Ijumaa, 24 Novemba 2023

NI KWASABABU YAKO:

 



Ø  Kufanya kitu sio tatizo maana hayo ndio maisha lakini endapo ukaamua kufanya kitu kwa ajili ya mtu mwingine hilo linakuwa ni jambo lingine na lenye mtazamo mwingine likiambatana na mguso mwingine.

Ø  Figo inaposhindwa kufanya katika viwango vyake na unapoenda hospitali kupata matibabu yake hilo ni jambo linalotarajiwa na watu wengi lakini endapo utaenda hospitali kwa ajili ya kutoa figo kwa ajili ya mtu mwingine ili aweze kuishi hilo ni jambo lingine lenye kuonyesha upendo wa namna yake. ( unahatarisha maisha yako kwa ajili ya mtu mwingine )!

Ø  Naam…….Kitendo cha kulia kinawezekana kuwa ni jambo la kawaida kutokana na majira na matukio fulani yanayo mkumba mtu lakini inapotokea unalia kwa ajili ya mtu mwingine linakuwa ni swala lingine lenye mtazamo mwingine wenye thamani nyingine,

-          Mathalani kumuona mtu analia unaweza kumpita tu au kutoa kauli ya pole kisha kuendelea na shughuli zako lakini pindi utakapojua kuwa analia kwa ajili yako hapo unaweza kuvuta subira na kutaka kuwa naye karibu hasa endapo kama hauta tambua kwanini anakulilia, kwakua utataka kujua kwanini ameamua kulia kwa ajili yako na wala sio mtu mwingine.

Ø  Pia………Ni jambo la kawaida kumuona mtu ameshika jembe na kuelekea shambani hasa katika mazingira ya vijijini, wakati mwingine ana kwenda asubuhi sana akiwa amebeba kidumu cha maji na jembe pamoja na panga, anakwenda shambani huku akijua amemuacha mke na watoto wake hivyo amebeba majukumu mabegani mwake akiwa anawaza tu kule aendako na familia aliyoaicha nyumbani na wakati mwingine hata bila kujijali yeye mwenyewe bali wale wanao muhusu tu ( familia ) na wakati mwingine anarudi jioni sana akiwa amechoka sana akili, hisia na kimawazo pamoja na mwili lakini bado atawaza kesho kwenda tena.

Ø  Vilevile unaweza kukuta mtu asubuhi na mapema tayari yuko barabarani akigombania magari/mabasi ya kwenda kwenye shughuli zake ( hasa maeneo ya mjini ) uwaacha jamii inayomzunguka na kumtegemea/kumuhitaji anaenda kutafuta kwa ajili yao, mvua na jua vyote vinaishia katika mwili wake lakini anakubali hali zote ili mtu mmoja awe salama hama jamii yake kwa ujumla iweze kukaa katika hali njema.

Naam!

-          Hakuna raha unayoipata kama ukisikia au kujua kuwa haya yote mtu anayafanya ni kwa ajili yako tu na wala sio kwa mtu mwingine hama jamii yeyote, na wala sio kwa ajili yake! Amekubali adhalilike au aibike au pengine hata mwili wake kupata shida ili wewe uwe katika namna njema.

-          Bila shaka hakuna mtu asiyependa kuwa na mtu wa namna hii, mtu mwenye kuhakikisha furaha yako haipungui/ huzuni inapita mbali na maisha yako bali utulivu na raha unakuwa matuo ndani yako.

-          Naamini kama ungetambua mtu wa namna hiyo yupo duniani hata kama anaishi pembeni mwa dunia amini ungejipanga kwenda kukutana naye hata kama sio leo au kesho hama wakati muafaka ili siku ukikutana naye maisha yako uyaweke mikononi mwake kwa kuwa utajua maisha yako yatakuwa salama katika matunzo mema.

-          Na ukweli huo ndio mtihani unawakumba wanadamu katika dunia ya leo….anapoona hapa ndipo barafu anashangaa moto umeanza kumchoma na anapofikiri hapa ni sehemu salama ya kupumzika anakuta majani yameanza kumuwasha mpaka inampelekea machafuko kutokea, mauaji na hata chuki iliyokithiri inakuwa katika mioyo ya watu, watu wanatembea huku mioyo yao inavuja damu kwa sababu uliye muamini hakuweza kudumu katika kuaminika.

-          Uzuri ni kwamba yuko Mungu anayekujua na alishakujua kabla ujaja duniani na anajua kuwa ni nani yuko tayari kuibeba aibu yako na kukustili katika hali yoyote utakayo kuwa nayo.

-          Kiukweli una muhitaji Mungu kwanza yeye ndiye anaweza kukutanisha na yeye aliyemkusudia ambaye atakuwa kimvuli salama kwako na sio jangwa.

-          Bidii utakayoitumia katika kumtambua yeye naye atakutambulisha katika mtu atakayekamilisha ndoto yako na sio kuhiharibu.

 

INAITWA KESHO! BARIKIWA SANA.

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson……………………………………………………………………..0764 018535

Jumamosi, 11 Novemba 2023

KUMPENDA MUNGU KAMA NJIA YA UKOMBOZI:



Zaburi 107:20 Hulituma neno lake, huwaponya, Huwatoa katika maangamizo yao.

-          Neno la Mungu lina uwezo kukutoa katika maangamizo yote endapo utalikubali na kulipa nafasi.

Kuna maisha uwa yanaanza pale mtu anapokombolewa, maisha ya kwenye vifungo hayana uhuru na amani timilifu.

Naam ukombozi ni jambo muhimu na baadhi ya wakristo wanaamini kufunguliwa kunakotokana na maombezi ( kwa kiasi kikubwa ) watu uamini hapo nami kwa kiasi kikubwa na kubaliana nao japo na amini ukombozi huu unaweza usiwe wa kudumu.

Lakini napenda kusema kufunguliwa kunakotokana na kumpenda Mungu uwa ni wakudumu kwa asilimia kubwa labda ukengeuke au kuiacha imani.

Uponyaji unaozaliwa katika kumpenda Mungu huu ni uponyaji unaoanza ndani yako ukiruhusiwa na ufahamu wako uliokubali mabadiliko hayo.

Huu uponyaji uwa unajijenga kwa ndani vizuri kabla ujaanza kudhihirika kwa nje na uwa ukipona unapona jumla ( sio ugonjwa wa kujirudiarudia ).

Kama ilivyokuwa uhitaji mkubwa kwa wanadamu ni kupendwa ndivyo ilivyo kwa Mungu haja yake kupendwa!

Na kama watu wanapopendana sana, uweza kupelekea kuishi pamoja, ndivyo hivyo ukimpenda Mungu uwa unaacha vyote na kuamia kwako jumla vile alivyo na vyote alivyonavyo anakuja na kukakaa kwako milele.

Kama unahitaji ufunguzi wa kweli na wakudumu unahitaji kumpenda Mungu kwelikweli, kwa kiwango kile unachompenda ndicho kiwango utaona mema yake katika maisha yako.

Unapompenda kwa kweli unafanya yeye kuwa jukumu la kuhakikisha maisha yako yako salama wakati wote.

Ni kama vile mtu anapougua utegemea dawa/ maelekezo ya daktari yanaseamje: wengine wataambiwa wameze dawa, na wengine kujichua n.k, pindi mgonjwa atakapopewa maelekezo ya kumeza dawa naye akaanza kutumia na baadae akaanza kuona unafuu katika mwili wake basi hizo dawa zimefanikiwa katika lile lengo lililokusudiwa endpo huo unafuu utakamilisha uzima mkamilifu.

Ndivyo ilivyo katika kusudi la Mungu kupitia neno lake unapolimeza/kulisoma linakwenda kupambana na vitu visivyosahihi kukaa ndani yako ikiwemo magonjwa ya kutupiwa/ya kawaida au tabia ngumu katika uwezo uliondani ya neno hakuna kitu kitabaki salama labda neno likose ushirikiano na wewe.

“ ukinipenda utalishika neno langu”

Yohana 14:23 Yesu akajibu, akamwambia, Mtu akinipenda, atalishika neno langu; na Baba yangu atampenda; nasi tutakuja kwake, na kufanya makao kwake.

Unapoamua kulishika neno lake naye Mungu anashika maisha yako na kukufanya vile apendavyo yeye.

Kulishika neno kwa lugha nyepesi tunasema ni kulisikiliza vile linavyotaka na kuamua kufanya sawasawa na lilivyokukuagiza.

Ukiisha katika agizo lake hapo utaona utajiri wa neno ulizaidi ya duniani hata mbinguni.

Unahitaji kumpenda Mungu ili afanyike uzima na nguvu dhidi ya maradhi na uvamizi wowote wa giza.

“UKIMPENDA  ATAKUPENDA”

INAITWA SIKU! BARIKIWA SANA.

Imeandaliwa na:

Cothey Nelson……………………………………………………………………0764 018535