Msingi kama kitu muhimu na cha kwanza cha kufanya/kuzingatia kabla ujafanya jambo lolote……..mathalani unapotaka kufanya biashara lazima uhakikishe una msingi unaokidhi hio biashara naam unapotaka kujenga nyumba lazima kwanza uanze na ujenzi wa msingi.
Katika ulimwengu wa kuzaliwa………kuna furaha ya kuwa wa kwanza pia kuna gharama za kuwa wa kwanza maana wewe ndio unakuwa kioo cha kufuatwa na wengine.
Moja kilio cha watu wengi kama sio wazazi wote ni kuona mtoto wa kwanza akienda katika njia ambayo mzazi anajua hatakuwa na maisha bora/mazuri baadae…….maana mtoto wa kwanza ndio zao la kwanza la tumbo lake au anaitwa kifungua mimba muda wote wazazi wanatamani wamuone maana ni mtoto wa ujana wao.
Bila shaka ni mtoto pekee anayependwa pasipo kuangalia jinsia yake kwa wazazi wengi japo baadhi ya wazazi au jamii inaweza kutarajia kuwa mtoto wa kwanza msicha au mvulana kutokana na taratibu zake au matarajio yao.
Naam mtoto wa kwanza ni mtoto anayependwa na wazazi wake na kuwekewa matarajio makubwa sawasawa na uwezo walionao au wakati mwingine hata zaidi ya uwezo wao huku waki mwamini Mungu,
Baadhi ya familia mtoto wa kwanza anapozaliwa panaweza kutokea na mkesha usiopangwa na usingizi ukapaa pasipo kutarajia kwa furaha kuu inayotawala mioyoni mwao na umakini uliopitiliza.
Kwa asilimia kubwa inategemewa/inaaminika kuwa mtoto wa kwanza ndio mwangalizi wa wadogo zake na ndio mfano au mwelekeza njia na inawezekana kuwa ndio msimamizi mkuu wa mali za familia, hata katika upande wa urithi anaangaliwa kwa umaalumu wake,
Maana inaaminika kwa kiasi kikubwa yeye anawatambua wazazi wake wanapenda nini na nini hawapendi ( maana alishafundishwa ) hivyo inategemewa yeye kuwa mwalimu wa wadogo zake.
Japo anaweza kukua na ikatokea asiwe vile ambavyo wazazi walitegemea awe, japo ataendelea kuwa mtoto wa kwanza lakini baadhi ya majukumu atanyang’anywa hama kupunguziwa au kupatiwa msaidizi inategemea na uhakika wa wazazi juu ya huyo mtoto.
Karibu sana!
Kwa namna yoyote kitu kikubwa kinachoweza kuumiza kichwa ni namna gani nitaanza na je! Lile ninalolikusudia litakuwa kama ninavyokusudia au itakuwa tofauti.
Mara nyingi katika ujenzi wa nyumba ikitokea fundi ameweza kuset vizuri msingi katika viwango vyake basi kuendelea na ujenzi hilo swala linakuwa hana wasiwasi nalo japo umakini utahitajika kwa kile alichikianzisha ili kiiendelee vizuri zaidi.
Ni kweli kila kitu kina gharama lakini sio gharama ya msingi kuna gharama kubwa ambayo yesu aliingia ili atengeneze msingi wa uwokovu wetu nasi tuweze kuendelea vyema sawa na kusudi lake.
Ni rahisi kurekebisha kitu kikarekebishika kuliko nyumba kubwa iliyojengwa katika msingi ulikosewa gharama yake inakuwa ni kubwa mathalani unapokuwa safarini pindi ukakosea mwelekeo katikati ya safari unaweza kubadilisha mwelekeo na kuanza upya, kuliko ukamalishe jambo fulani alafu ukagundua msingi umekosewa hivyo inabidi uharibu kila kitu ili uanze moja.
Hauhitaji kulaumu kwanini mchungwa huu umezaa machungwa machachu bali tafuta kujua mbegu yake ilikuwa ya namna gani maana vile mbegu ilivyo ndivyo matokeo yake yatakavyokuwa huna haja ya kulaumu mchungwa bali badilisha mbegu yake basi matokeo yatabadilika sawasawa na radha inayotokana na hiyo mbegu.
Mambo mengi yanapo wakuta watu katika siku za leo kwa asilimia kubwa yanatokana na misingi walio jengewa hapo nyuma au kujijengea wenyewe kwa kujua au kutokujua.
Kwasababu ili mtu abadilishwe ni lazima ubadilishe msingi ( chanzo ) au mfumo unaotawala maisha yake.
Na kwa maana rahisi pindi usipotambua misingi gani inayotawala maisha yako ni vigumu kutoka hapo hata kama wakikuombea kwa namna gani au kwa mtindo wowote maadamu hujui msingi unaoshikilia maisha yako ni ngumu kutoka hapo au kuwa salama katika mazingira hayo.
Unahitaji kufunuliwa na neno la Mungu katika kutambua msingi gani unaotawala maisha yako , na liruhusu neno la Mungu likague moyo wako pindi unaposoma ukiongozwa na Roho mtakatifu maana yeye anaweza kubomoa misingi isiyofaa na kuweka misingi yakewakati mwingine utumia watumishi wake kukuonyesha wapi umeshikiliwa lakini kazi ya ukombozi kamili ni Mungu mwenyewe.
Ni kweli kuna maisha unaweza ukaishi ukaona sawa unaishi kumbe kuna maisha uliyokusudiwa tangu kuumbwa kwa dunia na uwezi kuyaona na kuyaishi kwa kuwa msingi mbovu umeshikilia afya yako, uchumi wako, mahusiano yako na mengine yote.
Ni muhimu kutambua kwamba hatuishi kwasababu wengine wanaishi hivi au vile bali tunaishi kwa mpango kamili wa Mungu sawasawa na ahadi yake na sio tunavyohisi au tunavyojua.
Mungu ajakusudia uishi vyovyote bali katika misingi ya NENO LAKE!
Hili neno ndilo linakutambulisha na kukujuza kujua wapi kuko sawa na wapi hakuko sawa!
Wapi pa bomolewe na wapi pajengwe!
INAITWA SIKU! BARIKIWA SANA
Imeandaliwa na:
Cothey Nelson………………………………………….……………..0764 018535
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni