Pindi unasikia neno hili “ Mungu Anajua” uwa huna mashaka hata kidogo na moyo wako unasema ni KWELI, maana hakuna kificho mbele za Mungu....maana yeye anajua hata utawaza nini baada hilo la sasa unalowaza!
Kujua ni uhuru na ushindi wa kufanya mambo mengi na kuto kujua utumwa usio wa hiari unaokupeleka mahali pengine usipotaka kwenda!
Naam!
Ni kweli umeshiba leo lakini Mungu anajua pia utahitaji kula kesho.
Ni kweli una nguvu leo maana ni kijana lakini Mungu anajua kesho yako maana nguvu zako zitaisha maana utakuwa ni mzee.
Karibu!
Moja ya kitu kinachosababisha watu kukata tamaa hama kukosa matumaini ni kutojua kuwa Mungu anajua na anaelewa vizuri sana.
Katika dunia tuliyonayo wako watu baada ya kuachwa na wapenzi wao wanafikiri kujiua ndio dawa ya kuficha aibu yao, pia wako watu walioachishwa kazi au madili yao kuharibiwa na hata kupelekea kucheleweshwa mipango yao, wengi wamekata tamaa na kuhisi wana mikosi na wanaona kama Mungu AJUI!
Ni muhimu utambue kuwa akili yako inapokosa majibu haina maana kuwa Mungu amekosa majibu, ikiwa maisha yako umeyakabidhi kwake jua kila jambo linalotokea limebeba hatima kubwa njema katika maisha yako. ( Mungu yeye anajua mwisho tangu mwanzo )!
Wakati mwingine uwa tunalia kwasababu atukutegemea yatokee yale yalitokea hasa kwa yale yanayoonekana mabaya lakini kwa Mungu sio kitu au jambo la kushangaza kwake.
Na muhimu tutambue utofauti wa akili zetu na Mungu ndo maana yeye anaitwa Mungu na sisi wanadamu.
Pia kuna wakati mambo yanaweza kutokea katika maisha yako ukajua Mungu yuko na mambo mengine kabisa wala akufikirii wewe, hivyo unaweza kuzidi kuwa chini kwa kukosa mwelekeo uliosahihi.
Uwa Mungu anajua sio kwa kuwa una matatizo tu bali anajua hata jambo lingine likikutokea na namna gani ya kuwa salama hapo.
Ni maisha mawili haya ukiishi, kuishi katika mazingira uku ukijua Mungu anajua kinachoendelea na wewe hama ajui kitu au chochote kinachokuhusu wewe, wakati mwingine ni kweli inaweza kukupa wazo hilo kutokana na mazingira lakini ukweli haupo hivyo.
Katika maisha haya kuna uwezesho mkubwa wa Mungu wa ajabu pindi unapojua katika hali ngumu inayokuzunguka Mungu anajua utatoka vipi!
Hauhitaji maombi mengi sana ili utoke ulipo kuwa bali unahitaji akili yako ikubaliane kuwa Mungu anajua na uwe tayari kufuata njia zake ili utoke hapo ulipo.
Nikubaliane tu, uwa ni ngumu tu kujua hasa kama Mungu anajua kinachoendelea katika maisha yako!
Yesu “ mimi ndimi ufufuo na uzima “-lazaro.
Yohana 11:1 Basi mtu mmoja alikuwa hawezi, Lazaro wa Bethania, mwenyeji wa mji wa Mariamu na Martha, dada yake.
2 Ndiye Mariamu yule aliyempaka Bwana marhamu, akamfuta miguu kwa nywele zake, ambaye Lazaro nduguye alikuwa hawezi.
3 Basi wale maumbu wakatuma ujumbe kwake wakisema, Bwana, yeye umpendaye hawezi.
4 Naye Yesu aliposikia, alisema, Ugonjwa huu si wa mauti, bali ni kwa ajili ya utukufu wa Mungu, ili Mwana wa Mungu atukuzwe kwa huo.
5 Naye Yesu alimpenda Martha na umbu lake na Lazaro.
6 Basi aliposikia ya kwamba hawezi, alikaa bado siku mbili pale pale alipokuwapo.
7 Kisha, baada ya hayo, akawaambia wanafunzi wake, Twendeni Uyahudi tena.
8 Wale wanafunzi wakamwambia, Rabi, juzijuzi tu Wayahudi walikuwa wakitafuta kukupiga kwa mawe, nawe unakwenda huko tena?
9 Yesu akajibu, Je! Saa za mchana si kumi na mbili? Mtu akienda mchana hajikwai; kwa sababu aiona nuru ya ulimwengu huu.
10 Bali akienda usiku hujikwaa; kwa sababu nuru haimo ndani yake.
11 Aliyasema hayo; kisha, baada ya hayo, akawaambia, Rafiki yetu, Lazaro, amelala; lakini ninakwenda nipate kumwamsha.
12 Basi wale wanafunzi wakamwambia, Bwana, ikiwa amelala, atapona.
13 Lakini Yesu alikuwa amenena habari ya mauti yake; nao walidhania ya kuwa ananena habari ya kulala usingizi.
14 Basi hapo Yesu akawaambia waziwazi, Lazaro amekufa.
15 Nami nafurahi kwa ajili yenu kwamba sikuwako huko, ili mpate kuamini; lakini na twendeni kwake.
16 Basi Tomaso, aitwaye Pacha, akawaambia wanafunzi wenziwe, Twendeni na sisi, ili tufe pamoja naye.
17 Basi Yesu alipofika, alimkuta amekwisha kuwamo kaburini yapata siku nne.
18 Na Bethania ilikuwa karibu na Yerusalemu, kadiri ya maili mbili hivi;
19 na watu wengi katika Wayahudi walikuwa wamekuja kwa Martha na Mariamu, ili kuwafariji kwa habari ya ndugu yao.
20 Basi Martha aliposikia kwamba Yesu anakuja, alikwenda kumlaki; na Mariamu alikuwa akikaa nyumbani.
21 Basi Martha akamwambia Yesu, Bwana, kama ungalikuwapo hapa, ndugu yangu hangalikufa.
22 Lakini hata sasa najua ya kuwa yo yote utakayomwomba Mungu, Mungu atakupa.
23 Yesu akamwambia, Ndugu yako atafufuka.
24 Martha akamwambia, Najua ya kuwa atafufuka katika ufufuo siku ya mwisho.
25 Yesu akamwambia, Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima. Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa anaishi;
Usihisi mambo yanaweza kukuchanganya basi ukajua na Mungu yana mchanganya sawa na akili yako inavyo waza bali Mungu uwa anaona njia mahali panapoonekana giza.
Unapoyaendea mambo/kuyakabili mambo huku ukijua kuwa Mungu anajua na hali hii bado nitatoka salama na ushindi ni haki yangu.
Katika mazingira yeyote upaswi kujiweka chini lazima roho yako iwe na nguvu kwa kuwa MUNGU ANAJUA ULIPO NA UNAPOENDA!
Mashaka wala uwoga sio fungu lako!
INAITWA SIKU! BARIKIWA
Imeandaliwa na:
Cothey Nelson..............................................................................0764 018535
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni