Jumamosi, 26 Machi 2022

UELEWA SAHIHI UKUPELEKEA MAAMUZI SAHIHI!

 



( Sio kila kitu unavyokiona ndivyo kilivyo )

Watu usema uelewa ( maarifa ) ni nguvu, kweli ni nguvu inayoweza kukupeleka kufanya maamuzi sahihi.

Unapo pambana na jambo pasipo kutafuta muhafaka wa njia itakayokupa utatuzi wa sahihi wa jambo hilo bila shaka hali hiyo inaweza kukupelekea kuchoka kama sio kujichosha.

Wakati mwingi jambo lolote linalokupata au kukutokea kutokana na uelewa sahihi uliojikita katika fahamu zako unajikuta ujasiri na kujiamini unakuwa fungu lako ( endapo ukijitambua ).

Moja ya kitu kinachopelekea kufanya maamuzi mabaya ni ujuaji ( kujiona unajua na hakuna wa kukushauri ).

Ni muhimu utambue maadam unaishi basi jua unayahitaji maarifa ( uelewa ) ili kuleta  umaana wa kuwepo na kuishi kwa furaha!

Na muhimu ujifunze maadam upatapo nafasi ya kufanya maamuzi basi ujue wakati au miaka hairudi nyuma.

Ni muhimu uchelewe kufanya maamuzi ukitafuta maamuzi sahihi ili ya kuweka katika nafasi nzuri usalama wa kesho yako.

Ni vizuri upate uelewa sahihi ni kwa ajili ya faida yako na jamii inayokuzunguka.

Hata kama jambo linafanyika kwa namna uliyozoea tambue majira yanabadilika namna ya kuyafanya jambo hilo linaweza kubadilika na kukupa matokeo tofauti.

Mathalani katika mambo ya Mungu…tunamuona musa aliambiwa mara ya kwanza upige mwamba kasha ukatoa maji na mara nyingine aliambiwa ahuamuru mwamba utoe maji ila yeye aliupiga tofauti na maagizo aliyoambiwa/aliyopewa.

Tambua majira yanapita hivyo kukosea kosea kunaweza kufanya kuchelewa kufikia pale ulipokusudiwa, ni vizuri utambue uelewa sahihi ukuwezesha kule ulikokusudiwa ukiwa kamili katika akili na neema kamilifu.

Hali ya kupenda kufanya maamuzi kabla ujatafuta uelewa sahihi wa jambo husika unaweza kukutana na mtihani wa chuo kikuu wewe ukajibu kidarasa la saba ukadhani maadamu ni maandishi yameandikwa kwenye karatasi nyeupe basi majibu yake yatakuwa sawa tu pasipo kujua hayo maswali ni kiwango/kidato gani? Ili uweze kujibu sawa na kidato/kiwango husika.

Ni vizuri kutambua kuwa sio kila maamuzi unaweza kuyafanya matokeo yake yatapotea/kusahaulika kirahisi tu bali yako maamuzi ambayo matokeo yake yanaweza kugharimu maisha yako yote mathalani unapofanya maamuzi ya kuua na ukapatikana na hatia maisha yako yanaweza kuishia jela au kunyongwa hadi kufa.

Uwa atufanyi maamuzi kwa kuangalia watu wanataka tufanye hivyo bali kwa kujali na kuthamini ustawi wa hatma iliyoko ndani yetu.

Ni muhimu kufanya maamuzi kwa kuboresha kesho yako na sio kutimiza matakwa ya mwili wako!

INAITWA SIKU! BARIKIWA

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson……………………………………………………………………0764 018535

Ijumaa, 11 Machi 2022

SIONI THAMANI YA MALI ZANGU

 



Watu upenda kusema “ tajiri na mali zake na maskini na watoto wake”! sijajua kwanini?

Karibu!

Ni jambo la fahari au linapendeza kuona mtu ana miliki mali zake na pengine tunaweza enda mbali zaidi sio kuwa na mali tu bali ni kuwa na mali zile unazozitaka sawa na ndoto yako hapo furaha kwake uwa inazidi.

Tukubaliane tu kuwa na mali ni kitu kimoja na kuzifurahia mali ni kitu kingine pia tunaweza kwenda mbali kidogo pindi unapoanza kupata mali unaweza kuwa na furaha na baadae unaweza kukosa kuzifurahia hizo mali kwanini tuendelee mbele?

Ni kweli unapokuwa na mali unakuwa ni mlango wa kupata mali zingine lakini endapo itakapotokea hizo mali kuanza kupungua basi hata zile zilizopo unakosa ujasiri nazo.

Kila kitu kinachotokea kina kuwa na sababu ya kutokea au kuwepo!

Hivyo hali ya mtu anayemiliki mali kukosa kuona thamani ya mali zake inaweza kusababishwa na sababu zifuatazo:

Ugonjwa, watu wengi waliokumbwa na maradhi mbalimbali uweza kukosa radha ya kuwa na mali hasa vijana wengi wanaweza kuwa na msongo sana katika akili zao pindi anapojua awezi tena kutumia mali zake kwa sababu ya ugonjwa alionao, mpaka anajuta kwanini alitia bidii nyingi kuvitafuta na wakati sasa hana fahari nazo, labda kwa watu wazima wenye familia japo wanaweza kukosa matumaini ya kupona ila wanaweza wasiweze kujuta sana kwa kuwa kila mtu ataonja mauti na kuugua ni moja njia ya kuicha dunia ( kufariki ) hivyo uweza kusema watoto wake wanaweza kuzitumia.

Kukosa mtoto, hili ni jambo ambalo limekuwa janga kubwa kwa familia nyingi za kiafrika kwa wale walikosa neema ya kuwa na watoto,limekuwa likiwaumiza wengi hata kama wanandoa wanaishi kwa amani kwa waliowengi pengo la kutokuwa na watoto linabaki hivyohivyo hata ukiziangalia mali zao pindi utakapoondoka duniani ujui nani atakaye zichukua inawezekana kuchukuliwa na watu usiowapenda kumiliki jasho lao,

Pia unaweza kuwa na watoto lakini unaweza ukakosa hata mmoja wa kumuacha kumiliki mali zako kama unavyotaka, hivyo  unyonge unatawala nafsi yako wakati mwingine unafikiri hata usingewaleta dunia, japo wakati mwingine unaweza kujipa matumaini labda siku zinavyozidi kubadiliki wanaweza kuwa sawa vile unavyoona.

Chanzo kisicho sahihi, tunajua wote  kama sio wengi tunategemea kudra za Mungu ili kupata hizo mali lakini viko vyanzo visivyo sahihi vinaweza kusababisha kupata hizo mali mathalani imani za kishirikina na wizi pia ni njia zitumikazo kupata mali isivyo halali ili kukamilisha na kupata ustawi na kushamiri wa mali zako;

Imani za kiushirikina, pindi unapopata mali katika njia hii bila shaka kuna maisha unaweza kuishi uku nafsi yako ikikosa uhuru wa kweli au yanaweza kukunyima raha hata usifurahie mali zako mathalani kuishi kwa kunywa damu za watu au kufanya mapenzi na wanyama mpaka kufa kwako, ni kweli mwanzoni unaweza kutimiza bila shaka kwakuwa unatafuta  lakini baadae hayo masharti yanaweza kukuchosha na kuwa mzigo kwako hata unapoangalia unaweza usione fahari ya kuendelea na hizo mali wakati nafsi yako inateseka au kudharirika zaidi sana akili yako inaona giza lisilo na kikomo.

Wizi, unapopata mali kwa njia hii uwa kunauwezekano mkubwa kukosa amani nazo maana haujua nini kitatokea pindi jambo lako litakapo gundulika, utakuwa katika fungu gani? Unaishi nazo uku ukiwa binafsi ukifikiri endapo siri hiyo itagundulika je! Utakuwa uraiani au utakuwa jela,jibu la swali hili litakutesa katika maisha yako.

Thamani ya mali unaipata kwa kumiliki pamoja mtoa mali ( Mungu )!

INAITWA SIKU! BARIKIWA

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson…………………………………………………………….0764 018535