Alhamisi, 6 Oktoba 2022

KUJUA KUNA GHARAMA

 



 Akiona hazina kwenye shamba………..akaenda kuuza alivyonavyo ili anunue shamba!

Mathayo 13:44 Tena ufalme wa mbinguni umefanana na hazina iliyositirika katika shamba; ambayo mtu alipoiona, aliificha; na kwa furaha yake akaenda akauza alivyo navyo vyote, akalinunua shamba lile.

Pindi unapofanya kitu ambacho  kinajulikana kwa watu wengi watu hawawezi kukushangaa sana mathalani unapopeba gunia la mahindi kwa ajili ya kwenda kupanda shambani watu awatashangaa bali watakuona mtu mwenye akili lakini pindi ikatokea unaenda supermarket na jembe lililoshikama na udongo bila shaka ukinusulika kusimamishwa na askari basi unaweza kusababisha mtafaruku kwa wateja waliopo hapo.

Naam shida ni pale wewe utaona lulu iliyojificha na watu hawaoni kile unachokiona pindi utakapo jibidisha kufanya kitu au kuingia gharama ili uweze kupata kitu ambacho wengine awakioni tegemea kutopewa ushirikiano pia ni wewe ulio na jukumu hilo hivyo likamilishe kwa gharama yoyote maana ni wewe umeona hiyo lulu.

Maana kile unachokiona wewe ambacho wengine awakioni au kuona kuwa ni kitu cha maana sahau kutiwa moyo ( maana hawaoni thamani ambayo wewe unaiona )

Unahitaji kujua zaidi kuhusu hiyo lulu/hazina unayoitafuta ili uweze kuimili kishindo cha kupingwa sio na watu tu bali hata historia inaweza kukuhukumu.

Nuhu alijenga safina huku yeye akiamini sauti ya Mungu kuwa kutakuwa na gharika hivyo ili aweze kuwa salama ni kutengeneza safina , ila pindi alipoanza kujenga na hata kumaliza lakini watu awakumuelewa ila walimwelewa pale gharika ilipotokea.

Kujua kuna raha pia kuna mateso, raha ni pale utakapofanya utajisikia vizuri haijalishi kinalipa au akilipi kwa wakati huo na mateso ni pale utakapo pata upinzani kwa watu unaowaamini na kuwa tegemea kuwa upande wako wakawa kinyume nawe kwa vile unapofanya na kukosa mwitikio mfano.mwimbaji unapoimba imba hovyo hovyo kila mahala wataona ni kero.

Kutokujua kuna ondoa gharama hama kujigharimu kwani unaweza kushika dhahabu na ukaiona jiwe unaweza kulitupa na ukawa na amani tu pasipo kujua kile ulichokitupa kina thamani gani?

Pindi inapotokea kuwa wewe tu ndio unajua kwanini unafanya hivi na kitakuweka wapi kesho! Usipo kaza katika kufanya unaweza kujikuta unajitenga na baraka zako, ukaenda katika mwelekeo tofauti na uliokusudiwa pindi utakaposhtuka unaweza kuona umechelewa/unamwendo mrefu hadi kurudi kule katika njia yako.

Unapojua kitu cha kufanya ambacho wengine awakioni usitake kutumia nguvu sana ili waelewe kama wewe unavyoelewa, ukifanya hivyo utapoteza muda na nguvu zako, kwani mchungwa unapoanza kuota unaweza usielewe au ukaufananisha na miti mingine lakini utauelewa au utaanza kupata uhakika pale utakapoona machungwa yakianza kuchomoza hapo maswali yote yatakuwa yanajijibu yenyewe tena kwa ufasaha zaidi.

Unahitaji kutia bidii katika kile unachokijua NO MATTER WHAT! Kama mkulima anapolima kwa bidii uku ukijua mara baada ya kulima kuna mavuno atakayoyapata ambayo yata mnufaisha yeye na jamii yake uona hivyo tu na hali hiyo umfanya awe na bidii na hata akichoka anajitia nguvu kwakuwa anajua kuna jamii inamtegemea na ndo mana maneno yoyote yakumvunja moyo hayatapata nafasi ndani yake bali yeye uishi kwa kile anachokiamini kwani anajua kama akiishi katika maneno hayo ya watu anaweza akajikuta ana kufa njaa.

Uzuri na umaana wa wewe kujua unakuja pale utapojua hiyo gharama  na kuipenda kuibeba au kuikubali na kuikabili maana hapo ndipo itakapotimia dhana ya kuwa huyu anajua anachokifanya , ni kama mwanafunzi mwenye ndoto kubwa mbele yake ni lazima atajibadisha kusoma sana pasipo kuchoka huku akijua bidii yake sio bure.

Ni kawaida tu mjenzi anapotaka kujenga lazima aka echini na kujua kwanza gharama yake kasha ndipo hapo atatoa maamuzi ya kujenga au kusubiri.

Luka 14:28 Maana ni nani katika ninyi, kama akitaka kujenga mnara, asiyeketi kwanza na kuhesabu gharama, kwamba anavyo vya kuumalizia?

              29 Asije akashindwa kuumaliza baada ya kuupiga msingi, watu wote waonao wakaanza kumdhihaki,

              30 wakisema, Mtu huyu alianza kujenga, akawa hana nguvu za kumaliza.

Unapojua usiogope gharama maana gharama zipo ili kuthibitisha kujua kwako.

INAITWA SIKU! BARIKIWA SANA

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson……………………………………………………………….0764 018535

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni