“ KUFUNGULIWA” hili neno limebeba furaha ya watu wengi, maana wanajua hapo ndipo chanzo cha uhuru wao.
Uwa kifungo nikifungo tu, haijalishi ni kidogo au kikubwa kwa kuwa ni mahala unaishi nje ya utashi wako, amani na furaha ya kweli inakuwa adimu.
Vipo vifungo ambavyo unaingia kwa kutaka au kwakutegemea mathalani mtu anapanga kufanya uhalifu huku akijua kabisa jera itamuhusu ndo unakuta mtu anasema “ tutagawana majengo ya serikali mmoja atakuwa hospitali na mwingine jera” na wengine kutotegemea wakajikuta wapo kifungoni au katika mazingira ya kusababisha kuwa kifungoni.
Bila shaka mlango unapofunguliwa nawe ukajikuta uko nje au uko huru na inawezekana ulikuwa unaliona jua kwa mara ya nyingine tena toka muda mrefu, kwa maana rahisi maisha sasa unayashika mwenyewe na sio kushikiwa na mtu mwingine.
Bila shaka unapoishi kifungoni ikatokea umetoka kifungoni ukaanza kuyaona mambo yale ambayo ulikuwa uyaoni ulipokuwa kifungoni lakini hayo mambo usipokuwa mwangalifu yanaweza kukusaidia au kukuharibu kwa namna nyingine.
Nakubaliana kabisa kuna faida kubwa kuishi katika uhuru lakini usipoutumia huo uhuru vizuri unaweza kuwa ni chanzo cha uharibifu kwako.
Karibu katika somo!
Ninaposikia kuwa “mlango umefunguliwa” inanikumbusha nilipokuwa shule ya msingi ( 2003 ) kengeleinapo gungwa na mlango kufunguliwa wanafunzi wote tunakuwa na furaha na ndelemo tayari kwa kuelekea nyumbani.
Katika dunia tunayoishi imefunikwa na neema kubwa ( maendeleo ya sayansi na teknolojia-mtandao ) sijajua kutoka wapi?
- Yale yalikuwa mafichoni sasa yamekuwa hadharani.
- Yale yaliyokuwa siri sasa hivi sio siri tena
- Yale yalikuwa magumu kupatikana sasa hivi yanapatikana kwa urahisi sana ( no confidential )
- Yale yaliyokuwa hayaonekani sasa hivi ukifungua tu yanaonekana kwa wingi wa kutosha.
Nipende kusema si kila mlango ulifunguliwa basi unapaswa kuingia ndani hata kama umekaribishwa kwa ukarimu gani maana baadhi ya mahali pengine ukiingia unaweza kuua hatma yako kama nguvu yako ni ndogo.
Huyu ndugu yetu mtandao amekuwa akicheza nafasi nyingi mojawapo ni kuharibu watu wa rika zote sio watoto wala watuwazima na hata waliookoka na wasiookoka naam sio walikuwa katika ndoa tu hata wasiokuwa katika ndoa.
Mitandao imeingiza sumu na hatakudondosha mbuyu uliokaa kwa miaka mia moja, maana sumu yake ni kali hata mbuyu unashindwa kuimiri na kudondoka.
Mahusiano yaliyojengwa kwa miaka mingi yanaweza kuvunjika katika siku moja isiyo na jina haijalishi yalijikita mizizi kiasi gani?
Mtandao unakuaminisha mambo ambayo upaswi kuyaamini! Unakufanya ufanye mambo ambayo ukupaswa kufanya!
Ila matokeo yanapotokea na unapoanza kujuta hapo rafiki mtandao hawezi kukusaidia,
Ni kweli kabisa dunia imefungua mlango na kukukaribisha kuingia lakini kwanza angalia usalama wako ili usije ukaingia mahali ambapo ukupaswa kuingia.
Naam kweli watu wanaweza kukukaribisha usipende kuingia tu kwasababu umechoka au ukaingia na kula kwa sababu unanjaa maana baadhi ya chakula vina sumu badala ya kwenda kuujenga mwili wako una kwenda kuharibu na kuleta umauti katika maisha yako.
Nakubaliana kabisa kuwa mitandao sio mibaya kwasababu yana namna moja au nyingine umefika na umekuwa pale ulipofika katika hali ya faida lakini watu wengi wanasema sio nzuri kwa sababu ya matokeo hasi katika maisha yao.
Utakiwi kucheka kwasababu watu wanacheka bali cheka kwasababu wewe unaona sababu ya kucheka maana hiyo itakuwa na maana nzuri kwako.
INAITWA SIKU! BARIKIWA SANA
Imeandaliwa na:
Cothey Nelson…………………………………………..………….0764 018535
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni