungu na Mungu kusema  huyu ananitegemea mimi! Hizi ni kauli mbili ambazo zimebeba ukamilifu wa jambo husika.

Japo kwa kiasi kikubwa maarifa uliyonayo kuhusu Mungu ndio yanaweza kukupa nguvu ya kusema ya mimi na mtegemea Mungu au lah!

Hatuwezi sema tunamtegemea kwasababu watu wanasema tunamtegemea au wanamtegemea Mungu bali ni dhamira yako iliyobeba uhalisia ndiyo yenye nguvu ya kuonyesha kuwa wewe unamtegemea Mungu au lah!

Zipo tafsiri nyingi nzuri tu zinazoelezea nini maana ya kumtegemea Mungu lakini mimi ningesema hivi kwa kifupi kumtegemea Mungu ni Mungu kuishi katika akili yako!

Ubora wa utendaji wa watu wengi utambulishwa na utendaji mzuri unaotokana na akili ya mtu hivyo hivyo utendaji mbovu/mbaya wa mtu utambulisha matumizi yasiyo sahihi ya akili ya mtu.

Tukienda mbali kidogo tunaweza kufananisha akili katika maisha ya mwanadamu ni sawa uskani katika gari na endapo ukaweza kuutawala uskani vizuri basi gari litaenda katika mwelekeo mzuri nje hapo unaweza kusababisha  matatizo katika uendeshaji wako.

Ni kweli kuna mambo unahitaji kutumia akili za kawaida tu na yakaenda lakini sio kila jambo linakuwa na majibu kutokana na akili uliozaliwa nazo.

Kama kweli unatamani kuliona tabasamu la Mungu basi hakikisha akili yako inaishi katika kauli ya Mungu.

Maisha ya kumtegemea Mungu ndio maisha ambayo Mungu anayatarajia kuona tunaishi humo.

Makutano yetu na Mungu yanakuwa ni rahisi ni pale tu tunapoamua maisha ya kumtegemea maana hapo tutapata majibu ya maswali yetu na kupata nguvu mpya kila itwayo leo.

Kama kweli unadhamira ya dhati ya kutoka katika hali ya manung’uniko au lawama ni pale tu akili yako ijifunze na kuishi kwenye kauli ya Mungu.

Lazima uone kwa fahari ya Mungu kwake inakuwa kubwa pindi unaizoesha akili yako kumtegemea Mungu.

Ni muhimu utambue kuwa hakuna namna moja ya kumtegemea Mungu bali ni namna anavyojifunua katika akili yako na kukupa namna ya kuishi sawa na maongezi yake.

Kuishi uku ukimtegemea Mungu sio maisha ya mateso bali ni maisha ya kuishi kwa ajili ya faida ya Mungu.

Maisha ya kumtegemea Mungu ni maisha ya kuongezeka nguvu hata nguvu, maarifa hata maarifa na kuweza kuwa bora kwa wakati uliopo na ujao.

Unapokubali kuishi maisha ya kumtegemea Mungu unapata neema ya kuwaona watu na kuwathamini kama Mungu anavyowaona kwa kuwa unakuwa na akili yake basi hapo unakuwa na akili yake.

INAITWA SIKU! BARIKIWA

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson…………………………………………………………0764 018535

Maoni 1 :

  1. Titanium Strength - Table games - The Tithron
    The Tithron medical grade titanium earrings is a game-playing card game with 5 titanium nitride coating players. It titanium linear compensator is played on a standard deck. When titanium armor you place any value on it, you can play toaks titanium as a total

    JibuFuta