Ni kawaida tu, kibinadamu kila mtu yeyote pindi anapojingalia kwenye kioo, upenda kujiona yeye na wala sio mtu anayefanana na yeye na wala sio yeye!
Katika mambo ambayo yanayomfurahisha Mungu kama sio kumpendeza ni pindi anapomuona mwanadam anapenda ajione yeye katika kila kitu kinachohusu maisha yake afya, uchumi na mambo yote ya kijamii.
Pindi anapojiona yeye katika maisha ya mwanadamu basi hapo udhihirisha kuwa huyo ni mali yake hata bila kusema kwa mtu husika kuwa yeye ni mali ya Mungu.
Lengo kubwa la Mungu kukufanya ni kutaka utambue na kumpa heshima kama Mungu na wala sio kitu kingine.
Ndomana anapoona utendaji wako mkubwa wa akili katika mambo yanayo kukabili upenda kukuacha ili utukufu wake usichanganyike na uwezo wa kibinadamu.
Namna nyepesi ya kumruhusu Mungu atawale/ahusike na shida hama jambo lako ni kutokuwa na nia ya kuwa komoa watu bali kuhakikisha Mungu anaonekana na kuwa unakuwa kwa faida yake.
Mtihani mkubwa unakuja pale namna gani Mungu anataka aonekane katika kile unacho/kinachokukabili inawezekana kazi pengine wewe ungependa kuendelea hapo ili wale wanaokuchukia wakuone, hivyo ukawa unafunga na kuomba katika hali hiyo lakini Mungu pengine anataka uondoke hapo ili utukufu wake uonekana huko unakokwenda! AU kuna mabaya yatakuja kwenye ofisi hiyo ambayo yanaweza kuweka maisha yako rehani.
Mathalani,Daudi alikuwa anaomba ili mwanae apone na aliacha hata kula ili amshawishi Mungu afanye kitu kwa ajili ya kunusuru uhai wa mwanae lakini Mungu akutaka kuonekana kwa namna hiyo ambayo sawa na matakwa yake.
Watu wengi wanakata tama kwa kutojua namna gani Mungu anataka aonekane katika yale yanayo kukabili, mathalani wengine walitegemea afanye leo lakini Mungu alipendezwa kufanya kesho kutwa hivyo akili ya Mungu na mtu zikatofautiana, naye akashindwa kukubaliana na tofauti hiyo.
Pindi unapotambua namna gani Mungu anataka ajionyeshe kwa watu kutokana na yale yanayo kukabili ushindi unakuwa ni haki yako mathalani wanaisraeli walipokuwa wakipigana vita Mungu aliwapa ushindi kwa namna mbalimbali sawa na namna yake au alivyokuwa anataka wakati mwingine waliimba na ushindi ukapatikana na mara nyingine Musa kwa kunyoosha mkono Israel walishinda n.k
Ukitaka kushindana na Mungu au kuchelewa katika hatua yako basi tafuta namna yako tofauti na mpango wake au alivyokusudia.
Moja ya kitu ambacho Mungu anataka akione yeye kwako pindi unavuka salama au kushinda vita ni watu wamuone yeye katika huo ushindi na sio wewe kutaka wakuone wewe! Mungu anaweza kubatili huo ushindi au usijirudie tena katika hatua inyofuata.
Unahitaji kujua Mungu anataka kujiona yeye katika maisha yako na sio mtu mwingine ili aweze kuwa Mungu kwako kwelikweli na kuchukua shida yako pamoja na kuwa furaha yako katika siku zote za maisha yako.
Unahitaji kujua Mungu anataka aonekane katika jambo lolote linalo kukabili hivyo kumruhusu aonekane kama anavyotaka ni kumshawishi atende .
Muhimu katika yote, ni vizuri utambue pindi Mungu atakavyojionyesha bila shaka nawe UTAONEKANA TU! Usiwe na haraka.
INAITWA SIKU! BARIKIWA
Imeandaliwa na:
Cothey Nelson…………………………………………………………….0764 018535
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni