Ni jambo jema na zuri kuwepo kwa mabadiliko hasa chanya katika mambo mbalimbali yanayoendelea katika ulimwengu huu, kwasababu hayo mabadiliko ndiyo yanapelekea mafanikio/ maendeleo mengi katika dunia tuliyonayo ya kianza katika jamii husika na hatimaye kuenea ulimwenguni mathalani maendeleo ya sayansi na teknolojia yalivyo pelekea urahisi wa mawasiliano na hata kurahisisha kwa usafirishaji wa watu pamoja na bidhaa kutoka sehemu moja na kwenda sehemu nyingine na faida nyingine nyingi ambazo unapoziona unaona maajabu ya akili ya Mungu kwa mwanadamu.
Kwa Afrika kwa asilimia kubwa tunashukuru Mungu kwa sababu tulivyokuwa jana sio tulivyo leo hasa kwa upande wa mavazi , mavazi ya enzi hizo sio tunayovaa sasa japo tunayafurahia na kumshukuru Mungu kwa hilo ingawa yameboreshwa hata kupitiliza maana siku hata siku mitindo inakuja ya hatari zaidi na hata material ( malighafi ) ya tofauti tofauti kulingana na wazo ( idea ) ya mtengenezaji ( designer ) wakati mwingine nguo za kulalia zinakuwa za kutokea hapo na wanyoshea mikono mafundi “ designer “ wetu! Hakika kweli wakati tunaenda nao vizuri
Ni kweli jana na leo zote ni siku ila zinatofautiana kwa majira yake kama sio kwa tarehe.
Natambua tunamtambua umuhimu wa mkunga baada ya kumsaidia mjamzito kujifungua salama.
Na mwanafunzi wanatambua umuhimu wa mwalimu baada ya kufaulu maana sio rahisi kwa mwanafunzi aliyefeli akamtafuta mwalimu na kumwambia asante kwa kunifundisha!
Japo ni vizuri kumkumbuka mwalimu hata kama ujafanikiwa kufanya vizuri maana kuna maarifa fulani umeyapata kutoka kwake.
Ni muhimu sana kutokusahau jana kwasababu imekuja leo, kwasababu sio vitu vyote ulivyojifunza jana kuwa leo havitatumika tena.
Kwani hata chakula kilichobaki jana kinaweza faa leo ( baadhi ya familia ) ni muhimu tu ukiandae vizuri kitumike leo tena na kwa asilimia kubwa chakula kilicho lala uitwa kiporo na wengine ukifurahia sana.
Ni muhimu utambue mambo yako ya jana ambayo upaswi kwenda nayo leo na vilevile yako ya leo haupaswi kuyakataa kwa kuwa yanaweza yasikifae ila yaka mfaa mwingine na mengine yanaweza yasiwafae wote ya kaja na kupita.
Naam hata utandawazi unaokuja leo tusisahau asili yetu ya jana! Kwa kuwa kupitia utandawazi unaweza kuona mambo mbalimbali hivyo usione kila kitu kinachoonyeshwa na kupitia mtandao basi kinafaa kuwa sehemu ya maisha yako.
Wako watu wanakosoa jamii yao kwakuona kutembea katika asili yake ni kupotoka au kutoheshimu hadhi yake lah! Katika mabaya unayo yaona yako mema usiyoyaona au uliyoyasahau.
Tambua ni hao watakao kukumbatia na kukusitiri na hata kukuzika pindi utakapo pumzishwa katika nyumba yako ya milele na sio wale unaowafuata utamaduni wao!
Haijalishi kama unawajua kiasi gani japo uko mbali ( utandawazi ) jua lako litabaki kuwa lako tu na hapo awatajali kuwa wewe ni shabiki wa utamaduni wao au la!
Sio kila kitu kinacholetwa mezani kwako ukachukua na ukala lazima uangalie kwa umakini je! Hicho chakula akitaathiri afya yangu ulimbukeni usikutese.
Ni vizuri unapofanya jambo lazima liwe jema machoni pa jamii yako hasa likiwa lililo chanya kwako.
Unapokuwa kijijini ishi kama mwanakijiji na unapokuwa mjini basi ishi kimjini basi hapo utakuwa bora kwa jamii yote zaidi sana mpende Mungu.
INAITWA SIKU! BARIKIWA
Imeandaliwa na:
Cothey Nelson………………………………………………………………………..0764 018535
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni