Ni haki yako kama binadamu kujua kitu chochote kinachoendelea katika sayari unayoishi inayoitwa dunia, naam kupata habari zinazoendelea na hata kupata mambo mazuri ambayo wengine wanayapata.
Katika dunia tuliyonayo sasa ( sayansi na teknolojia ) inasaidia kupata habari kutoka katika ulimwengu wote ukiwa popote ulipo ( ulimwengu kiganjani kwako )!
Kwasasa jinsi teknolojia ilivyo ya hali ya juu mtu uweza kujua shughuli zake zinazoendelea nyumbani, ofisini na maeneo mengi ambayo yeye anataka kujua maendeleo yake kwa uhakika zaidi hata yeye asipokuwepo eneo hilo.
Hali hii imeendeleza watu kuongeza umakini sana katika utandawazi ili asiwe nyuma na kile kinachoendelea/nyuma ya wakati.
Wakati mwingine watu upenda sana kujua kinachoendelea ulimwenguni, ila kutokana na ukosefu wa vyanzo ( fedha au vifaa ) uishia kutamani tu ila inapotokea mwingine anakuwa na fursa hiyo basi uweze kuambatana na kuyaangalia yale mwenzake anayoyapenda kuyaangalia na hatimaye kuweza kuwa sehemu ya maisha yake.
Naam! Kama binadamu uwa hatupendi kupitwa na mambo tunayoyaona na kuyapenda uwa tunajitahidi kwa gharama yoyote kutunza au kuyafanya ili yaendelee kuwepo.
Ila kwa mambo tunayo yaona ni mabaya, uwa tunapenda yatupite kufumba na kufumbua maana yana kuwa janga kwetu! Japo sio kila linaonekana baya kwako litakuwa baya kwa macho ya mtu mwingine.
Ila mara nyingi atufikirii kuwa kile kinachotufaa leo kinaweza kisiwe cha faida kesho na pia kile tunachokiona akitufai leo kumbe kinaweza kuwa cha faida kesho.
Acha ipite! Wakati mwingine inaweza isiwe rahisi kukubaliana na kauli hii maana kuna vitu vingine inabidi vipite ili vingine vije maana pasipo kupita vingine haviwezi kuja hata kama ulivipenda kiasi gani?.
Kuna baadhi ya vitu inawezekana umevizoea kwa muda fulani ila kuna muda Mungu anataka vitengane nawe unaweza usielewe ukajikuta unapingana na Mungu kana kwamba ulijua kama vitakuja, maana yeye Mungu alivileta kwa namna yake na anapotaka kuleta vingine mwache afanye kama anavyotaka maana Mungu anaona jema kila siku.
Kwa kiasi kikubwa maisha tuliyo nayo au tunayoyaishi yamesharatibiwa na mbingu, na mbingu inapoachilia kitu anajua ukikaa nacho kwa muda fulani kusudi lake litakuwa limekamilika hivyo kusudi lake linapokuwa limekamilika hivyo linapaswa liondoke nawe ubaki salama.
Ila kwa ung’ang’anizi wako chakula kinaweza kuwa sumu baada ya kuwa faida hapo ikawa ni hasara….sawasawa chakula kinaweza kuwa kizuri kikipikwa leo na kuliwa lakini kikisha chacha na kuendelea kuharibika lakini wewe ukakomaa nacho kula tu basi hapo tegemea uharibifu na sio faida tena.
Hivyohivyo unahitaji kuwa makini sana hata kama dunia ipo kiganjani pako lazima uwe na uwezo kujua yale unayoyaangalia ujue yapi ni yako na yapi sio yako maana baadhi ya mambo yametumwa kuua hatma yako haijalishi yanaonekanaje au yanavutia kwa kiasi gani cha muhimu ni kilichobebwa ndani yake (content) ni uuaji au uzima!
Na utajua hichi kitu kimebeba uzima au mauti baada ya kuanza kuona umauti au uzima umeanza kuingia ndani yako!
Japo baadhi ya mambo ya mauti yanaweza yasionekane leo yakatokea baada ya miaka, kwa hiyo wanaweza kufanya yote lengo kubwa kuandaa mauti yako au kuandaa anguko lako.
IPENDE NAFSI YAKO KWA KURUHUSU MAMBO MENGINE YAENDE!
INAITWA SIKU! BARIKIWA SANA
Imeandaliwa na:
Cothey Nelson……………………………………………………………0764 018535
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni