Ijumaa, 23 Septemba 2022

MWISHO WA MCHEZO;

 



Ni mwisho wa mchezo tu ndio unaamua shangwe iendelee au ikatike!

Mwisho wa mchezo ndio unaobeba kicheko au kilio cha kudumu na wala sio mwanzo au katikati ya mchezo!

Naam mwanzo wa jambo ni vigumu kutambua/kugundua mwisho wa jambo utakuaje? Japo unaweza kukisia kutokana uwezo/uzoefu ulionao.

Laiti tungepata neema ya kujua mwisho wa jambo na amini tungekuwa makini katika mwanzo wake hama kuacha kabisa kama utaona mwisho si mzuri.

Wakati mwingine namna ulivyoanza inaweza isiwe na nguvu sana lakini mwisho ukawa ni mwisho wa kishindo kama sio wa neema/ustawi, kuna wakati unaweza kuanza kwa kusuasua/pasipo uhakika wa kufika lakini mwisho ukafika ushuhuda unakuwa na nguvu hata kusahau magumu uliyoanza nayo.

Wakati mwingine watu wengi wanaishi kana kwamba maisha yao yako mikononi mwao, wenyewe tahadhari na umakini katika maisha yao unakuwa haupo.

Kuna maisha ya mtu anaishi kwa uhuru zaidi pasipo kujali hiki wala kile kwasababu ya fedha anazozipata ili kuishi anavyoona yeye pasipo kujua kuna giza au mtelelemko mkali kule anako kwenda au anako endea.

Ni kweli kuna wakati, mathalani mechi zinapocheza uchezaji au timu moja inaweza onekana kuwa inazidiwa na hata ufanisi wake unaweza usionekane lakini mwisho wa mchezo endapo ikaibuka mshindi hivyo hapo watu wanaweza kusahau makosa waliyo yaona uwanjani na kujiunga katika kusherekea ushindi uliopatikana.

Pia kuna uwezekano mkubwa kwa watu wanaokuangalia wanaweza wasikuelewe na wakati mwingine wanaweza kukuona unapoteza muda lakini mwisho kitu chako kinapoanza kuonekana na hata kushika mizizi basi hapo wataanza kukuelewa mathalani mwimbaji wakati mwingine anapoanza kuimba wakati huo uweza kuonekana kama kero na wakati mwingine anaweza kuonekana kuwa anapoteza muda ni bora ungesoma na baadae hata ukawa mtaalamu wa jambo Fulani kuliko kupoteza muda kufanya jambo lisilo na tija lakini mwishoni utapoendesha maisha yako katika uchumi mzuri basi hapo wataanza kuona maana ya wewe kuimba.

Na neema inapoanza kushuka kwako usipende kuishi kana kwamba ni kipofu kana kwamba baada ya leo hakuna kesho ni muhimu utambue hipo kesho na anayeijua Mungu tu, usifanye/usiishi katika dunia kana kwamba ulishirikishwa katika uumbaji wake na unahati miliki ya maisha yako.

Unapaswa kujua watu watakuona wa maana endapo tu kuwa mwisho wako utabaki kuwa kileleni katika maisha yenye ushindi mzuri.

Usiishi maisha ambayo hauta tamani kuishukuru jana yako ukajutia na hata ukatamani hata isingekuwepo maana mwisho umekuacha pasipo mwelekeo wa maana wa kutoa mwanga wa kesho yako au jamii inayokuzunguka kufaidika na uwepo wako.

Ni kweli maadamu unaishi utakiwi kukata tamaa lakini ukumbuke kwa kila fursa unayoipata ujue una sababu ya kuitendea haki, hivyo usipoitumia vizuri ujue kuna gharama utaingia inaweza kuwa ya muda tu au muda mrefu pasipo kikomo.

Mwisho wa mchezo unaweza kukupa maana ya wewe kuwepo duniani au ukakosa maana ya w ewe kuwepo hapa duniani, chochote Mungu anapofanya kwako ni kwa ajili yake na wala sio kwa ajili yako tu binafsi.

INAITWA SIKU! BARIKIWA SANA

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson………………………………………………………………….0764 018535

Ijumaa, 9 Septemba 2022

MAONGOZI YAKE (MUNGU) NDIO UBORA WAKO!



Kadili unavyodumu katika maongozi yake ndivyo hivyo ubora wako unavyo thibitika!

Ubora ni uhitaji wa dunia!

Ø  Makazini ( jeshini, bandarini, viwandani na mashuleni )

Ø   kanisani

Ø   mwenza

Hata mbingu inataka mtu aliye bora!

Ndo maana ukienda kuomba kazi basi wata mwitaji mtu aliye bora na sio mtu anayefanya kazi tu bali kazi yenye viwango ( ueledi na bidii ) ili wapate tija katika biashara zao, ndo mana utoa vigezo ukifuatilia kwa umakini vigezo hivyo utajua hapo utafutwa mtu aliyebeba ubora na sio ubusy usio na tija katika shughuli zao.

Boss urelax pindi anapompata mtu ambaye anafanya kazi katika ubora anakuwa na imani naye pasipo mashaka kazi itaenda na faida itapatikana.

Naam…………hivyo tunakubaliana kuwa ubora ni chaguo la watu wenye akili, sababu ziko nyingi kwa nini mwenye akili achague kilichobora lakini hizi mbili zinaweza kutupa mwanga,

i.                    Tija

Kitu chochote kilicho bora uwa kinakuwa na ufanisi mkubwa katika utendaji wake, uwa akisumbuisumbui mara kwa mara.

ii.                  Kina dumu

Unaweza kukitumia kwa muda mrefu mpaka ukasahau kama kunakifaa umekiweka kwa sababu kina uimara hivyo utatumia muda mrefu kifaa au mashine yako kwakuwa umeweka kifaa chenye ubora.

Muhimu ni kutambua kuwa ni Mungu ndiye anayekutengeneza ili uwe bora na ufae katika jamii, pia unaweza kupitia mikono ya watumishi na ukawa bora.

Kuwa bora sio kitu rahisi japo kinawezekana kwa kuwa mwezeshaji yupo anasubiri utayari wako ili akutengeneze uwe kiumbe cha ajabu.

Ni vizuri ujue endapo usipokubali maongozi yake unaweza kufahamika sana lakini usiwe bora.

Naam ubora sio mtelezo bali ni matokeo ya kukabiliana na mambo yanayoweza kutingisha imani.

Matendo 21:13 (10-13)………………….

10 Basi tulipokuwa tukikaa huko siku nyingi, nabii mmoja jina lake Agabo akashuka kutoka Uyahudi.

 11 Alipotufikia akautwaa mshipi wa Paulo, akajifunga miguu na mikono, akasema, Roho Mtakatifu asema hivi, Hivyo ndivyo Wayahudi wa Yerusalemu watakavyomfunga mtu mwenye mshipi huu, nao watamtia katika mikono ya watu wa Mataifa.

 12 Basi tuliposikia haya, sisi na watu wa mahali pale, tukamsihi asipande kwenda Yerusalemu.

13 Ndipo Paulo alipojibu, Mnafanya nini, kulia na kunivunja moyo? Kwa maana mimi, licha ya kufungwa, ni tayari hata kuuawa katika Yerusalemu kwa ajili ya jina lake Bwana Yesu.

 

“ Ndipo Paulo akajibu, mnafanya nini, kulia na kunivunja moyo?..............

Ni muhimu ujue Mungu anakufanya bora kwa ajili ya utukufu na sio ulete shida katika jamii.

Ø  Nitalijenga kanisani langu na milango ya kuzima haitaishinda!

Naam ni kawaida tu, ili uweze kupata moyo wa mtu kwa urahisi ni kukubali kuishi katika maongozi yake ( mzazi, boss,mme)- maneno yake.

Na kufanya mambo mengi nje ya maelekezo/mwelekeo au dira yake ( Mungu ) ni kupoteza muda na kuuchosha mwili.

Luka 10:40-42

40 Lakini Martha alikuwa akihangaika kwa utumishi mwingi; akamwendea, akasema, Bwana, huoni vibaya hivyo ndugu yangu alivyoniacha nitumike peke yangu? Basi mwambie anisaidie.

 41 Bwana akajibu akamwambia, Martha, Martha, unasumbuka na kufadhaika kwa ajili ya vitu vingi;

 42 lakini kinatakiwa kitu kimoja tu; na Mariamu amelichagua fungu lililo jema, ambalo hataondolewa.

 

Endapo ukitaka kuona mtu anaambatana na wewe siku zote au haukauki kinywani mwake ni kuishi kwa kufuata maongozi yake.

Yohana 8:29

Naye aliyenipeleka yu pamoja nami, hakuniacha peke yangu; kwa sababu nafanya sikuzote yale yampendezayo.

 

Kwa namna unavyojigharimu kuishi katika maongozi yake yeye atatengeneza maisha yako ili yawe bora.

Namna unavyotoa macho kuangalia mambo yake naye ndio anavyotoa jicho lake kuangalia maisha yako.

Kuishi katika maongozi ya Mungu kunahitaji MAAMUZI BINAFSI!

Joshua 24:15

Nanyi kama mkiona ni vibaya kumtumikia Bwana, chagueni hivi leo mtakayemtumikia; kwamba ni miungu ile ambayo baba zenu waliitumikia ng'ambo ya Mto, au kwamba ni miungu ya wale Waamori ambao mnakaa katika nchi yao; lakini mimi na nyumba yangu tutamtumikia Bwana.

“…………….chagueni hivi leo mtakaye mtumikia;

Hakuna ushoga/ubest/urafiki katika hili.

NAWEZAJE KUISHI KATIKA MAONGOZI YAKE:

Mbali ya kuwa na kiu/shauku juu ya Mungu pia kuna maarifa unatakiwa uwe nayo.

i.                    Ipende hatma yako

mbali na kuiombea hatma yako na kufanya mambo mengine lakini usisahau kuwa hiyo hatma inavumbuliwa katika kuishi ndani ya maongozi ya Mungu.

Wagalatia 1:16

alipoona vema kumdhihirisha Mwanawe ndani yangu, ili niwahubiri Mataifa habari zake; mara sikufanya shauri na watu wenye mwili na damu;

 

  alipoona vema kumdhihirisha mwanawe ndani yangu,…………………….”

Hatma ni jambo/kitu alichokiweka na Mungu ndani yako ( ramani ya Mungu inayoongoza maisha yako ) ili dunia iwe salama na dunia haiwezi kuwa salama nje maongozi yake.

Usipojua njia/mwelekeo utapotea/kupotezwa na watu wasio na nia njema kwako au walio na maslahi yao.

ii.                  Tamani kuona jicho la Mungu linakufurahia.

Jicho la Mungu pindi linapokutazama linaweza kuwa sura mbili kukufurahia au kukuhuzunikia, tamani kufanyika kicheko cha Mungu na atamani kukuona wakati wote.

Hapa duniani jitahidi sana kuishi maisha yatakayoleta furaha katika macho ya Mungu na sio kwa wanadamu.

Mathayo 10:32-33

32 Basi, kila mtu atakayenikiri mbele ya watu, nami nitamkiri mbele za Baba yangu aliye mbinguni.

 33 Bali mtu ye yote atakayenikana mbele ya watu, nami nitamkana mbele za Baba yangu aliye mbinguni.

 

Pindi Mungu anapotupia jicho kwako au kukuangalia aseme kweli ana mtoto anayejigharimu kuishi kwa ajili yake,

Na kufurahisha jicho la Mungu lazima uwe tayari kwa gharama:

a)      Matakwa binafsi kupoteza/kukiondoa kipaumbele chako.

I wafalme 17:10-13,9

9 Ondoka, uende Sarepta, ulio mji wa Sidoni, ukae huko. Tazama, nimemwagiza mwanamke mjane wa huko akulishe.

 10 Basi, akaondoka, akaenda Sarepta; hata alipofika langoni pa mji, kumbe! Mwanamke mjane alikuwako akiokota kuni; akamwita, akamwambia, Niletee, nakuomba, maji kidogo chomboni nipate kunywa.

 11 Alipokuwa akienda kuleta, akamwita akasema, Niletee, nakuomba, kipande cha mkate mkononi mwako.

 12 Naye akasema, Kama Bwana, Mungu wako, aishivyo, sina mkate, ila konzi ya unga katika pipa, na mafuta kidogo katika chupa; nami ninaokota kuni mbili ili niingie nijipikie nafsi yangu na mwanangu, tuule tukafe.

 13 Eliya akamwambia, Usiogope; enenda ukafanye kama ulivyosema; lakini unifanyie kwanza mkate mdogo ukaniletee; kisha ujifanyie nafsi yako na mwanao.

 

MJANE:

Ø  Konzi ya unga katika pipa

Ø  Mafuta kidogo katika chupa

Mjane “ tuule tukafe”

Katika hali hiyo yote mjane aliweza kujitoa mwanga maisha, kwakutoa nafasi ya kwanza kwa mtumishi wa Mungu baadae ajiweke yeye!

Ukimweka Mungu mbele naye anakuweka mbele.

b)      Kutokuwa kipenzi cha watu

Unaweza kuwa kwa ajili ya kusaidia jamii husika lakini hao hao wasikupokee au kukubali.

Yohana 1:11

Alikuja kwake, wala walio wake hawakumpokea.

“ alikuja kwake, walio wake hawakumpokea”

Ni muhimu kujua kuwa uwa kusudi ni lazima litimie haijalishi wamekupokea au hawajakupokea.

Kusudi linajitosheleza lenyewe alihitaji msaada mwingine wowote.

Yohana 11:8

Wale wanafunzi wakamwambia, Rabi, juzijuzi tu Wayahudi walikuwa wakitafuta kukupiga kwa mawe, nawe unakwenda huko tena?

“ wale wanafunzi wakamwambia, Rabi, juzijuzi tu wayahudi walikuwa wanakutafuta……………”

Unaweza kuhatarisha maisha yako ili wengine wawe salama.

iii.                Epuka mazoea

Kila mtu ana ramani yake katika kuishi katika maongozi ya Mungu akiwepo hapa duniani.

Mungu uwa hana nafasi ya mbadala vile alivyo ndivyo anakuwa wala sio mjomba au bibi yake ili amtanie.

Ni muhimu ujue pindi utakapoanza kuishi kwa mazoea hapo ndipo utakapo punguza penzi lako kwake. ( ushirika )!

NDOA: Moja ya sababu inayopelekea ndoa kuvunjika kumzoea mwenzi hivyo kufanya jambo pasipo kujali nini kitatokea au atajisikiaje ( kutojali hisia za mwenzako ).

Mazoea pia ndio mwanzo wa kupoteza njia unayotakiwa kuendea.

KIBURI NA UJUAJI ni pacha wa mazoea, mathalani nishachoka na mahubiri ngoja mwezi huu ni pumzike nyumbani kidogo nione nitapungukiwa na nini.

INAITWA SIKU! BARIKIWA SANA

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson…………………………………………….. 0764 018535