Ijumaa, 6 Oktoba 2023

MIA MOJA NI BORA KULIKO MILIONI MIA MOJA!

 



Zaburi 84:10 Hakika siku moja katika nyua zako Ni bora kuliko siku elfu. Ningependa kuwa bawabu nyumbani mwa Mungu wangu, Kuliko kukaa katika hema za uovu.

Thamani yako mbele za Mungu sio kuwa na kitu bali ni kuwa na kitu ambacho amekupatia yeye.

Furaha ya mwanaume sio kuona mke wake mjamzito tu bali uona fahari kuona huo ujauzito alionao mke wake yeye ndiye muhusika.

Nje ya muongozo wake katika kupata kitu ni ngumu  kudumu na hicho kitu kwa kuwa nje yake yeye hakuna kitu kinawezi kushikilia hayo mafanikio.

Pia ni vizuri kufahamu kuwa nje ya Mungu umiliki wowote unagharama zake, hasa katika utunzaji wake, wakati mwingine unaweza kuhatarisha maisha yako kwa ajili ya kuficha ukweli.

Na ni ukweli usiopingika kuwa ni kusudi la Mungu tuwe na furaha kamili katika maisha yetu na mali ni moja ya chanzo cha furaha japo sio furaha ya kudumu, bali kutokana na uhakika ongezeko la furaha yako na mifupa yako inakuwa salama.

“ Ni bora mia moja ya halali kuliko milioni mia moja ya ubadhilifu”

Ni kweli tunajua tunahitaji kuishi maisha ya mamilioni lakini ni lazima tuanze na moja ili kuelekea kwenye milioni.

Mungu anapoamua kukufanya kuwa tajiri uwa anafanya kwa raha zake mwenyewe/kusudi lake, hivyo ni muhimu utumie huo utajiri kwa namna yake, japo wewe binafsi utanufaidika nao lakini usisahau kufanyika baraka kwa wengine.

Ni vizuri utambue kwamba ukianza na mia moja uwa ni tabia ya Mungu kukuzidisha.

Ndomana biblia inasema ukiwa mwaminifu kwa machache Mungu anakuweka katika kufanya makubwa zaidi.

Mathayo 25:23 Bwana wake akamwambia, Vema, mtumwa mwema na mwaminifu; ulikuwa mwaminifu kwa machache, nitakuweka juu ya mengi; ingia katika furaha ya bwana wako.

Siri kubwa katika kauli hii ni lazima uridhike kwanza na kile alichokupa Mungu hata kama ni kidogo kiasi gani? Maana ndani ya shukrani kuna mazidisho bali lawama kuna kuchukuliwa vyote ulivyopewa kuwa navyo.

Kwa asilimia kubwa watu wengi wakiwekewa kati ya mia na milioni bila shaka watachagua milioni pasipo kujua kwa nini ni chague milioni na sio mia? kwa asilimia kubwa mtu uona uhitaji uliombele yake na huo ndio unaomsukuma pasipo kujali gharama zitakazotokana na uchaguzi atakaoufanya.

Ni kweli kuwa na maisha mazuri ni jambo linalo vutia watu wengi kama sio wote lakini swali ni kwamba hayo maisha yanakujaje na gharama zake ni zipi? Unaweza kujikuta baada ya kupata kile unachokiona ni kizuri ukakukata maisha yako yakaingia katika gharama kubwa hata yakaondoa kabisa furaha uliyokuwa nayo.

Unaweza kuwa ni binti ukatokea umempenda mtu mwenye miliki zake ( kupenda sio dhambi bali kile kinachokusukuma kupenda kinaweza kupelekea dhambi ), ikatokea mmefunga ndoa maisha yakaanza ikawa ni mwendo wa kuku na mrija ( unakula unachokitaka na sio kinachopatikana )….ikatokea ukagundua kuwa kazi anayoifanya ni ujambazi na umwagaji damu wa watu wasio na hatia ndio fahari yake au utajiri wake na ikatokea siku moja mmepishana akakujeruhi jeraha litakalo hatarisha maisha yako……………Nini maamuzi yako! Itakutegemea wewe binafsi katika halmashauri ya kichwa chako.

Japo ni wazi kuwa hekima ya maskini haisikilizwi hata akiongea kwa namna gani?

Ikumbukwe kuwa utajiri ni kitu kizuri na Mungu anataka tuishi humo, lakini muache Mungu akuingize kwenye utajiri wake na sio wako wala wa dunia, maana utajiri wa Mungu hauna majuto.

Na raha yake inakuwa zaidi ya utajiri ulionao.

INAITWA SIKU! BARIKIWA SANA

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson……………………………………………………………0764 018535

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni