Katika ukuaji wa mtoto kuna hatua anazotakiwa kupitia ili kuweza kutembea na hatimaye kukimbia na kila hatua ina umuhimu wake……. Naam ili aweze kutembea ni muhimu aweze kusimama kwanza!
Ni hali ya kawaida kibinadamu, kuvutiwa na jambo jema au kitu kinachooneka katika muonekano wa kupendeza macho ( kuvutia ) mathalani unapoona nyumba nzuri ya kisasa ukadhani imeshushwa tu ikawa hapo, pasipo kujua walianza na msingi kabla ya kufikia hapo au katika ukamilifu wake.
Mathalani pindi unapokuwa na ndoto ya kuwa mfanya biashara mkubwa, lakini mawazo na uwoga wa kupata hasara unaweza kukupa hofu ya kuanza hiyo biashara hivyo ukabaki kufikiri tu.
Kuna watu awapendi misukosuko katika hatua ya awali pasipo kujua misukosuko ndio inajenga uimara wao wa kesho, na msingi bora wa kesho unategemea misukosuko ya leo.
Kwa mwanamke mwenye akili na mwenye mapenzi ya kweli kwa mwanae uwa anakaa uku anamategemeo kuwa miezi kadhaa ikifika utegemea kumuona mtoto wake akitembea mwenyewe na pindi anapoona anachelewa kutembea inaanza kumsumbua moyoni mwake hivyo uweza kumfanyisha mazoezi na hata kumnunulia vitu au kumpa visaidizi ili aweze kumsaidia kutembea ( mapenzi ya mama kwa mtoto wake ).
Karibu katika somo!
Usiogope kusimama maana huo ndio mwanzo wa kutembea:
Inawezekana kabisa ni kweli ujawahi kusimama mwenyewe katika jambo lolote, hata unalolifikiria unahisi utaanguka au watu watakuonaje maana walizoea kuona katika hali fulani tu! Usiogope ni kama mtoto anapotoka katika hatua ya kutambaa na kuanza kusimama japo anaweza kuanguka mara nyingi lakini mwisho atasimama na hatimaye akaanza kutembea naam mwisho kabisa akakimbia na hapo furaha mzazi uongezeka.
Ni majira tu yakifika tu ni viungo vyenyewe vinampa msuko wa kufanya jambo sawa na hatua aliyonayo hata kama yeye ayuko tayari viungo vitamsukuma.
Ujue mtoto anapoanza kutembea uwa hana reference/ pa kufuata bali yeye ufanya kile anachokiona na uwa hana wazo nitadondoka na kuumia japo hali hizo zinaweza kujitokeza/kumpata bali yeye ujisikia raha anapotembea na hata akianguka bado haimkatishi tamaa ya kusimama tena na kukimbia.
Naam unapotaka kuisimamia ndoto yako lazima ujiangalia ndani yako na sio nje yako bali ujue wewe ndio mwenye dhamana ya maisha yako na wala sio mtu mwingine.
Ni muhimu kutambua hali uliyonayo sasa ( nguvu ) sio hali hiyo utakayo kuwa nayo kesho ( uzee ) lazima uandae kesho yako kuwa na kicheko kuliko leo usije ukasema” Ningelijua Ningelifanya”
Kumbuka wanaosema umechelewa au hautaweza ndio watu hao hao watakaokusifia utakapofikia kwenye kilele chako, ukiishi katika maneno yao hauwezi kuiona nuru yako ya kesho.
Unapoufurahia mchana lazima ujiandae kwa usiku ili uendelee kufurahia maana huo ndio ukamilifu wa siku.
INAITWA SIKU! BARIKIWA
Imeandaliwa na:
Cotrhey Nelson………………………………………………………….0764 018535
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni