Ijumaa, 11 Februari 2022

MUNGU ASIPOTOA DUNIA ITATOA?

 



Uhitaji moja ya ishara ya kuwa kiumbe hai, japo kunatofauti ya uhitaji lakini hali ni ileile tu, UHITAJI.

Naam ili kupata kitu lazima mchakato upitie katika usaidizi wa Mungu au Dunia kufanikisha jambo unalolihitaji.

Hivyo ili upate kitu ni lazima dunia ikupe au Mungu akupe.

Luka 4:3 Ibilisi akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, liambie jiwe hili liwe mkate.

 4 Yesu akamjibu, Imeandikwa ya kwamba mtu hataishi kwa mkate tu.

 5 Akampandisha juu, akamwonyesha milki zote za ulimwengu kwa dakika moja.

 6 Ibilisi akamwambia, Nitakupa wewe enzi hii yote, na fahari yake, kwa kuwa imo mikononi mwangu, nami humpa ye yote kama nipendavyo.

 7 Basi, wewe ukisujudu mbele yangu yote yatakuwa yako.

 8 Yesu akajibu akamwambia, Imeandikwa, Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake.

 

Japo dunia au mbingu imepanga kukupa lakini kila utawala unapokupa kitu chake unakuwa una matakwa yake ni muhimu utambue matakwa ya kila utawala kabla ujaingia mahali ambapo utajuta kwa nini upo hapo!

 

Ili mradi tu unahitaji basi jua dunia na mbingu ziko mbele yako zikisubiria maamuzi yako.

 

Kumbukumbu la Torati 30:15 Angalia, nimekuwekea leo mbele yako uzima na mema, na mauti na mabaya;

 

Maamuzi yako ndio ukombozi wako! Basi utaamua nini ndivyo itaamua hatma yako na sio unavyotaka.

 

Kila kitu alichonacho au alichonacho mtu kina pande mbili Mungu ametoa au dunia imetoa, na tunapozungumzia dunia sio lazima utumie nguvu za giza bali yenyewe kutokana na kanuni zake iliyo asili yake.

Mathalani ibrahimu, Ishmael mwanae ambaye dunia ilitoa na isaka naye ni mwanae lakini Mungu ndiye alitoa………………..japo wote ni watoto lakini ni mfumo miwili tofauti!

Hivyo sio kuwa na kitu tu bali iko kitu umepokea kutoka katika mikono ya dunia au mbingu hilo lina maana sana hasa katika ustawi na mstakabali wako.

Na umuhimu utambue kila kitu kitoe au kikupe kina utaratibu wake kinategemea sana akili yako na namna yako ili kukufuata.

Usipokuwa mwangalifu dunia inaweza kukupa ukafikiri Mungu amekupa ukamshukuru yule asiyestahili na aliyekupa akigundua anaweza kukichukua.

Siri kubwa ya kukipata kitu chochote ni umakini wa kusikiliza, kitu gani umekipa uzito wa ndani wa kumsikiliza hivyo ukamsikiliza vizuri Mungu basi utavipata vyake hivyohivyo ukiisikiliza vizuri dunia na kuifuata basi utavipata vile vilivyo vyake.

Na muhimu utambue dunia inapotoa uwa inalenga kwa faida yake hata kama baadae utapata maumivu, dunia yenyewe haijali ili mradi imetimiza lengo lake lakini Mungu anapotoa inakuwa kwa ajili ya ustawi wako wa leo, kesho na milele mathalani na mzazi mwenye akili njema anapokubali kunyima ili mwanae asome.

Ni muhimu iwe dhahiri pindi Mungu anapofanya basi iwe ni kweli Mungu amefanya na dunia inapofanya basi ijulikane tu ili ushuhuda wako uweze kudumu.

Ikumbukwe unaweza kuwadanganya wote lakini sio nafsi yako wala Mungu/dunia mathalani mtu anapotafuta muujiza dunia inaweza fanya maajabu yake na Mungu anaweza fanya muujiza hivyo sio kila muujiza chanzo chake ni Mungu.

Ili uweze kuvipata vitu vya Mungu lazima ukubali kutulia na kukubaliana na dhoruba na vitisho vya dunia maana dunia upenda kukuonyesha jinsi gani uwezi kutoka ulipo bila kumsikiliza au kufuata njia zake.

Kwa harakaharaka dunia inatoa vitu vyake haraka na kwa muonekano mwepesi “ easy come easy go” na kukunawirisha kwa kitambo baadae ukuacha kwa kuwa ilishatimiza haja yake.

Lakini Mungu “ Alfa na Omega” akianza na wewe hauwezi kukuacha labda wewe ndio umuache lakini ujue ukimwacha ni kwa hasara yako.

 

INAITWA SIKU! BARIKIWA

 

Imeandaliwa na:

 

Cothey  Nelson…………………………………………………………0764 018535

 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni