Ni kweli unaweza usijue kwanini hilo limekupata lakini hilo jambo linasababu yake kuja kwako na kukupata.
Kulia ni jambo linalotokea katika maisha ya kila mwanadamu kutokana na jambo husika lakini huzuni nyingi na ukiwa ulioambata na machozi unakuwa ni kwasababu ya kukosa kujua kwanini jambo hili limekupata wewe na wala sio mwingine.
Kutoka uko liliko toka na kukufikia wewe sio bure ila linakuwa na sababu ya kukufikia wewe! Haijalishi lengo lake kuwa zuri au baya,
Litakuwa tayari lina ramani ya kukufikia au sababu ya kuja kwako!
Inaweza kuwa ni sababu iliyo katika uovu au ni sababu inayotengeneza kesho yako yenye baraka.
Naam kila kitu kinacho kufuatilia kina kuwa na sababu ya kukufuatilia unaweza usiijue lakini uwa kuna sababu ya kukufuatilia pia inaweza kuwa imetumwa na mtu au umeisababisha mwenyewe kikufuate kwa kujua hama kuto kujua.
Laiti tungejua kwasababu gani haya yanakupata au yanatokea kwa asilimia kubwa tusingeweza kujilaumu au kulaumu watu zaidi ya kutafuta namna ya kutoka hapo au kusubiri kwa furaha hadi wakati sahihi wa ustawi wako.
Sio kila kitu ambacho unakiona kuwa ni kizuri na unasababu ya kukipata na endapo ikatokea ukakikosa basi ukaishia kulaumu na hata chuki kuzaliwa ndani yako hali hii sio sawa.
Mambo mengi yanakaa kwa muda mrefu au yanachelewa kwasababu tunakuwa atujui kwanini yanatokea au kusudi la kutokea.
Mara nyingi yanapotokea mambo mabaya tunakuwa ni watu wakujilaumu au kuwalaumu watu na pengine watu uweza kwenda mbali zaidi hata kumlaumu Mungu lakini mwisho unaweza kumshukuru Mungu, mathalani unaweza kuwa na mtu kwenye mahusiano na ikatokea umempenda sana hata ukasema hata ikitokea yeye amekufa basi utajiua ili mapenzi yakaendelee peponi ( sijui uko kama mapenzi yanaendelea ) naam ikatokea mahusiano yamekatika/yameisha ukapatwa na bumbuazi /butwaa usijue lakufanya bali machozi yako yakawa chakula chako usiku na mchana, naam ukaone bora ulie siku nzima kuliko ule chakula maana akipandi, muda si mrefu ukapata habari kwamba yule mtu uliyempenda sana amefriki na ugonjwa wa ukimwi muda si mrefu ( na ulikuwa ujui kama ameathirika ) bila shaka baada kupata pumziko kwa muda bila shaka unaweza kushusha pumzi kuanza kuona thamani ya chakula na kuanza kula.
Sio kila kitu unacho kosa kikupe sababu ya LAWAMA.
Ni kweli mambo mengi yanayo kutokea yanakuwa hayana taarifa za kufanya uweze kujiandaa, ila jambo husika linakuwa katika ratiba yake ambayo wewe uwezi jua kwanini hili lakini wewe unaweza usijue na pengine ukajiona vile unavyojiona sasa.
Lakini katika yote kikubwa jipe nafasi ya kutulia mbele za Mungu, hakikisha nafsi yako inatulia mbele zake kwa ukimya wa tofauti, na hapo fumbo linaweza kutatuliwa na hata kupata amani ya kustahimili kipindi hicho.
Bila shaka ufumbuzi au sababu ya jambo hilo linaweza kuwa kwa njia ya ndoto , sauti mawazoni mwako hama sauti itokayo na neno la Mungu ndani yako.
Usipotafuta sababu zaidi ya kutaka nani wa kumlaumu hauwezi kukata tamaa wala kumbebesha mtu lawama na hapo utaona njia na hatimaye kupita hapo salama.
Unapojua sababu ya jambo hapo uwezi kuona kama kunakuchelewa wala kushindwa.
Kujua sababu ya tatizo/jambo hapo ndipo chanzo sahihi na jicho sahihi na jibu la uhakika katika kutoka pale ulipo.
Kila jambo linalo kutokea uwa lina maana yake lakini shida ni pale tu ile maana! Na endapo ukajua hiyo maana basi inakuwa sio shida tena.
Ni sawa na mlango ulifungwa kwa muda mrefu kwa kukosa funguo lakini ikatokea ukaiona fungua yake basi hapo unakuwa sio mlango uliofungwa tena mbele ya macho yako!
INAITWA SIKU! BARIKIWA SANA
Imeandaliwa na:
Cothey Nelson…………………………………………………..……….0764 018535