Kuomba ni zaidi ya kutoa machozi au kulia kwa sauti kubwa hama kusema asante/kupeleka haja zako kwa sauti ya chini huku ukiwa umepiga magoti, japo yote yanawezekana kutokea katika uwanja maombi lakini yanaweza yasimaanishe maombi.
Moja ya sababu ya msingi sana kwanini unaomba ni kwa sababu aliye ndani yako anataka uombe, anajisikia vizuri maana maombi yako ni manukato mbele zake yanawezesha ibada kufanyika na malaika kuwajibika sawa na manukato ya maombi yako.
Napia sababu ya msingi kwa nini unaomba ni kwa ajili ya kuimarisha ushirika wako na Mungu, maana mawasiliano yanajenga ushirika wenye nguvu.
Sifa za muombaji:
- Zipo sifa nyingi lakini hizi ni baadhi tu ya sifa mtu yeyote anayeomba anatakiwa kuwa nazo:
(a) Mjue unayemuomba
- Hatuombi tu kwasababu wengine wanaomba bali tunajimimina mbele zake kwa sababu tuna mjua tunaye muomba.
- Mtu unaye mjua unaujasiri kwenda mbele zake kwa muda wowote kwasababu unaujua moyo wake basi unauhakika kuwa ukimuomba atakupa.
- Ndani ya moyo wa rafiki yako hata ona unamsumbua hata kama wewe utaona unamsumbua bali ataona unamthamini na kujali uwepo wake, maana ungeweza kufa na njaa yako au kupata aibu lakini umeona bora umshirikishe ndugu yako hitaji lako.
“ ukamgongea rafiki yako usiku bila kuchoka kwa kuwa kuna rafiki amekutembelea na wewe hauna chakula………”
Luka 11:5 Akawaambia, Ni nani kwenu aliye na rafiki, akamwendea usiku wa manane, na kumwambia, Rafiki yangu, nikopeshe mikate mitatu,
Luka 11:6 kwa sababu rafiki yangu amefika kwangu, atoka safarini, nami sina kitu cha kuweka mbele yake;
Luka 11:8 Nawaambia ya kwamba, ijapokuwa haondoki ampe kwa kuwa ni rafiki yake, lakini kwa vile asivyoacha kumwomba, ataondoka na kumpa kadiri ya haja yake.
(b) Amini jibu lake au likubali.
- Mungu unapokuwa na ushirika naye hauwezi kukupa kitu kitakachokuumiza au kitakachokuwa na madhara kwako.
“ mkiniomba mkate je! nitawapa jiwe au samaki nitawapa nyoka”
Luka 11:11 Maana ni yupi kwenu aliye baba, ambaye mwanawe akimwomba mkate, atampa jiwe au samaki, badala ya samaki atampa nyoka?
12 Au akimwomba yai, atampa nge?
13 Basi, ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je! Baba aliye mbinguni hatazidi sana kuwapa Roho Mtakatifu hao wamwombao?
- Upendo wa mtu udhihirika pale unapomuomba naye akawajibika katika kile unachomuomba.
- Neno la Mungu haijalishi limekuja katika muonekano upi bali tambua limesheeni mema yako kupita kipimo.
- Unapo liamini jibu la Mungu unarahisisha utendaji wa kimbingu katika jambo unaloliendea au unaloliomba.
- Hofu inaondoa utendaji wa Mungu.
“ mkiomba na kuamini hayo yatakuwa yenu”
Marko 11:24 Kwa sababu hiyo nawaambia, Yo yote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu.
(c) Ishi katika jibu lake
- Unapoomba jambo hakikisha unadumu katika utimilifu wake na kufanya kuwa maisha yako.
Marko 11:23 Amin, nawaambia, Ye yote atakayeuambia mlima huu, Ng'oka ukatupwe baharini, wala asione shaka moyoni mwake, ila aamini kwamba hayo asemayo yametukia, yatakuwa yake.
- Ishara kubwa ya kuamini ni kukiishi kile ulichokiomba, endapo maisha yako yakapingana na kile ulichokiomba matokeo ni ngumu kutokea.
- Kuna baadhi ya majibu ya Mungu yanatoa maelekezo fulani katika maisha yako ili ya dhihirike pindi utakapoamua kuishi humo basi matokeo yatakuwa dhahiri.
“ hata ibrahimu akusita kuto kuamini bali alitiwa nguvu”
Warumi 4:16 Kwa hiyo ilitoka katika imani, iwe kwa njia ya neema, ili kwamba ile ahadi iwe imara kwa wazao wote; si kwa wale wa torati tu, ila na kwa wale wa imani ya Ibrahimu; aliye baba yetu sisi sote;
17 (kama ilivyoandikwa, Nimekuweka kuwa baba wa mataifa mengi); mbele zake yeye aliyemwamini, yaani Mungu, mwenye kuwahuisha wafu, ayatajaye yale yasiyokuwako kana kwamba yamekuwako.
18 Naye aliamini kwa kutarajia yasiyoweza kutarajiwa, ili apate kuwa baba wa mataifa mengi, kama ilivyonenwa, Ndivyo utakavyokuwa uzao wako.
19 Yeye asiyekuwa dhaifu wa imani, alifikiri hali ya mwili wake uliokuwa umekwisha kufa, (akiwa amekwisha kupata umri wa kama miaka mia), na hali ya kufa ya tumbo lake Sara.
20 Lakini akiiona ahadi ya Mungu hakusita kwa kutokuamini, bali alitiwa nguvu kwa imani, akimtukuza Mungu;
21 huku akijua hakika ya kuwa Mungu aweza kufanya yale aliyoahidi.
- Mungu alipomuahidi ibrahimu isaka ili mlazimu ibrahimu kuendelea kuamini na kuishi maisha ya imani hata kama macho yake hayajaona.
Mwache yeye aombe kupitia wewe ( Roho mtakatifu ) maana yeye ndiye mleta majibu yako.
Pia ni muhimu kutambua kwamba atuombi kwasababu tumekosa kazi hivyo tunaitumia nafasi hiyo kwa kufanya maombi, bali ni lazima utambue moja ya kitu kinacholeta uhai katika maisha ya ukristo ni maombi.
Ni vizuri utambue kuwa bila maombi uwezi kuwa salama, maana maombi ufanya utendaji wa anga uwe juu yako, malaika wanakuwa tayari kukusikia na kutekeleza kile walichoamliwa.
- Maombi ni kitu muhimu sana kupita tunavyofikiria au kuwaza, mbingu inasubiri maombi ili shughuli zake ziendelee ni sawasawa na kiwanda kinasubiri malighafi ( raw material ) ili shughuli zianze, na unajua kama hakuna malighafi katika kiwanda watu watakosa kazi ya kufanya ndivyo ilivyo kama hakuna maombi malaika wanakosa kazi ya kufanya.
Katika maombi unamshawishi Mungu kuangalia kuangalia uhitaji wako!
“ haya njooni tusemezane……..”
Isaya 1:18 Haya, njoni, tusemezane, asema Bwana. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu.
Mtoto anapofika hatua ya kuongea na akifika mbele ya mzazi na uhitaji endapo kama hataongea mzazi huweza kuwa vigumu kuuujua uhitaji wake mapema na kuanza kushughulika nao.
Nguvu ya kusimama na kuendelea pia uzalishwa katika maombi, katika maombi wewe ujifunua mbele za Mungu na yeye Mungu uweza kuona mapungufu yako na uhitaji wako na kuachilia vitu vyake kuja kwako ili kukuimarisha zaidi na uwe na nguvu mpya.
Kuna maombi ya ndani au kimyakimya pale roho yako inaposema na Mungu pasipo kinywa chako kutamka Mungu anaanza kukupa nuru katika ufahamu wako na kukujulisha kile unachopaswa kukifanya kwa msaada wako.
Kuomba ni namna nyingine ya kumkumbusha Mungu neno lake na pale palipo na neno lake utendaji wa kimbingu ufanyika.
Unapoishi maisha ya maombi unaifanya roho yako kuwa na afya hivyo kuweza kuvishinda vizuizi vinavyoikabili katika maisha yako.
Ushindi wa kweli upatika katika maombi mwilini udhihirika tu, kama ujamaliza katika ulimwengu wa maombi uwezi kushinda ulimwengu wa mwli,
Ndani ya maombi kuna ramani kamili unaipata ya namna ya kufanya mambo mbalimbali yahusuyo ufalme wa Mungu na maisha yako kwa ujumla.
Unapoishi katika maombi unawezesha nuru katika maisha yako isizimike bali iendelee kuwaka ili uone mwanga katika maisha yako.
Uwa kuna nguvu inadhihirika pindi utakapoingia katika maombi yenye uvuvio wa Roho mtakatifu.
“ walipoomba ardhi ikatikisika…………..”
Matendo 16:24 Naye akiisha kupata amri hii akawatupa katika chumba cha ndani, akawafunga miguu kwa mkatale.
25 Lakini panapo usiku wa manane Paulo na Sila walikuwa wakimwomba Mungu na kumwimbia nyimbo za kumsifu, na wafungwa wengine walikuwa wakiwasikiliza.
26 Ghafula pakawa tetemeko kuu la nchi, hata misingi ya gereza ikatikisika, na mara hiyo milango ikafunguka, vifungo vya wote vikalegezwa.
Katika kuomba Mungu anakupa maelekezo yake na pindi utakapoamua kuyaishi wewe ufanyika kuwa furaha ya Mungu na Mungu anapofurahia maisha yako hayatabaki kama vile yalivyo.
Ndani ya maombi Mungu anaifunua nafasi yako na kukupa neema ya kuishi katika ukamilifu wake.
Pia ndani ya maombi hekima uzaliwa maana Mungu ukufunulia watu jinsi walivyo na namna ya kuenendana nao katika kuimarisha ushirika wako na Mungu,
Unahitaji kuyapenda maombi ili uyajue au ulijue PENZI LA MUNGU jinsi lililivyo katika Ukubwa na mapana yake.
INAITWA SIKU! BARIKIWA SANA
Imeandaliwa na:
Cothey Nelson…………………………………………………………..0764 018535