Haya maisha ya kumtegemea Mungu na yafananisha na maisha ya mtu aliye kipofu anayetembea usiku pasipo usaidizi wa mtu ila anakuwa ana matumaini kuwa safari yake anayoiendea atafika hata ikitokea amejikwaa mara zote lakini ana amini kufika kupo tu!
Ni rahisi kusema au kujishuhudia kuwa unamtegemea Mungu lakini ni kitu kingine Mungu mwenyewe kukushuhudia kuwa unamtegemea.
Naam ni fahari ya mzazi kuona watoto waliochini ya uangalizi wake wanamtegemea yeye! Na sio jirani zake.
Hivyo linakuwa ni jukumu lake kuhakikisha hao watoto wako salama na wanafurahia maisha yao hasa katika uwepo wake.
Katika kumtegemea Mungu uwa hatusemi kuwa sisi tunamtegemea Mungu! basi inatosha, bali zaidi sana maisha yenyewe yanajieleza kuwa yanamtegemea Mungu au la!
Kumtegemea Mungu ni siri iliyojificha ndani ya mtu binafsi na sio kitendo cha kujivika majukumu ili uonekani kwamba uko kanisani na unamtegemea Mungu.
Kumtegemea Mungu ni kuishi au kutembea na moyo wa Mungu, unatembea uku ukisababisha shangwe katika moyo wa Mungu.
Mtu anapoishi maisha ya kumtegemea Mungu hayo ndio maisha yanaitwa maisha ya uchaji/ moyo wa ibada.
Hakuna jambo utakalo lifanya mbele za Mungu naye Mungu akakufurahia nje ya maisha ya kumtegemea yeye pasipo kujali watu wanasisimka kwa kiasi gani hama changamko lao.
Kabla ujazama katika kutumika zaidi ni vizuri ujikite sana kumtegemea Mungu maana swala hili limekuwa ni mtihani mkubwa, mtu anakuwa bora zaidi kutumika katika vipawa kuliko kukua na kuzidi katika kumtegemea Mungu pasipo kujua kutumika pasipo kudumu katika kumtegemea Mungu inakuwa sawa na nahodha wa meli anayeendesha kwa bidii uku akikosa dira sahihi ya kule anakoelekea.
Kama ikatokea fursa ya kusoma na ukawa na masomo mengi mathalani kujifunza kuimba , kuponya wagonjwa, kuubiri hata kutoa unabii na likawepo pia somo la kumtegemea Mungu basi mimi ningekushauri acha kwanza masomo yote na ujikite katika kujifunza kwanza kumtegemea Mungu na ndivyo masomo yote yatakuwa mepesi na hata kuwezekana.
Unapotaka kumuona mtu mwenye nguvu za rohoni na mwenye akili kubwa ni mtu anayemtegemea Mungu wakatiwengine watu wanataka upite huku ili wakupate lakini watashangaa umepita njiia wasioijua na kufika mahali ambapo awakutegemea utafika na kuketi pale wasipo penda.
Mtu anayemtegemea Mungu uwa anaona mahali ambapo wengine hawaoni na anatembea mahali ambapo watu kwa kawaida wa akili za kinadamu awezi kutembea hapo naam anakaa mahali kwa akili timamu hauwezi kukaa hapo.
Ø Danielkatika tundu la samba
Daniel 6:23 Basi mfalme akafurahi sana, akaamuru wamtoe Danieli katika lile tundu. Ndipo Danieli akatolewa katika lile tundu, wala dhara lo lote halikuonekana mwilini mwake, kwa sababu alikuwa anamtumaini Mungu wake.
Daniel 6:24 Mfalme akaamuru, nao wakawaleta wale watu waliomshitaki Danieli, wakawatupa katika tundu la simba, wao, na watoto wao, na wake zao; na wale simba wakawashinda wakaivunja mifupa yao vipande vipande, kabla hawajafika chini ya tundu.
Ø Shedrack, Meshack na Abenego katika tanuru la moto
Daniel 3:19 Ndipo Nebukadreza akajaa ghadhabu, na sura ya uso wake ikabadilika juu ya Shadraka, na Meshaki, na Abednego, basi akatoa amri watie moto ile tanuru mara saba kuliko desturi yake ya kutiwa moto..
Daniel 3:26 Kisha Nebukadreza akaukaribia mdomo wa ile tanuru iliyokuwa inawaka moto. Akanena, akasema, Enyi Shadraka, na Meshaki, na Abednego, watumishi wa Mungu Aliye juu, tokeni, mje huku. Ndipo Shadraka, na Meshaki, na Abednego, wakatoka katika ule moto
Ukifanikiwa kujua namna ya kumtegemea Mungu kuna maisha hauwezi kupitia mathalani maisha ya kukata tama, kuwa na chuki, kisirani na hata magomvi kwakuwa uyaweka maisha yake ndani yako.
Kwakuwa mtu anayemtegemea Mungu uwa kila jambo linalotokea katika maisha yake yeye anamuona Mungu tu haoni kingine kwa kuwa anajua jambo ambalo lililoanzishwa na Mungu yeye atalikamilisha kwa wakati wake hivyo furaha kwake ni kama pumzi katika maisha yake siku zote.
INAITWA SIKU! BARIKIWA SANA
Imeandaliwa na:
Cothey Nelson……………………………………………………………..0764 018535