Watu upenda kusema “ tajiri na mali zake na maskini na watoto wake”! sijajua kwanini?
Karibu!
Ni jambo la fahari au linapendeza kuona mtu ana miliki mali zake na pengine tunaweza enda mbali zaidi sio kuwa na mali tu bali ni kuwa na mali zile unazozitaka sawa na ndoto yako hapo furaha kwake uwa inazidi.
Tukubaliane tu kuwa na mali ni kitu kimoja na kuzifurahia mali ni kitu kingine pia tunaweza kwenda mbali kidogo pindi unapoanza kupata mali unaweza kuwa na furaha na baadae unaweza kukosa kuzifurahia hizo mali kwanini tuendelee mbele?
Ni kweli unapokuwa na mali unakuwa ni mlango wa kupata mali zingine lakini endapo itakapotokea hizo mali kuanza kupungua basi hata zile zilizopo unakosa ujasiri nazo.
Kila kitu kinachotokea kina kuwa na sababu ya kutokea au kuwepo!
Hivyo hali ya mtu anayemiliki mali kukosa kuona thamani ya mali zake inaweza kusababishwa na sababu zifuatazo:
Ugonjwa, watu wengi waliokumbwa na maradhi mbalimbali uweza kukosa radha ya kuwa na mali hasa vijana wengi wanaweza kuwa na msongo sana katika akili zao pindi anapojua awezi tena kutumia mali zake kwa sababu ya ugonjwa alionao, mpaka anajuta kwanini alitia bidii nyingi kuvitafuta na wakati sasa hana fahari nazo, labda kwa watu wazima wenye familia japo wanaweza kukosa matumaini ya kupona ila wanaweza wasiweze kujuta sana kwa kuwa kila mtu ataonja mauti na kuugua ni moja njia ya kuicha dunia ( kufariki ) hivyo uweza kusema watoto wake wanaweza kuzitumia.
Kukosa mtoto, hili ni jambo ambalo limekuwa janga kubwa kwa familia nyingi za kiafrika kwa wale walikosa neema ya kuwa na watoto,limekuwa likiwaumiza wengi hata kama wanandoa wanaishi kwa amani kwa waliowengi pengo la kutokuwa na watoto linabaki hivyohivyo hata ukiziangalia mali zao pindi utakapoondoka duniani ujui nani atakaye zichukua inawezekana kuchukuliwa na watu usiowapenda kumiliki jasho lao,
Pia unaweza kuwa na watoto lakini unaweza ukakosa hata mmoja wa kumuacha kumiliki mali zako kama unavyotaka, hivyo unyonge unatawala nafsi yako wakati mwingine unafikiri hata usingewaleta dunia, japo wakati mwingine unaweza kujipa matumaini labda siku zinavyozidi kubadiliki wanaweza kuwa sawa vile unavyoona.
Chanzo kisicho sahihi, tunajua wote kama sio wengi tunategemea kudra za Mungu ili kupata hizo mali lakini viko vyanzo visivyo sahihi vinaweza kusababisha kupata hizo mali mathalani imani za kishirikina na wizi pia ni njia zitumikazo kupata mali isivyo halali ili kukamilisha na kupata ustawi na kushamiri wa mali zako;
Imani za kiushirikina, pindi unapopata mali katika njia hii bila shaka kuna maisha unaweza kuishi uku nafsi yako ikikosa uhuru wa kweli au yanaweza kukunyima raha hata usifurahie mali zako mathalani kuishi kwa kunywa damu za watu au kufanya mapenzi na wanyama mpaka kufa kwako, ni kweli mwanzoni unaweza kutimiza bila shaka kwakuwa unatafuta lakini baadae hayo masharti yanaweza kukuchosha na kuwa mzigo kwako hata unapoangalia unaweza usione fahari ya kuendelea na hizo mali wakati nafsi yako inateseka au kudharirika zaidi sana akili yako inaona giza lisilo na kikomo.
Wizi, unapopata mali kwa njia hii uwa kunauwezekano mkubwa kukosa amani nazo maana haujua nini kitatokea pindi jambo lako litakapo gundulika, utakuwa katika fungu gani? Unaishi nazo uku ukiwa binafsi ukifikiri endapo siri hiyo itagundulika je! Utakuwa uraiani au utakuwa jela,jibu la swali hili litakutesa katika maisha yako.
Thamani ya mali unaipata kwa kumiliki pamoja mtoa mali ( Mungu )!
INAITWA SIKU! BARIKIWA
Imeandaliwa na:
Cothey Nelson…………………………………………………………….0764 018535
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni