Kwa asilimia kubwa katika watu wengi uwa awapendi kusikia hili neno KUOZA maana wanaamini jambo lolote likifika hatua hii uwa hakuna matumaini tena zaidi ya kuwa na kero sehemu husika,
Japo kuna baadhi ya vitu vinapooza ndio mwanzo wake wa kuchipuka tena hapo kuna kuwa na siri kubwa iliyojificha,
Tunajua kuoza ni hatua inayofuata mara baada kitu kufa/kufariki pasipo kujua baadhi ya vitu vinazaliwa baada ya kitu kimoja kufa na kuoza.
Naam kuoza ni hatua inayofuata baada ya kiumbe kufa/mbegu kufukiwa ardhini na katika hatua hii ya kuoza kuna siri kubwa inafanyika katika hali hiyo hadi inapelekea mmea kuchipuka katika ardhi,
Kuna maajabu mengi ya uumbaji wa Mungu yanafanyika katika hatua hii na kubeba utukufu wake mkamilifu,
Kwa lugha ngumu kidogo tunaposema kuoza tuna maanisha ni hali ya mwili au nyama kupukutika na kurudi ardhini.
Bila shaka MBEGU inapooza uwa kuna mabadiliko makubwa yanafanyika ili iweze kubeba vazi la kuishi juu ya ardhini hali hii inafanyika toka katika mfumo mmoja kwenda mfumo mwingine na huo mchakato sio mchezo hata ukiushuhudia hautaweza kuamini au kuelewa.
Na kwa kawaida pindi mbegu inapoanza kuoza kinachofuata hapo ni mazidisho makubwa mathalani unapo panda mbegu ya mahindi moja lakini baada ya muda mbegu zitakuwa nyingi.
Kitu ninachokipenda sana katika hatua hii ya kuoza kwa kiasi kikubwa ardhi uchangia kuhakikisha mbegu inaoza ili ifanane na ardhi hiyo pasipo kujua hiyo mbegu baada ya kuoza itachipuka na kuwa na mawanda katika ardhi.
Pia mbegu inapooza inakuwa na sura ambayo haiwezi kurudi tena, mathalani mbegu ya mbuyu inapooza inapochipuka na kuenea pia uimara wake unakuwa mkubwa sana.
Ndivyo ilivyo/yalivyo maajabu ya mbegu katika kuoza ile siri/mambo yanayofanyika katika kuoza kwake yanamfanya kuwa tishio pindi itakapo chipuka kutoka katika hatua hiyo.
Sawasawa na bondia inawezekana alikuwa wa kawaida sana mathalani katika mapambano kumi, tisa anapigwa na moja anaweza jitihidi kutoa sare (draw) lakini pindi akaamua kwenda kambini kujifua kwa muda wa kutosha, na sasa akiingia ulingoni anakuwa sio yule tena na hapo pindi anapokuta na mpinzani ikatokea huyo mpinzani amefika round ya tatu bila kwenda chini basi alijipanga sana au bahati imemuangukia.
Na yote inawezekana kutokana na mchakato aliopitia akiwa kambini.
Pamoja tunajua kuoza kama hatua baada ya kufa, pia hatua hii tunaipitia katika maisha ya mwanadamu japo unaweza usijue kuwa hatua uliyonayo ni kuoza.
Na hatua hii ya kuoza au kutengenezwa nje ya utashi wako, unaweza kujikuta katika mazingira usiyoyapenda na wala ukupanga japo inawezekana hayo mazingira ndio uliokusudiwa kuwepo pasipo kuangalia utayari wako au hiari yako.
Japo hatua hii sio pendwa au rafiki kwa wengi lakini ndio hatua pekee inayosababisha mazidisho hata tungepata kujua kusikia jinsi mbegu inavyojisikia pindi inapofukiwa katika ardhi inaweza jiona kama imesahaulika lakini hakuna njia nyingine ya mazidisho zaidi ya njia hiyo, hama umuulize mwanamke katika kipindi anajifungua akili yake inampeleka wapi? Wako wanawake wanaona kama roho yake inaachana na mwili wake, japo kinawezekana kuwa ni kipindi kigumu lakini hakuna njia nyingine ya mazidisho nje ya njia hiyo,
Na ukiwa katika hali hiyo unaweza usijue unatokaje hapo au utakuwa hapo kwa muda gani? Ni kama vile mbegu inavyojikuta imefukiwa chini ya ardhi na mkulima ndivyo hivyo Mungu wakati mwingine anakuingiza katika mazingira usiyoyajua ila yeye anayajua.
Ila ujue baada ya kutoka hapo yale mazingira yaliyo kuwa yanakuonea hayatakuonea tena, maana unakuwa katika matengenezo ili ufae zaidi/ushinde katika mazingira hayo.
Hichi ni kipindi kisichovutia kwa watu wengi hasa jamii ya waliookoka maana wakati huu Mungu anaweza ziba mifereji yote ya kufanya ufurahie maisha yako maana hapo anakuwa na kazi ya kutengeneza akili yako ili ibebe ubora kwa utukufu mwingine.
Hakuna namna nyingine ya kufanya dhahabu ing’ae zaidi ya kupitishwa kwenye moto hivyo hakuna namna nyingine ya Mungu ya kukufanya kuwa bora bila kukupitisha hatua hiyo.
Mungu haitaji sana uipende hii hatua bali uikubali tu na uingie katika utukufu wake, ni sawa na mgonjwa ni kweli sio mpenzi wa vidonge lakini inabidi atumie tu ili apone kwa njia yoyote lazima vidonge umeze.
INAITWA SIKU! BARIKIWA SANA
Imeandaliwa na:
Cothey Nelson………………………………..…………………………….0764 018535
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni