Ni kweli kabisa unaweza penda sana na kujisikia fahari pale unaposikia neno hili kumtegemea Mungu, kama ngao katika maisha yako………maana hata dunia inatambua ukiweka tumaini kwa Mungu basi maisha yako, yako salama!
Naam ni kweli unaweza kutokuwa halisi katika mambo mengi na watu wasikugundue/kutambua mathalani unaweza ukawa na njaa lakini ukataka watu waamini kuwa umeshiba na watu wakaamini hivyo kwa urahisi kabisa.
Pia unaweza kuwa katika hali mbaya inayoleta au sababisha maumivu katika moyo wako lakini unaweza kujitahidi kuficha huo ukweli usijulikane badala yake ukataka watu wakuone kuwa mwenye furaha isiyo na kifani na kicheko ndio maisha yako…….unaweza ita ni hekima! Sawa.
Lakini twende mbele na kurudi nyuma mtu anayemtegemea Mungu ujue ukimuona huyo ujue umemuona Mungu mwenyewe naam na ni Mungu anaishi kupitia yeye, maana unakuwa ni muunganiko unaozalisha kitu kimoja.
Kwa uhalisia mbele za Mungu uwezi kuonyesha kuwa unamtegemea Mungu na huku haumtegemei yeye ni seme tu udhihirisho wa mtu anayemtegemea Mungu sio swala la kuhisi au kukisikia bali ni kishindo chenye uvivuo wa nguvu za Mungu,
Uwa hatusemi sisi kuwa tuna mtegemea Mungu bali udhihirisho wake ndio utaonyesha kuwa tunamtegemea na sisi kuwa watu wake.
Mambo mengi yanayoendelea katika dunia ya leo kwa asilimia kubwa yanachangia kuondoa uhalisia wa kumtegemea Mungu badala yake kuna na namna ya kufikirika zaidi kuliko uhalisia uliopo.
Mathalani watu uweza kutoa ongo katika kupata kazi au haki yake na baadae kuona ni Mungu amefanya, watu uweza kusababisha fitina kati ya bosi na mfanyakazi au mtu na mchumba/mke wake ili mradi huyo atoke na aingie yeye…..wakibebwa na kauli ambayo haipo kwenye biblia kuwa” jisaidie nami nitakusaidia”
Ukweli kwamba kumtegemea Mungu sio kujua kuhubiri au kuweza kufungua watu japo hayo yanaweza kuwa ni udhihirisho mdogo wa kumtegemea Mungu, kwani unaweza fanya yote lakini bado usimtegemee Mungu.
Ni vizuri kutambua kuwa Mungu atafuti watunzaji wa zuri wa biblia au waaminifu katika kuudhuria vipindi kanisani bali wanaomtegemea yeye wanao muonyesha kama alivyo katika jamii hata ulimwengu wote katika uweza na nguvu zake.
Unapoishi maisha ya kumtegemea Mungu unakuwa na maisha ambayo yanakufanya kuwa wewe ni kioo kiasi kwamba watu wakikuangalia wewe wanaona utendaji mkamilifu wa Mungu.
Kitu kikubwa kitakacho dhihiirisha kuwa wewe unamtegemea Mungu ni hile hali kamilifu ya kukubali GHARAMA ya kumsikia na kuishi humo ( utii ) kama hakuna utii wa kujidhabihu hapo haiwezekani kumtegemea Mungu.
Kumtegemea Mungu ni kuishi anavyotaka sio kama unavyotaka, kuishi katika sauti yake pasipo kuangalia kushoto au kulia,
Mwanzo 22:12 Akasema, Usimnyoshee kijana mkono wako, wala usimtendee neno; kwa maana sasa ninajua ya kuwa unamcha Mungu, iwapo hukunizuilia mwanao, mwanao wa pekee.
Kumtegemea Mungu sio kama dunia inavyoenda/inavyo amini bali neno la Mungu linavyosema na hapa pamekuwa ni tanzi kubwa kwa waliokoka.
Kujiingiza katika ubazilifu wa dunia ( Rushwa ) bila kutoa rushwa hauwezi kupata haki yako.
Hivyo mtu uweza kutoa rushwa na baada ya kupata hicho kitu kwa njia zake na sio za Mungu ukaenda kutoa shukrani kanisani.
Mtegemee Mungu ili akutegemeze!
INAITWA SIKU! BARIKIWA SANA
Imeandaliwa na:
Cothey Nelson……………………………………………………….0764 018535