Majira kama vipindi mbalimbali vinavyotokea katika dunia na kukamilisha asili yake, na kwa kiasi kikubwa uchangia maisha ya binadamu kuendelea,
Naam katika dunia tunayoishi kuna majira mbalimbali mathalani majira ya joto,baridi na upepo mkali haya yote uonyesha fahari ya dunia katika asili yake.
Hakika kuna tofauti kubwa kati ya mtu anayeishi anayeelewa majira yake na yule asiyeelewa majira yake, kwa mtu anayeelewa majira uwa anajiandaa na hali ijayo anapojua majira ya baridi yanakaribia basi hapo uweza kuandaa mavazi ya aina fulani katika kukabili na hali hiyo mfano.nguo nzito….. ila kwa mtu asiyejua hali ya hewa ijayo anaweza akaandaa nguo nzito wakati hali ya hewa ijayo ni ya joto.
Ni wazi unapoishi bila kujua majira yako basi hapo……………..!
“ wakati wa kucheka wewe utakuwa unalia na wakati wa kulia wewe utataka ucheke”
Kwa asilimia kubwa uwezi kuwa mtu mwenye ubora endapo tu ukiishi nje ya majira,
“ muda wa kufanya kazi utataka kulala na muda wa kulala utataka kufanya kazi”
Unapoishi nje ya majira mateso ( mwili na akili ) yana kuwa ni fungo lako.
Majira kwa asilimia kubwa uwa hayafanani inawezekana ni majira ya mwenzako kuvuna lakini ni majira yako kupanda tofauti na mwenzako hivyo usiwe na haraka.
Mhubiri 3:1-8
1 Kwa kila jambo kuna majira yake, Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu.
2 Wakati wa kuzaliwa, na wakati wa kufa; Wakati wa kupanda, na wakati wa kung'oa yaliyopandwa;
3 Wakati wa kuua, na wakati wa kupoza; Wakati wa kubomoa, na wakati wa kujenga;
4 Wakati wa kulia, na wakati wa kucheka; Wakati wa kuomboleza, na wakati wa kucheza;
5 Wakati wa kutupa mawe, na wakati wa kukusanya mawe; Wakati wa kukumbatia, na wakati wa kutokumbatia;
6 Wakati wa kutafuta, na wakati wa kupoteza; Wakati wa kuweka, na wakati wa kutupa;
7 Wakati wa kurarua, na wakati wa kushona; Wakati wa kunyamaza, na wakati wa kunena;
8 Wakati wa kupenda, na wakati wa kuchukia; Wakati wa vita, na wakati wa amani.
Maisha ili yaende yanahitaji kufuata majira!
Dunia ili iende inahitaji kufuata majira yake! Kujizungusha kwenye muhimiri wake.
Mkulima ili aweze kulima na kuvuna mavuno yake kwa ajili ya kujikidhi yeye na familia pamoja na jamii yake basi hapo ni muhimu azingatie majira ya kupanda ili aweze kuvuna.
Ni muhimu kuyaelewa vizuri majira yako maana ni kwa faida yako na usipoyaelewa majira basi hapo ni kwa hasara yako, maana hata mkulima akilima nje ya msimu anaweza kupata kidogo mavuno yake au asipate kabisa.
DUNIA INATEMBEA KATIKA MAJIRA YAKE!
a) Kilimo
Kilimo kinapande mbili kuu: kupanda na kuvuna!, ili uweze kuwa mkulima mwenye tija ni lazima ujue ni majira gani unapaswa kulima hama kupanda ili yakija majira ya kuvuna uweze kuvuna,
Naam kila mazao yana msimu wake ( maembe, machungwa, mananasi n.k ) hivyo ukitaka kufaidi vizuri basi hapo ni muhimu utembee katika msimu wake ili usichangaye mambo.
Wingi na ubora wa mazao yako unategemea vitu vingi mathalani unalima kwa kutumia teknolojia ipi ( kisasa au zamani ), ubora wa mbegu,unalitunzaje hilo shamba ( umwagiliaji,kuweka dawa na mbolea) kila kitu inabidi ifanyike kwa wakati wake pamoja na usimamizi ulioutumia kutoka hatua awali, kuvuna na hata ya mauzo ( faida/hasara ).
b) Uchumi
Matukio yoyote yanatokea duniani yana mchango mkubwa katika kukuza uchumi au kuharibu uchumi mathalani magonjwa ( CORONA-COVID 19 ), Vita ( urusi dhidi ya ukrain ) na vitu vingine vingi vimechangia uchumi kudorora japo na siasa imejificha ndani yake.
Uchumi unasema bidhaa inapoadimika sokoni basi gharama yake inapanda! ( moja ya kanuni )
Ni muhimu kuelewa mambo ya dunia yanavyoendelea kwa maana baadhi ya matendo yanahusiana na biblia inavyosema.
MBINGU INATEMBEA KATIKA MAJIRA YAKE!
Ili kuyaelewa haya majira kuna vitu viwili vya msingi:
Ø NENO LA MUNGU ( MSINGI )
Ø ROHO MTAKATIFU ( MTEMBEO )
Ukiweza kuvielewa vizuri hivi vitu basi hapo utakuwa umeinasa network vizuri kama bar basi zote hapo zimesimama vizuri tayari kwa kupokea mawimbi kwa ukamilifu.
Ni kweli usiopingika wakati mwingine majira ya dunia yanakidhana na majira ya mbingu japo sio mara zote ni kwa kusudi maalum.
Mfano; unapokuwa mwanafunzi alafu usitie jitihada katika masomo yako hivyo ukafanya mitihani na matokeo yakatokea mabaya, usianze kumlaumu shetani na kusema shetani amejiinua dhidi ya elimu yako.
Nilipata nafasi ya kusoma na kiongozi wangu wa fellowship nilipokuwa kidato cha sita alikuwa na jitihada sana katika kazi ya Mungu lakini matokeo ya mwisho yakatoka na kupata division 0,
Hivyo niseme kuwa sio kila kufail ni mapito , mengine ni kutotumia nafasi nzuri uliyopata kwa kuwa kila jambo lina wakati wake japo katika mazingira yoyote neema bado ipo.
NAJUAJE KAMA NATEMBEA KATIKA MAJIRA YA MBINGU:
I. AMANI YA KUDUMU
Hata mambo yakikusumbua au kukutingisha ile amani ipitayo ufahamu inakuja kukufunika na kukupa kuendelea mbele.
Wafilipi 4:7 Na amani ya Mungu, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu.
Waamuzi 6:23 Bwana akamwambia Amani iwe pamoja nawe; usiogope; hutakufa.
Ayubu 22:21 Mjue sana Mungu, ili uwe na amani; Ndivyo mema yatakavyokujia.
Yohana 14:27 Amani nawaachieni; amani yangu nawapa; niwapavyo mimi sivyo kama ulimwengu utoavyo. Msifadhaike mioyoni mwenu, wala msiwe na woga.
II. MNG’AO WA KIMUNGU
Ni kweli mnapitia katika majira ambayo sio sahihi/mazuri inawezekana kuna ukata wewe hivyo mng’ao wa dunia unapoishia basi hapo mng’ao wa kimbingu unachipua.
Ukitegemea pekee yake dunia icheke ili nawe ucheke basi dunia inapoishia hapo nawe utakuwa umeishia.
INAITWA SIKU! BARIKIWA
Imeandaliwa na:
Cothey Nelson…………………………………………………………………..0764 018535
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni