Jumamosi, 25 Machi 2023

KUMTEGEMEA MUNGU

 



Kumtegemea Mungu imekuwa fumbo la maisha ya watu wengi: imekuwa kila mtu upenda kusema anamtegemea Mungu pasipo kujua nini hasa ana maanisha!

Waendao katika nyumba za ibada na wasioenda wote wanasema wanamtegemea Mungu kwa maana Mungu ni mmoja, pia waliookoka na wasio okoka wote wanasema wana mtegemea Mungu.

Hivyo neno hili limekuwa ni la kawaida sana kulisikia kwa mtu, japo wakati mwingine unapolitamka katika mazingira yanayotegemewa kusikiwa hili neno uweza kuonekana kuwa ni mtu mwenye busara.

Hivyo neno hili kumtegemea Mungu limekuwa  likitumika kwa watu wote na asilimia kubwa hata awe ameokoka au mwislam wote wanasema neno hili.

Kumtegemea Mungu ni zaidi ya mtoto mdogo kuwa tegemea kwa wazazi wake au mfanyakazi kutegemea mshahara hama mkulima kutegemea mavuno yake ili aishi.

Wengi wao wanasema pasipo kujua hasa maana ya kumtegemea Mungu kwa uhakika, wengine wanasema kwa sababu awamuoni na wanamuogopa, pia kuna jehanam na yeye ndiye muamuzi wa mwisho, hivyo wanadhani kwa kusema hivyo wanaweza kumshawishi Mungu kuiona pepo/kuikwepa jehanamu.

Mathalani unaweza kukuta watu wamekaa wanajadili mambo mbalimbali yawe magumu au mepesi, pale wanapofikia akili zao kutokuwa na majibu ya uhakika basi hapo neno kumtegemea Mungu lina kuwa na maana sana, kwahiyo kumtegemea Mungu inakuja pale akili zao zimefika mwisho kwa maana hiyo kama akili zao zisingefika mwisho wasingeona umuhimu wa kumtegemea Mungu.

Ukweli katika hali ya kumtegemea Mungu kuna mawanda mapana sana, wako wengi hawana uhakika kwamba wanamtumaini/kumtegemea Mungu na wengine wanahisi kuwa wana mtegemea Mungu na wengine uwa wanaambiwa tu ila wenyewe hawajui “ kweli wewe unamtegemea Mungu maana alipokuwepusha pale”

Warumi 8:16…. Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu;

Japo Mungu ndio pekee hajuaye nani amtegemeaye yeye lakini kwa mtu anayemtegemea Mungu  Roho mtakatifu umshuhudia toka ndani yake,

Moja ya faida ya kumtegemea Mungu ni hali ya Mungu kukupa uwezesho/kukutegemeza zaidi juu ya dunia tuliyonayo ili tuweze kuyashinda yote kwa njia zake.

Kumtegemea sio swala la tukio gani lililo kukuta bali ni hali ya kukua katika ushirika na Mungu na huku ukitambua pasipo yeye wewe hauna maisha.

Kumtegemea Mungu lazima ukue katika ufahamu wake ongezeko la nguvu ya ndani yako ikupayo kushinda katika yote yanayokuzunguka.

Kumtegemea Mungu haya maisha yaliyo ambatana na furaha, amani, na utulivu ulio katika ukamilifu.

Ni mumhimu kutambua kuwa hauwezi kumtegemea Mungu katika misimu fulani tu baada ya msimu huo hakuna kinachoendelea tena, usimtegemee Mungu katika majira/msimu ambao unaona wewe, Mungu haitaji kuwa mtatuzi wa shida zako tu bali anataka usalama wote wa maisha yako uwe mikononi mwake, uwe chini ya maongozi yake.

Kuna faida kubwa hapa duniani ukitambua siri iliyopo katika maisha ya kumtegemea Mungu, ujasiri juu ya Mungu unakuwa mkubwa sana na unakuwa unajua kile unachokiamini hivyo kufanya wepesi katika kumdhihirisha katika mazingira yako.

Mungu uwa anatambua nani anamtegemea yeye na nani ni anaigiza kumtegemea yeye, kwa yule kweli ambaye Mungu anajua anamtegemea uwa hawezi kushindwa kujidhihirisha kwake.

Usibweteke pindi ukawa unahisi tu unamtegemea Mungu na ikatokea bahati mambo yakaenda sawa ukafikiri sasa wewe unamtegemea Mungu, sio kweli kwani wako watu ambao hawana fikra ya kumtegemea Mungu lakini mambo yao kuna wakati yanaenda sawa.

Unahitaji Roho mtakatifu akushuhudie kama unamtegemea Mungu na mtu anayemtegemea Mungu uwa hanamashindano ila uweza kuisimamia haki yake.

INAITWA SIKU! BARIKIWA SANA.

Imeandaliwa na:

Cothey Nelson………………………………………………………..0764 018535

Ijumaa, 10 Machi 2023

ACHA IOZE



Kwa asilimia kubwa katika watu wengi uwa awapendi kusikia hili neno KUOZA maana wanaamini jambo lolote likifika hatua hii uwa hakuna matumaini tena zaidi ya kuwa na kero sehemu husika,

Japo kuna baadhi ya vitu vinapooza ndio mwanzo wake wa kuchipuka tena hapo kuna kuwa na siri kubwa iliyojificha,

Tunajua kuoza ni hatua inayofuata mara baada kitu kufa/kufariki pasipo kujua baadhi ya vitu  vinazaliwa baada ya kitu kimoja kufa na kuoza.

