Ijumaa, 23 Septemba 2022

MWISHO WA MCHEZO;

 



Ni mwisho wa mchezo tu ndio unaamua shangwe iendelee au ikatike!

Mwisho wa mchezo ndio unaobeba kicheko au kilio cha kudumu na wala sio mwanzo au katikati ya mchezo!

Naam mwanzo wa jambo ni vigumu kutambua/kugundua mwisho wa jambo utakuaje? Japo unaweza kukisia kutokana uwezo/uzoefu ulionao.

Laiti tungepata neema ya kujua mwisho wa jambo na amini tungekuwa makini katika mwanzo wake hama kuacha kabisa kama utaona mwisho si mzuri.

Wakati mwingine namna ulivyoanza inaweza isiwe na nguvu sana lakini mwisho ukawa ni mwisho wa kishindo kama sio wa neema/ustawi, kuna wakati unaweza kuanza kwa kusuasua/pasipo uhakika wa kufika lakini mwisho ukafika ushuhuda unakuwa na nguvu hata kusahau magumu uliyoanza nayo.

Wakati mwingine watu wengi wanaishi kana kwamba maisha yao yako mikononi mwao, wenyewe tahadhari na umakini katika maisha yao unakuwa haupo.

Kuna maisha ya mtu anaishi kwa uhuru zaidi pasipo kujali hiki wala kile kwasababu ya fedha anazozipata ili kuishi anavyoona yeye pasipo kujua kuna giza au mtelelemko mkali kule anako kwenda au anako endea.

Ni kweli kuna wakati, mathalani mechi zinapocheza uchezaji au timu moja inaweza onekana kuwa inazidiwa na hata ufanisi wake unaweza usionekane lakini mwisho wa mchezo endapo ikaibuka mshindi hivyo hapo watu wanaweza kusahau makosa waliyo yaona uwanjani na kujiunga katika kusherekea ushindi uliopatikana.

Pia kuna uwezekano mkubwa kwa watu wanaokuangalia wanaweza wasikuelewe na wakati mwingine wanaweza kukuona unapoteza muda lakini mwisho kitu chako kinapoanza kuonekana na hata kushika mizizi basi hapo wataanza kukuelewa mathalani mwimbaji wakati mwingine anapoanza kuimba wakati huo uweza kuonekana kama kero na wakati mwingine anaweza kuonekana kuwa anapoteza muda ni bora ungesoma na baadae hata ukawa mtaalamu wa jambo Fulani kuliko kupoteza muda kufanya jambo lisilo na tija lakini mwishoni utapoendesha maisha yako katika uchumi mzuri basi hapo wataanza kuona maana ya wewe kuimba.

Na neema inapoanza kushuka kwako usipende kuishi kana kwamba ni kipofu kana kwamba baada ya leo hakuna kesho ni muhimu utambue hipo kesho na anayeijua Mungu tu, usifanye/usiishi katika dunia kana kwamba ulishirikishwa katika uumbaji wake na unahati miliki ya maisha yako.

Unapaswa kujua watu watakuona wa maana endapo tu kuwa mwisho wako utabaki kuwa kileleni katika maisha yenye ushindi mzuri.

Usiishi maisha ambayo hauta tamani kuishukuru jana yako ukajutia na hata ukatamani hata isingekuwepo maana mwisho umekuacha pasipo mwelekeo wa maana wa kutoa mwanga wa kesho yako au jamii inayokuzunguka kufaidika na uwepo wako.

Ni kweli maadamu unaishi utakiwi kukata tamaa lakini ukumbuke kwa kila fursa unayoipata ujue una sababu ya kuitendea haki, hivyo usipoitumia vizuri ujue kuna gharama utaingia inaweza kuwa ya muda tu au muda mrefu pasipo kikomo.

Mwisho wa mchezo unaweza kukupa maana ya wewe kuwepo duniani au ukakosa maana ya w ewe kuwepo hapa duniani, chochote Mungu anapofanya kwako ni kwa ajili yake na wala sio kwa ajili yako tu binafsi.

INAITWA SIKU! BARIKIWA SANA

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson………………………………………………………………….0764 018535

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni