Katika dunia kuna vitu vinasemekana kuwa na nguvu mathalani maji,upepo na hata matetemeko ya ardhi hata vinaweza kuzamisha au kuondoa vitu kama sio kudondosha fahari ya dunia: mathalani majengo makubwa na hata milima mikubwa lakini haijafikia nguvu iliyojificha ndani ya PENZI!
Niseme tu, mahali penye penzi ni mahali ambapo ni makimbilio ya kila kitu: wanyama, binadam na hata viumbe vingine.
Mahali penye penzi unaweza usione ajabu chizi,mgonjwa aliyepalalaizi au kuvunjika akapona na kuwa msaada kwa wengine.
Ndomana hata wanyama wakihisi mahala hapa pana upendo hawatapenda kuondoka mahali hapo miguuni pa mwenye upendo.
Ni kubaliane kuwa upendo sio kucheka,kuongea wala kula pamoja tu bali pia kunauhusisha kukubali na kuingia gharama kwa ajili ya kuhakikisha furaha ya mtu haipotei wala aipungui bali inaongezeka siku baada ya siku.
Ni kweli mahali penye kutimiza uhitaji wa watu/viumbe, viumbe au watu uweza kuja ili kukizi uhitaji wao mathalani nzi upenda kutoa kwenye kidonda lakini awezi kuweka makazi hapo lakini mahali penye upendo hata mtu akishapata uhitaji uweza kuyaamisha maisha yake na kuweka kituo mahali penye upendo.
Ni pende kusema hitaji kubwa la binadamu ni PENZI na wala sio kitu chochote kinachoonekana kuwa kina kifaa hama kuvutia.
Mtu mwenye akili uweza kukataa pesa na kulipokea penzi litokalo katika moyo wa mtu aliyobeba dhamira njema japo kuwa anaweza kuwa na matakwa mengi lakini tulizo la moyo wake lazima lianzie katika penzi la dhati.
Ukweli unaweza kuwa na vitu vingi lakini vikapukutika lakini sio PENZI mahala penye penzi hilo lenyewe alijali pesa au kitu kipo au akipo lenyewe lipo tu,
Karibu!
PENZI KAMA CHOMBO CHA MAREKEBISHO SALAMA,
Kama kuna kitengo kigumu basi ni hiki kitengo cha marekebisho!
Siko tofauti na kutumia adhabu kali ilete mabadiriko au marekebisho kwa mtu hususa tabia yatokee.
Lakini iko njia rahisi na yenye uhakika inaitwa NGUVU YA PENZI:
Katika njia hii hakuna kitu kikashindwa kurekebishwa haijalishi itachukua muda gani lakini hipo siku mabadiriko yatadhihirika siku moja.
Na ukitumia njia hii vizuri uwezi kushindwa kupata matunda uliyo yakusudia hasa yaliyo mema.
Unapoonyesha penzi katika tatizo la mtu unavumbua thamani yake na kuonyesha namna ya kuitunza ili thamani isipotee.
Mahali penye pendo la kweli hata tabia ikiwa ngumu kiasi gani mahali penye upendo endelevu mabadiriko yatatokea.
Nguvu ya penzi inayo uweza kumuonyesha mtu majukumu yake na kuyatekeleza kwa uaminifu hata bila ya usimamizi bali nguvu inampa kujisimamia.
Na penzi linapozidi linamfanya mtu azidi kujibidisha pasipo kuangalia vikwazo vyovyote bali anapoona mahali penye mashaka na yeye uaminifu uweza kupungua na bidii upotea kabisa hatimaye kushindwa kuendelea mbele.
Mahusiano yanatunzwa na nguvu ya penzi na sio uchumba wala ndoa bali vyote ubebwa na mwamvuli wa penzi maana anapopungukiwa mtu au kukosa inakuwa sio yeye amekosa bali unajiona wewe ndio umekosa kwakuwa unajiona wewe katika maisha yake.( unavaa viatu vyake ).
Unapoongea na mtu katika penzi uwa mtu anaona deni/na kujipa wajibu ili kujibu penzi analoliona katika sura yako ya kidhihirishwa kwa maneno yako.
INAITWA SIKU! BARIKIWA
Imeandaliwa na:
Cothey Nelson…………………………………………………………….0764 018535
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni