Jumamosi, 16 Julai 2022

YAELEWE MAJIRA YAKO!

 



UNDERSTANDING YOUR SEASON!

Usipoyaelewa majira kuna uwezekano mkubwa wa kupishana na ustawi wako,

Unapoishi pasipo kuelewa majira yako unakuwa sawa na:

(a)    Kwenda baharini na uku ukitegemea kumuona mamba akipiga mbizi! Ambacho ni kitu kisichowezekana

(b)   Kupanda mahindi na uku ukitegemea kuvuna maharage.

(c)    Kukaa karibu na bank na uku ukitegemea kuna siku hela zitatoka bank na kuja nyumbani kwako.

(d)   Kuimba mwenyewe chumbani kwako ukafikiri uko studio na kutega sikio au kutazamia nyimbo yako itapigwa radioni.

(e)    Kukaa na sehemu wanaopika chakula kizuri na ukategemea kupitia harufu yake utashiba hata bila ya kukiweka mdomoni.

Kuna maisha unaweza kuishi nje ya utaratibu wa kimungu endapo tu kama hauta kuwa makini na majira.

Wapo watu wamekatisha maisha yao kwa kukosa kuyaelewa majira yao vizuri katika majira ya kuvumilia wenyewe walifikiri ni majira ya kupata hivyo kwa kushindwa kuvumilia walipoteza maisha yao.

Ni muhimu kutambua majira maana ni ramani ya Mungu kwa maisha ya mtu binafsi, kwa kuwa majira yako ya kunyamaza yanawezekana kuwa ni majira ya mwingine kusema.

Unapokosea kuielewa ramani unaweza ukajikuta upo kariakoo badala ya kuwa America!

Moja ya sifa ya mtu anayetambua majira yake kiufasaha hawezi kuweka kinyongo au kisasi na mtu au watu bali furaha ya Mungu ina ushika moyo wake.

Yusufu “ sio ninyi mlionileta hapa “!

Mwanzo 45:1 Hapo Yusufu hakuweza kujizuia mbele yao wote waliosimama karibu naye. Akapiga kelele, na kusema, Mwondoeni kila mtu mbele yangu. Wala hakusimama mtu pamoja naye, Yusufu alipojitambulisha kwa nduguze.

 2 Akapaza sauti yake akalia, nao Wamisri wakasikia. Watu wa nyumba ya Farao nao wakasikia.

 3 Yusufu akawaambia ndugu zake, Mimi ndimi Yusufu; baba yangu angali hai bado? Wala ndugu zake hawakuweza kumjibu, maana waliingiwa na hofu mbele yake.

 4 Yusufu akawaambia ndugu zake, Karibuni kwangu; basi, wakakaribia. Akasema, Mimi ni Yusufu, ndugu yenu, ambaye mliniuza kwenda Misri.

 5 Basi sasa, msihuzunike, wala msiudhike nafsi zenu, kwa kuniuza huku; maana Mungu alinipeleka mbele yenu kuhifadhi maisha ya watu.

Niseme tu unapoamua kutembea katika majira sahihi tegemea kupingwa/kutotiwa moyo na hata kunenewa maneno mabaya na magumu kwakuwa majira yako anayoyaelewa ni Mungu tu na wala sio jirani wala rafiki hama mzazi au mchungaji.

Unahitaji kusimamia majira yako vizuri ili uweze kumpendeza Mungu zaidi ya kufurahisha majirani/watu kwa kitambo kidogo baadae wakakusahau.

Na uzuri wa kitu sio kuwa nacho tu bali ni kuhakikisha umekielewa, hivyo unaweza kuwa huru  katika kukitumia vizuri.

Moja ya kitu kitakachoweza kuondoa vikwazo katika jambo lolote utakalolifanya ni kuelewa majira yako, kuwa wakati huu natakiwa ufanye nini na nisifanye nini hapo utafika kwa haraka na kwa wepesi.

Majira wakati mwingine yanaweza kukupelekea kuchukua maamuzi ambayo yatahatarisha maisha yako kwa kiasi kikubwa kwa kuwa ni ramani inayoonyesha upitie hapo ili ufikie kwenye utukufu mwingine.

  Ni muhimu kujua uliko ili ujue unako kwenda “

INAITWA SIKU! BARIKIWA SANA.

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson………………………………………………………………….0764 018535

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni