Ijumaa, 26 Mei 2023

USIMWEKEE MUNGU MIPAKA

 



Moja swali linaweza kujibika kwa urahisi ni hili;

i)                     ushawai kumwekea Mungu mipaka?

Jibu:

-          Nawezaje mimi kumwekea Mungu mipaka wakati ni yeye aliyeniumba na mimi ni kazi ya mikono yake, kwa maana hiyo Mungu ndio mwenye uwezo wakiniwekea mipaka na wala sio mimi kumwekea Mungu mipaka.

Hili swali ukimuuliza mtu yeyote anayeenda kanisani atakujibu pasipo mashaka yoyote:

i)                    Mungu hana mipaka katika utendaji wake?

-          Bila shaka atajibu huyo ni Mungu hakuna kitu kilicho zaidi yake hivyo yeye ndio mwisho hakuna mwingine wala badala yake hatatokea.

ii)                  Ufahamu wako haujamwekea Mungu mipaka?

-          Naam bila shaka anaweza kujibu Mungu anaweza sana naanzaje kumwekea mipaka katika ufahamu wangu mdogo, Mungu ni mkubwa sana hawezi kutosha katika ufahamu wangu.

NI KWELI HATUMWEKEI MUNGU MIPAKA?

Sasa karibu tuingie katika kiini cha somo:

a)      Mathalani tarehe za kodi zinapokaribia kuisha na uhakika wa kupata kodi haupo hapo ufahamu wako utaweza kumuona Mungu anaweza!…………..kukupa maji jangwani!

b)      Umri unakwenda na uoni mwenzi wa kukuoa au kumuoa bado ufahamu wako utaona Mungu anaweza kukupa mpenzi hata uzeeni!……………………wakati ambao akili yako hawezi kutarajia?

c)      Miaka inazidi katika ndoa bila mtoto na wakwe wameanza kuamia hapo na vikao vimeanza kujadili swala kwanini upati mtoto je! Bado ufahamu unaweza kumuona Mungu ni mkubwa na anaweza kukufuta machozi yako kama sio yenu kwa wakati aliopanga?

d)     Inawezekana unapata ujauzito mara nyingi lakini inaharibika umejaribu kwenda hospitali mbalimbali pamoja na miti shamba ya kutosha hakuna msaada wala tumaini hata hapo bado ufahamu wako utaona uweza wa Mungu na kukutoa pale ulipo?

Ni kweli ukitaka kuona utendaji wa Mungu mkamilifu unahitaji kuishi katika ufahamu wake na sio ufahamu wako.

Unahitaji kujua unapaswa kujua umezaliwa na umekusudiwa katika Mungu na sio mpango wako hivyo unahitaji kuishi katika ufahamu wake ili umwelewe yeye katika akili yake/mawanda yake ili uweze kuishi vile unavyopaswa sawa na utajiri wake.

Moja ya kitu kitachokusaidia kutomwekea Mungu mipaka ni kutoishi katika hisia zako, usiwe kama muota ndoto za uwoga anaogopa kulala japo anataka kulala hivyo anakuwa katikati pasipo kujua nini cha kufanya.

Hama mtu na mpenzi wake pindi inapotokea tofauti kidogo maswali mengi uweza kutokea mathalani kachelewa kurudi au ajapokea simu kwa wakati, unaweza kuhisi mambo mengi labda ameshaanza dharau au kuna mtu mwingine ameanza kumwelewa vizuri kuliko wewe!

Unapoamua kuingia kwa Mungu hakikisha hauishi katika fahamu zako bali ziruhusu akili za Mungu ziishi ndani ya ufahamu zako na endapo kutakuwa na jambo baya linalotaka kukufikia Mungu atalifunua mapema sio kutembea katika kuhisi hisi tu.

Na unapoamua kuingiza ufahamu wa Mungu katika akili zako ni lazima usome neno la Mungu kwa bidii na uruhusu uhai wake na nafasi yake katika ufahamu wako na kudhihirika katika maisha yako.

Mungu anataka aishi yeye kupitia wewe  ili yeye ayaweze mazingira yote yanayo kuzunguka maana yeye anayajua yote na hakuna kitu kigeni kwake ndo maana anatuita sisi kuwa ni mabalozi wake kwa maana inabidi tufanye ya kwake na yeye atafanya ya kwetu kwa kuwa yeye ufanya kupitia sisi.

Watu wanaona ubora wako kupitia utendaji wa ufahamu wako, ufahamu ukiwa bora nawe unakuwa bora kwa kuwa ni yeye anakufanya kuwa bora kupitia ufahamu wake uliondani yako.

INAITWA SIKU! BARIKIWA SANA

Imeandaliwa na:

Cothey Nelson……………………..………………………………………..0764 018535

Ijumaa, 12 Mei 2023

UNAPENDA NINI HASA ZAIDI?

 



Ni kweli unaweza sema unapenda kula, lakini kipo chakula ambacho ukila unasikia burudiko ndani ya moyo wako maana unakipenda zaidi!

Naam, unaweza sema unapenda sana michezo lakini uko mchezo unaopenda sana, na sababu unaweza ukawa unayo moyoni mwako!

Pia unaweza sema natafuta msichana wa kumuoa, bila shaka utakuwa umaanishi ili mradi ni msichana tu bali huyo msichana kuna namna yupo, ambayo ukimuona tu moyo wako unafunguka wenyewe bila kufunguliwa!

Vilevile unaweza sema uwa unasema napenda kijana wa kiume wakunioa na hapo utakuwa umeshamtengeneza handsome wako katika akili yako na pindi picha ya kichwani ikagongana na mtu wa nje, unaweza kujikuta miguu inakuwa mizito kwenda mbele japo moyo wako unakusukuma uendelee tu kutulia na huku akili ikiwa katika bumbuazi!

Na vilevile unaweza kuwa mpenzi wa magari, lakini yako aina ya magari unayoyapendelea sana na pindi ukiyapata basi hapo sasa unaona au unajiona unaendesha gari la ndoto yako, na kupata raha isiyo ya kifani ndani yako.

Naaaam hiyo inaitwa……………..Nguvu ya uchaguzi/upekee wako!

Karibu katika somo!

Unaweza sema unapenda kazi fulani maana ukiipata unaifurahia sana, lakini ni vizuri kujiuliza kitu gani kina kuvutia hasa hata ujumuishe na kusema kazi hile/ hii naipenda sana.

Unapoweza kujibu swala hili kiufasaha, ndilo litakupelekea kudumu hapo au kuwa hapo kwa muda mfupi, mathalani unaweza sema napenda sana kazi ya upolisi labda utrafic kwakuwa unaona pindi utakapo kuwa barabarani elfu tano ( 5,000 ) au elfu kumu ( 10,000 ) hautaweza kukosa, hiyo ni mbali na posho na mshahara na maisha yako ya kasonga kwa wepesi.

Pia, unaweza jikuta unapenda sana kuwa wakili (mwanasheria) lakini hapo unaweza ukawa unalenga upataji wa hela kwa urahisi kwa kiasi kikubwa kutoka kwa waalifu au wasiojua sheria na waoga ili uwafichie maovu yao ili maisha yako yaende, pasipo kujali maumivu ya mwingine, na inawezekana kabisa kuwa mwanzoni ukuipenda kazi hiyo kwa lengo hilo lakini ukakutana na mfumo uliopo pale, na tamaa yako ikavutiwa zaidi ya vitu visivyo sawa, hatimaye ukabadilika.

Mbali na hayo pia unaweza kuta mtu anapenda sana aina fulani ya nyumba lakini inawezekana ni  kuonyesha na ufahari au pesa alizonazo tu.

NOTE; tunaweza sema haya yote ni maisha na kila mtu anapaswa kuishi sawa na aonavyo au awezavyo japo ni muhimu kuzingatia kutokua kero kwa mtu mwingine isiyo na sababu ya msingi.

Tuendelee kidogo………………..

Tukianza kusema na neno KUPENDA kwa tafsiri nyepesi tunasema ni matokeo ya macho kuona au masikio kusikia na kupata nafasi katika akili yako na huku ukiruhusu moyo kuzalisha shauku ya kupata hicho kitu kwa gharama au namna yoyote.

Nakubaliana sana, hasa katika ulimwengu wa sasa msemo unaosema “ easy come easy go” sio kwa watu wote ila kwa kiasi kikubwa huu msemo umebeba uhalisia katika jamii tuliyonayo.

Nakubaliana kabisa kuna raha inazaliwa ndani ya moyo wa mtu pindi anapotambua anapendwa sana na mtu anayependwa uwa hata mwendo wake unaweza badilika, naam hata kupelekea maisha kubadilika kabisa.

NAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAM!

Swali: Ni kweli unampenda mpenzi wako lakini nini hasa kinachosababisha umpende zaidi?

n  Bila shaka hili ni swali linalojibiwa na moyo tu, na mara chache sana ukute limejibiwa na kinywa katika ufasaha/ uhalisia wake.

Kwa kuwa ni jibu lililobeba uhalisia wa hilo penzi.

Napenda kusema swala sio kupenda tu, kwakuwa hata simba wanapendana na kuzaa na baadae wanaweza kula vitoto vyao.

Jambo kubwa ni nini hasa cha zaidi kinachokufanya umpende maana huo ndio msingi wa penzi lenu katika kudumu au kuwa la muda;

-          Unampenda kwa sababu:

a)      Mnaendana,

Pindi mnapo tembea pamoja unaona mfanano katika mwingiliano mzuri wa kimapenzi/mahaba.

Mnakuwa mapacha kwa muda! Pindi mnapotembea………………….!

b)      Unampenda/ unataka mzae watoto wazuri walio na ndoto katika maisha yako.

-          Wako watu wanapenda kuwa na watoto walio chotora wa kiindi, kijerumani, india, Kinyarwanda n.k hivyo utafuta mtu wa namna hiyo sawa na matarajio yake.

-          Pia inawezekana katika upande wa nywele, rangi yake n.k

 

c)      Ukiwa naye matatizo yako na familia yako yatakuwa yamekwisha, zile kero ndogo ndogo zitakoma kabisa.

 

d)     Ukweli huna sababu yoyote ila moyo wako umemuelewa ( umekufa ), ukimuona huyo mtu moyo wako hautulii kabisa unatamani usimame bado unaiona haitoshi unatamani ukae unaona unachelewa na ukiamua kukimbia unaona kama unawai.

Ukweli ziko sababu nyingi zilizo na msingi kwa huyu na kwa mwingine sio za msingi bado zinabaki kuwa ni sababu tu!

Pia ziko sababu nyingi nzuri kuliko hata hizo zinazofanya umpende mtu zaidi,

Katika dunia ya sasa propaganda ( maneno matamu ) ya mwanzoni uwa sio kitu kwa sasa japo anaweza kukusikiliza tu, kwani kuna watu wanauzoefu ( experience ) zaidi ya miaka ya thelathini ( 30 ) hivyo maneno yako sio kitu kwake, ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa ukitaka acheze.

Mapenzi ni kitu kizuri sana ila kinahitaji sana uhalisia wa moyo pamoja na kuruhusu moyo wako utulie hapo.

Ndo maana kwenye mapenzi yenye mwingiliano wa kweli tunaona maendeleo makubwa yakifanyika kutoka hapo, lakini pia tumeshuhudia mateso mengi, talaka hata vifo kutoka katika hali inayosemekana chanzo chake ni mapenzi ( mapenzi yasiyo salama )!

Mapenzi:

i)                    Hayahitaji ushawishi wa mtu/watu ( ndugu, wazazi au marafiki )

-          Wanaweza kukushauri tu lakini kukushurutisha uwe upande fulani au akuchagulie mpenzi lakini maamuzi hilo ni jukumu lako,

ii)                  Yana mwihitaji Mungu, yeye aliyeweka hali ya uhitaji wa ndani yako yeye anajua namna ya kukamilisha huo uhitaji.

iii)                Unahitaji kuelewa ndoa katika hali ya nje na ya ndani, sio kitu kidogo bali ni jambo kubwa linaloweza kuleta usaidizi kuishi katika ndoto zako.

NI HAKI YAKO KUSOMA PIA NI FAIDA YAKO KUAMUA!

INAITWA SIKU! BARIKIWA SANA

Imeandaliwa na:

Cothey Nelson…………………………………………………….……….0764 018535