Naam  kuoza ni hatua inayofuata baada ya kiumbe kufa/mbegu kufukiwa ardhini na katika hatua hii ya kuoza kuna siri kubwa inafanyika katika hali hiyo hadi inapelekea mmea kuchipuka katika ardhi,

Kuna maajabu mengi ya uumbaji wa Mungu yanafanyika katika hatua hii na kubeba utukufu wake mkamilifu,

Kwa lugha ngumu kidogo tunaposema kuoza tuna maanisha ni hali ya mwili au nyama kupukutika na kurudi ardhini.

Bila shaka MBEGU inapooza uwa kuna mabadiliko makubwa yanafanyika ili iweze kubeba vazi la kuishi juu ya ardhini hali hii inafanyika toka katika mfumo mmoja kwenda mfumo mwingine na huo mchakato sio mchezo hata ukiushuhudia hautaweza kuamini au kuelewa.

Na kwa kawaida pindi mbegu inapoanza kuoza kinachofuata hapo ni mazidisho makubwa mathalani unapo panda mbegu ya mahindi moja lakini baada ya muda mbegu zitakuwa nyingi.

Kitu ninachokipenda sana katika hatua hii ya kuoza kwa kiasi kikubwa  ardhi uchangia kuhakikisha mbegu inaoza ili ifanane na ardhi hiyo pasipo kujua hiyo mbegu baada ya kuoza itachipuka na kuwa na mawanda katika ardhi.

Pia mbegu inapooza inakuwa na sura ambayo haiwezi kurudi tena, mathalani mbegu ya mbuyu inapooza inapochipuka na kuenea pia uimara wake unakuwa mkubwa sana.

Ndivyo ilivyo/yalivyo maajabu ya mbegu katika kuoza ile siri/mambo yanayofanyika katika kuoza kwake yanamfanya kuwa tishio pindi itakapo chipuka kutoka katika hatua hiyo.

Sawasawa na bondia inawezekana alikuwa wa kawaida sana mathalani katika mapambano kumi, tisa anapigwa na moja anaweza jitihidi kutoa sare (draw) lakini pindi akaamua kwenda kambini kujifua kwa muda wa kutosha, na sasa akiingia ulingoni anakuwa sio yule tena na hapo pindi anapokuta na mpinzani ikatokea huyo mpinzani amefika round ya tatu bila kwenda chini basi alijipanga sana au bahati imemuangukia.

Na yote inawezekana kutokana  na mchakato aliopitia akiwa kambini.

Pamoja tunajua kuoza kama hatua baada ya kufa, pia hatua hii tunaipitia katika maisha ya mwanadamu japo unaweza usijue kuwa hatua uliyonayo ni kuoza.

Na hatua hii ya kuoza au kutengenezwa nje ya utashi wako, unaweza kujikuta katika mazingira usiyoyapenda na wala ukupanga japo inawezekana hayo mazingira ndio uliokusudiwa kuwepo pasipo kuangalia utayari wako au hiari yako.

Japo hatua hii sio pendwa au rafiki kwa wengi lakini ndio hatua pekee inayosababisha mazidisho hata tungepata kujua kusikia jinsi mbegu inavyojisikia pindi inapofukiwa katika ardhi inaweza jiona kama imesahaulika lakini hakuna njia nyingine ya mazidisho zaidi ya njia hiyo, hama umuulize mwanamke katika kipindi anajifungua akili yake inampeleka wapi? Wako wanawake wanaona kama roho yake inaachana na mwili wake, japo kinawezekana kuwa ni kipindi kigumu lakini hakuna njia nyingine ya mazidisho nje ya njia hiyo,

Na ukiwa katika hali hiyo unaweza usijue unatokaje hapo au utakuwa hapo kwa muda gani? Ni kama vile mbegu inavyojikuta imefukiwa chini ya ardhi na mkulima ndivyo hivyo Mungu wakati mwingine anakuingiza katika mazingira usiyoyajua ila yeye anayajua.

Ila ujue baada ya kutoka hapo yale mazingira yaliyo kuwa yanakuonea hayatakuonea tena, maana unakuwa katika matengenezo ili ufae zaidi/ushinde katika mazingira hayo.

Hichi ni kipindi kisichovutia kwa watu wengi hasa jamii ya waliookoka maana wakati huu Mungu anaweza ziba mifereji yote ya kufanya ufurahie maisha yako maana hapo anakuwa na kazi ya kutengeneza akili  yako ili ibebe ubora kwa utukufu mwingine.

Hakuna namna nyingine ya kufanya dhahabu ing’ae zaidi ya kupitishwa kwenye moto hivyo hakuna namna nyingine ya Mungu ya kukufanya kuwa bora bila kukupitisha hatua hiyo.

Mungu haitaji sana uipende hii hatua bali uikubali tu na uingie katika utukufu wake, ni sawa na mgonjwa ni kweli sio mpenzi wa vidonge lakini inabidi atumie tu ili apone kwa njia yoyote lazima vidonge umeze.

INAITWA SIKU! BARIKIWA SANA

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson………………………………..…………………………….0764 018535