Ijumaa, 25 Agosti 2023

FAHARI YA MUNGU!

 

MUNGU UMTAFUTA MTU AMBAYE FAHARI YAKE NI YEYE TU.


 

Katika dunia tuliyonayo kuna vitu mtu akiwa navyo vinamfanya ajisikie mtu katika watu!

Na ni kitu kizuri, maana ni fahari ya kila mtu kuishi katika dunia anayoipenda na vile anavyopenda maana katika hali hii inaweza kupelekea hata afya ya hisia za mtu husika kuwa njema.

Ni kama mke/mme haoni fahari tu kwa mali wanazomiliki kama familia bali fahari yake inakuwa au inaongezeka sana kwakuona mwenzi wake ndio anakuwa fahari yake ya kwanza hata kama vyote vikipotea na akibaki na mwenzi wake bado ataendelea kujivunia huyo na kuona kwamba bado yuko salama.

Pia furaha yake uongezeka pale anapojua huyo mwenzi wake yupo kwa ajili ya matumizi yake tu,

Na Mungu upenda kuona fahari kwa watu wake maana Mungu utafuta mtu ambaye akikosa vyote bado mtu huyo atakuwa fahari yake ni Mungu tu,

Watu walikosa vyote lakini walibaki na Mungu tu:

i.                    Daudi

-          Roho wako usiniondelee……….ni kweli sipo huku au kule lakini nibaki na neema yako tu! Hayo ni maneno ya daudi akiwa katika hali ya maombi mbele za Mungu.

Zaburi 51:11 Usinitenge na uso wako, Wala roho yako mtakatifu usiniondolee.

ii.                  Ayubu

-          Tupate mazuri tu na mabaya apate nani?

Ayubu 2:10 Lakini yeye akamwambia, Wewe wanena kama mmoja wa hao wanawake wapumbavu anenavyo. Je! Tupate mema mkononi mwa Mungu, nasi tusipate na mabaya? Katika mambo hayo yote Ayubu hakufanya dhambi kwa midomo yake.

Ayubu aliweza kumuona Mungu hata pale katika hali ya ubinadamu ungeona hauna sababu ya kuona wema wa Mungu katika maisha yako.

Naam katika maisha ya kawaida uwa ina vunja moyo tu kuona mtu thamani yake ni ndogo kuliko vitu mathalani unaweza kuwa na mchumba, mke au wafanyakazi pindi mtu huyo atakapotambua kuwa thamani yake ni ndogo kuliko gari au kiatu chako maana unaweza kukuta mtu yuko tayari akupoteze wewe kuliko kupoteza kiatu chake cha thamani.

Hali hiyo upelekea zaidi ya mtu kuweka mkazo wake kwenye  kitu kuliko mtu na bila shaka hali hiyo inaweza kupelekea kuvunjika katika mahusiano hata kama atavumilia kwa kiasi gani kuna kipindi kitafika atashindwa kuendelea na uvumilivu.

Mathalani bosi anaweza kumuuliza mfanyakazi wake kwanini ujafanya hili na lile katika majukumu yako, wakati mtu huyo anaweza kuwa alilazwa hospital na ripoti ameshatoa ofisini lakini bosi anataka majukumu yake ayafanye hata kama afya yake haiwezi kumruhusu kufanya hivyo ili mradi tu anamlipa mshahara ni mateso yasiyokuwa na sababu.

Watu wengi ( waliookoka ) uamini sana namna anavyojiweka/anavyoonekana kwa watu ndivyo hivyo Mungu anamuona, inawezekana fahari uliyonayo vile watu wanavyokuabudu unaweza  fikiri huko mbinguni  na Mungu anakupigia makofi kwahiyo mtu huyo anaweza kujisahau na kujua kuwa pesa zake zinaweza kufanya kila kitu na pengine uweza kujisahau na kuona kuwa hiyo pesa yake aliyonayo inaweza kununua hata uzima.

Ni kweli Mungu anataka tuwe na fahari zote maana alituumba ili tutawale dunia na vyote vilivyopo…na muhimu utambue kuwa na dunia inatoa vitu vyake hivyo inaweza kukupa na ukajua Mungu amekupa ukashangaa unapotea.

Mwanzo 1:26 Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi. ( kusudi la Mungu )

Luka 4:5 Akampandisha juu, akamwonyesha milki zote za ulimwengu kwa dakika moja.

            6 Ibilisi akamwambia, Nitakupa wewe enzi hii yote, na fahari yake, kwa kuwa imo mikononi mwangu, nami humpa ye yote kama nipendavyo.

           7 Basi, wewe ukisujudu mbele yangu yote yatakuwa yako.

            8 Yesu akajibu akamwambia, Imeandikwa, Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake. ( ushawishi wa shetani )

 

Paulo “ mtu akiona fahari haone fahari kwa kuwa anamjua Mungu………..”

Galatians 6:14 Lakini mimi, hasha, nisione fahari juu ya kitu cho chote ila msalaba wa Bwana wetu Yesu Kristo, ambao kwa huo ulimwengu umesulibishwa kwangu, na mimi kwa ulimwengu.

Mungu sio kwamba hataki tuishi ya furaha na kicheko ila anataka hivyo vitu vitokane na yeye na sio vitu vingine.

Unahitaji kuona kuwa Mungu ni kitu cha fahari kwako cha kwanza na vingine viwe na nafasi inayofuata ifike mahali uweze kuwa tayari kupoteza vitu vyote ili umpate Mungu maana ni yeye tu anayeweza kuvirejeza kwako kuliko ukubali kumpoteza Mungu ili uvipate vitu kwakuwa vitu haviwezi kumleta Mungu ila Mungu anaweza kuvileta hivyo vitu.

INAITWA SIKU! BARIKIWA SANA

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson……………………………………………………….0764 018535

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni