Ijumaa, 4 Novemba 2022

ONGEZA THAMANI YAKO;

 



Thamani inaongezewa au inajiongeza?

Au ongezeko la thamani ni matokeo ya jambo ulilolifanya na likafanikiwa?

Yote yanaweza kuwa ni majibu au maswli tena yanaweza kuwa sahihi kwa mtu huyu na kwa mwingine yanaweza  yasiwe sahihi inategemea sana tafsiri mtu,

Na kwa upande mmoja unaweza kujitahidi kujiongeza thamani yako na pindi watu wasipoona hilo/hiyo ongezeko watakuona vilevile wala hakuna kitakachobadilisha chochote akili zao.

Ni wazi tu, uwa thamani ya kitu inaongezeka pale uhitaji wa hicho kitu unapoongezeka lakini kikiwepo tu  na kwa kila mtu anayekitaka anakipata tu kwa urahisi tu, bila shaka thamani inapungua au inakuwa ya kawaida.

Wakati mwingine thamani uweza kuonekana pale mtu/kitu kinapokosekana mwenye uwezo wakufanya hilo jambo kwa ufanisi zaidi kuliko wengine ingawa inaweza kutokea wengine wakawepo wenye kufanya sawa na yeye lakini sio kwa ufanisi na moyo wote.

Naam bila shaka maisha yanakuwa na furaha pindi utakaposikia/kujua thamani yako imeongezeka/imepanda mahali popote ulipo: kazini,shuleni hama kanisani n.k

Baadhi ya watu wanaenda kusoma ilikupa shahada ya kwanza au ya pili na hata udhamivu ili kuongeza thamani katika mahali anapofanyia kazi na hatimaye mshahara kuongezeka kwa sababu ana amini akiongezeka katika elimu atapata nafasi ya juu ( madaraka ya juu ) lakini pindi anapoona miaka inaenda na ameshawasilisha vyeti vyake ofisini na mshahara haupandi anakuwa hanafuraha kamilifu.

Thamani inaongezeka: ufahamu + majira

Majira yanapofika yanapofika yanasubiri ufahamu ukubali ili iweze kuchukua nafasi kamili na mwili uhitikie.

Thamani inapotaka kuongezeka katika majira yake kuna mapinduzi makubwa yanabidi yafanyike katika ufahamu wako.

Wakati mwingine utaona unayaingiza maisha yako katika matatizo makubwa, baadhi ya watu watashindwa kukuelewa na wakati mwingine utaona muda hautoshi.

Ni sawa na mtu anayetaka kuwa na kiwango fulani cha elimu mathalani profesa, ili afike hapo ni lazima atumie muda mwingi katika kusoma vitabu hivyo atatumia muda mwingi katika maisha yake katika kuelekezea kule anakotaka kwenda.

Majira ya kuongeza thamani yako yanapofika ufahamu wako usipokubali mageuzi utaka hapo hapo na pengine hata kufanyika mazomeo.

Aliyekaa birikani, ufahamu ulijua ni lazima atumbukie katika birikani ili apone bila kujua kuwa majira yanaweza kubadilika kuwa unaweza kufunguliwa hama kuponywa hata bila kuingizwa birikani.

Yohana 5:7 Yule mgonjwa akamjibu, Bwana, mimi sina mtu wa kunitia birikani, maji yanapotibuliwa; ila wakati ninapokuja mimi, mtu mwingine hushuka mbele yangu.

Mageuzi ya ufahamu ni muhimu ili uweze kutembea katika thamani nyingine, na ufahamu unapobadilika na mtindo wa maisha yako unabadilika kuelekea katika ongezeko la thamani unaloliona.

Ufahamu kukubali mabadiliko yanahitaji moyo uliojaa ujasiri na ulioimara katika kukabiliana mabadiliko yajayo.

“ uwe hodari na moyo ushujaa”

Yoshua 1:7 Uwe hodari tu na ushujaa mwingi, uangalie kutenda sawasawa na sheria yote aliyokuamuru Musa mtumishi wangu; usiiache, kwenda mkono wa kuume, au wa kushoto, upate kufanikiwa sana kila uendako.

Mabadiliko mengine yatabadilisha maisha yako kabisa katika hayo mabadiliko kuna maumivu makali utayoyapitia.

“ No Pain No Gain”

Mathalani majira yanapofika kwa mama mjamzito anapotakiwa kubadilisha hadhi yake na kupakata, maumivu na uchungu ( mateso ) yanakuwa ni furaha baada ya kupakata.

INAITWA SIKU! BARIKIWA SANA.

Imeandaliwa na:

Cothey Nelson……………………………………………………….…..0764 018535

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni