Moja ya neno zuri ambalo watu wengi upenda kusikia na uwa mioyo ya watu uwa na bashasha na hata kupelekea hamasa ya kufanya zaidi ni hili neno ASANTE! ( lililo na tafsiri ya maana ya shukrani ).
Ni wazi hili neno linahitajika litumike katika hali ya jambo husika pasipo kujali kuwa ni kubwa au dogo, kwa maana ule moyo utakao kuwa nao kushukuru katika jambo ambalo wewe binafsi unaliona dogo basi hiyo ndiyo ishara kuwa utamshukuru Mungu hata lile linaloonekana kubwa.
Mungu anapofanya jambo kwako uwa haoni kuwa ni kubwa au dogo bali yeye uona ni jambo jema akutendealo hivyo unapaswa kumshukuru kwa moyo wote ili liweke msingi mzuri kwa Mungu kufanya zaidi.
Katika jamii tuliyonayo tumejengewa kumshukuru Mungu au kusema ASANTE kwa Mungu hasa mwisho wa mwaka ( ukiamini amekulinda toka mwezi wa kwanza hadi mwezi wa kumi na mbili na kwa kutambua kuwa wewe hauna upekee sana kuliko watu waliotangulia ( kufariki )
Uwa kila kitu kinakuwa na maana pindi utakapo tambua maana! Usipotambua maana akitakuwa na maana, haijalishi kina thamani kubwa kiasi gani?
Siku uwa ni matokeo ya mambo yaliyofanyika na ndio kiashirio kikubwa cha wakati ujao hivyo ni kiini kikubwa katika maisha yako, hauhitaji uipuuzie kwa namna yoyote.
Ni muhimu kutambua kuwa siku ni fumbo maana kila saa linapopita uwa kuna mambo yanafanyika yanaweza kuathiri maisha yako kwa namna moja au nyingine.
Siku ni jiko inapika cha jana ( kukitengeneza cha jana ) na kukiona kama kitafaa kuliwa ili kikufae kesho hama kuandaliwa kingine kama hicho akifai.
Ukweli siku moja imebeba maajabu makubwa wako watu wanaanza siku yao kwa furaha lakini baadae wanahitimisha kwa kilio, pia wako watu wanaanza siku yao kwa kilio lakini baadae wanahitimisha kwa tabasamu.
Siku inaweza kukatisha ndoto zako au kuendeleza!
Siku moja ni muhimu sana kwani wako watu wanafanya/wanafanyiwa jambo ambalo awakuwai kuliwaza au kutegemea kufanya mathalani wako watu wanabakwa na kuteswa katika siku na kubadilisha rangi ya siku yake pia wako watu wanachukua jukumu la kutoa uhai wa mtu japo hapo awali akuwai kuwaza wala kufikiria kufanya jambo kama hilo.
Ndomana ni muhimu sana kumshukuru Mungu kwa moyo wako wote haijalishi wengine wanaionaje hiyo siku lakini wewe uonyeshe thamani kwa Mungu kwa kukupa siku hiyo pasipo kujali kama ina utulivu au ina machafuko.
Usiwe na shukrani ya kina pindi utakapo nusulika na majanga makubwa yaliyoshtua moyo wako na kukupa tashwishwi mathalani mtoto wako kaponea chupuchupu kudumbukia katika shimo la maji taka sasa hapo uishii tu kushukuru hadi sadaka ya shukrani itatolewa kwa kuwa hilo umeliona, pasipo kujua yapo mengi usiyoyaona na pengine yalikuwa na hatari kubwa kuliko hilo uliliona au yale unayaona.
Kumbuka siku ndio msingi wa wiki hatimaye mwezi na mwishoe ukamilisha mwaka, hivyo ukiweza kuitengeneza leo yako vizuri basi umeitengeneza mwaka wako vizuri.
Hivyo usidharau leo kwa sababu ni masaa machache tu na ukaipa thamani kubwa mwaka ( kana kwamba umejitengeneza wenyewe kumbe huo mwaka ni zao la siku ) maana una siku nyingi, ni muhimu kutambua sio kila mtu anapata neema ya kufunga mwaka japo inawezekana walikuwa na malengo yao ya kufika hapo na malengo kama sio mikakati kuweka kwa ajili ya kufunga mwaka, hivyo kila siku utakayoipata ni muhimu umshukuru Mungu maana ujui kesho inaweza kuwa sio siku yako.
Unahitaji kuiona siku kama lulu ambayo thamani imezidi chochote,shukrani ya dhati lazima ionekane kwa Mungu na kuitambua siku Mungu amekupa kwa ajili ya faida yake,
INAITWA SIKU! BARIKIWA SANA
Imeandaliwa na:
Cothey Nelson……………………………………………..…………0764 018535