Hatua zako unazotembea ndivyo Mungu anavyotembea? Ni swali tu alihitaji jibu….!
Mawazo yako unayowaza ndivyo Mungu anavyowaza?
Maneno hayo unayonena ndivyo Mungu anavyonena?
Maana sisi tu kazi yake tumetokana na yeye na tu mali yake hivyo vile alivyo ndivyo tulivyo,
Na moja ya sifa inayompa ushindi wa halali kwa mwanariadha ni kukimbia akiwa katika mstari wake, ule mstari alioanzia ndio hakikishe anamalizia ili asipunguziwe point zako.
Naam kuna baadhi ya mambo ambayo mtu anapoyafanya uwa yanaleta furaha kama sio kwa jamii basi familia husika mathalani unaweza kukuta mmoja anapenda siasa basi watu wataanza kumzungumzia na walio na mawazo mema juu yake uweza kusema “ huyu kijana atafika mbali katika safari yake ya siasa na hata kuwa kiongozi mkubwa wanchi”……….na pindi mawazo hayo yanapovaa mwili au kutimia na kuanza kuwatumikia wananchi na kusababisha maendeleo ya sehemu husika, Hivyo faida inakuwa kwa jamii nzima kutokana na maendeleo hayo!
Karibu sana:
Moja ya kitu ambacho kama mkristo kinapaswa kikupe ujasiri sana, sio kwamba unaenda kanisani tu au kwa watu waliookoka bali ni kutembea katika mwendo wa Mungu, maana itakuwa ni Mungu anatembea na sio wewe tena bali ni yeye atakuwa anatembea kwa niaba yako japo wewe utaonekana ukishinda lakini Mungu haonekani japo uweza kudhihihirisha utukufu wake.
Unapotembea katika mwendo wa Mungu jua hapo hakuna kitu kitakachochelewa au kuwahi kwasababu hakuna kikwazo kitakachozuia huo mwendo.
Mahala pengine /mara nyingi mambo ya dunia yanavyoenda yanataka kukupa mwendo wake lakini unakuwa hauna mwelekeo wa kudumu au wa uhakika wa hatma yako.
Unapotaka kumuona Mungu ni lazima utembee katika mwendo wake yaani vile anavyosema ndivyo unavyofanya ( anavyosema simama basi unasimama ) hata bila kuuliza kwanini nisimame maana yeye anaona mbele kule ambako macho yako ya nyama hayaoni.
Usitafute ridhaa yako ndipo ufanye bali fanya sawa na maelekezo unayopewa kwa moyo wa unyenyekevu wote.
Unapoanza kutembea katika mwendo wa Mungu unampa Mungu nafasi ya kutawala mwendo wako na hatimaye uweze kupata matokeo yake yanayodumu na yenye tija katika ufalme wake.
Mungu anatarajia kukuongoza katika hatua zake ili ukamilishe kusudi lake na kwa hilo duniani upo na azidi kukufurahia kwasababu unafanya kitu ulichopaswa kufanya.
Ni muhimu kuruhusu akili yake kuishi katika akili yake kupitia neno lake ili uweze kuwa na mwendo usiochoka au kuishia njiani, chochote ambacho Mungu atakiachilia ndani yako ni kwa ajili ya utukufu wake na hiyo hali itakuimarisha na kufanya uzidi kusonga mbele kwakuwa nguvu zako ni nyingi.
Unahitaji mwendo wa Mungu ili mwendo wako kuwa thabiti nje hapo hakuna mwendo wowote utakaonzisha utakao kuwa na matokeo bora kwako kwakuwa nje yake hakuna uwezesho wake,
Naam nje ya mwendo wa Mungu kuna vipingamizi vingi peke yako hautaweza kushinda maana nguvu zinazotumika kushindana na wewe ni zaidi ya uwezo wako wa asili hivyo hauwezi kuzuia kimwili, hivyo unahitaji nguvu ya Mungu ili uweze kushinda nguvu zinazo kuzunguka.
INAITWA SIKU! BARIKIWA SANA
Imeandaliwa na;
Cothey Nelson……………………………………………………………0764 018535