Ijumaa, 26 Aprili 2024

INAONEKANA KAMA MVUA INATAKA KUNYESHA;

 



Sote tunaamini kuwa dalili ya mvua ni mawingu! Pia tunakubaliana pia sio lazima mawingu ya mvua yanapotanda angani basi hapo ni lazima mvua inyeshe, japo kwa asillimia kubwa wingu linapotanda basi mvua inanyesha na majira machache mawingu yanaweza kutanda anagani lakini mvua isinyeshe.

Naam Ni hatari sana kama  kuona uko salama alafu ghafla ukajikuta umevamiwa!

-          Ni bora mazingira yenyewe yange kuonyesha mahali hapo sio salama na akili yako ikaelewa hivyo ungejua namna ya kukaa hapo au kuondoka kuliko kujua kuwa uko salama kumbe hauko salama.

Katika dunia ya sasa watu hawatafutwi kupendwa au kuchukiwa tu bali upenda kuingia mahali ambapo usalama wa nafsi na mwili utakuwa kipaumbele,

-          Maana kuna kuna wakati macho na maneno ya watu wanaweza kukudanganya ukakuta unatupa lulu na kukumbatia jiwe!

Ni hatari sana kunywa maji ukijua kuwa ni salama kabisa kumbe sio salama na muda baada ya kuyanywa hayo maji ikapelekea mwili wako kuwa katika hali mbaya,

Bila shaka katika hali ya ukawaida kuna hali unakuwa nayo pindi unapobaini kuwa kuna janga linakuja lakini pindi linapotokea pasipo kujiandaa athari zake zinakuwa kubwa kiakili na  hata kimwili,

Mathalani wataalamu wanapobashiri kuwa kuna mvua kubwa inakuja na kutoa taadhali kwa watu wanaokaa katika mazingira hatarishi na kutoa ushauri kwa jamii nzima lengo ni katika kupunguza athari yake maana pasipo kuzingatia hilo inaweza kukuta unapoteza maisha ya watu na mali zao,

Kuna baadhi ya mambo yanapotokea katika maisha yako pasipo maandalizi unaweza kujikuta katika mazingira magumu sana mathalani umepata mkopo na wakati unarudi nyumbani ukanyang’anywa na vibaka hali hii inaweza kuzaa maswali mengi kama vile nitawezaje kurudisha marejesho mkopo wakati sina kitu,

Naam “ Dalili ya mvua ni mawingu” lakini sio wakati wote mawingu yanapotanda mawinguni basi mvua itanyesha, japo kwa asilimia kubwa watu wanapoliona wingu la mvua wanakuwa na matumaini ya kupata mvua.

-          Maana kuna wakati wingu la mvua likatanda kwa ukubwa baadae likapotea, na hauwezi kulizuia!

Karibu katika somo:

Kuna mazingira unaweza kujiamini sana kwa kuhisi kuwa Mungu yuko pamoja na wewe, nawe ukajiachia kwa uhuru wote lakini pindi mambo yatakapoenda tofauti na hali yako inakuwa mbaya na kwa mtu unayeenda kanisani anaweza poteza hile hali ya kupenda kwenda kanisani.

Waamuzi 16:18 Delila alipoona ya kuwa amemwambia yote yaliyokuwa moyoni mwake, akatuma mtu akawaita wakuu wa Wafilisti, akisema, Njoni huku mara hii tu, maana ameniambia yote aliyo nayo moyoni mwake. Ndipo wakuu wa Wafilisti wakamwendea wakachukua ile fedha mikononi mwao.

 19 Naye akamlaza usingizi magotini pake. Kisha akamwita mtu akavinyoa vile vishungi saba vya nywele za kichwa chake; akaanza kumsumbua, nguvu zake zikamtoka.

 20 Kisha akasema, Samsoni, Wafilisti wanakujia. Akaamka katika usingizi wake, akasema, Nitakwenda nje kama siku nyingine, na kujinyosha. Lakini hakujua ya kuwa Bwana amemwacha.

-          Unapotembea na  mungu ni muhimu uweze kujua muambatano wa Mungu na wewe lasivyo usipokuwa makini mazingira yatakuonyesha kuwa pale ulikuwa peke yako,

Ni muhimu utambue kuwa hisia peke yake pasipo kuwa na uhakika ni kitu hatari sana ni zaidi na kupitisha moto kwenye kwenye petrol iliyo mwagika katika nyasi kavu.

Na kuna wakati mwingine mazingira ya nje yanaweza yasikupe usaidizi wa kutosha katika jambo unaloliendea ila ukabaki katika kuamini Mungu pasipo na tegemeo lingine hapo udhihirisho unapotokea basi ujasiri na imani vitaongezeka kwa kiasi kikubwa ndani yako.

Na ni muhimu pia mazingira yanapotanda hutakiwi kufikiria ili mvua kunyesha inaweza kuchukua miaka mitatu bali katika mawingu anga linaweza jitengeneza na mvua kuanza kunyesha hata ndani ya saa moja tu,

Ni jambo jema kuwa na uhakika wa mazingira ya nje ila sio ukamilifu wa kila kitu bali inaweza kufanya jambo moja kufanikiwa na upande mwingine ikawa shida iko palepale,

-          Ndo maana sio kila anayetoa tabasamu ana maanisha amevutiwa na wewe wengine wanatamani akumeze na upotee kabisa.

Bali amini sana katika ustawi wa ndani utakaojidhihirisha kwa upande wa nje ambao utakuwa ustawi wa kudumu,

-          Usiishi tu kwa kirizisha akili zako pasipo kupata uhakika katika Mungu.

Matumaini ya nje yasikupe nguvu katika kufanya maamuzi bali katika majira sahihi na maongozi ya Roho mtakatifu ya kweli,

 

INAITWA SIKU! BARIKIWA SANA

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson………………………………………………………………………..0764 018535

Ijumaa, 12 Aprili 2024

PUMZI YA MWISHO!

 

Neno “ mwisho” uwa linaleta tahaluki miongoni mwa watu wengi…….wengine wakihuzunika na wengine wakipata faraja na wengine wakifurahi kama sio kulia japo inategemea ni mwisho wa nini? Na baada ya huo mwisho maisha gani yataendelea,

Katika dunia tuliyopo na kwa asilimia kubwa ya jamii yetu hasa jamii ya kiafrika neno la mwisho linakuwa na nguvu sana maana linaweza kuwa limebeba hitimisho ya mambo mbalimbali na wakati mwingine hili neno linaweza kubeba matamanio halisi ya mtu husika,

Unaweza kukuta mtu anaongea sana lakini mwisho atakavyo malizia ndivyo hasa mtajua nini nia yake au mategemeo yake kama sio matarajio yake.

Neno la mwisho linakuwa na maana kwa mtu mzima au kwa marehemu neno analolitoa kabla ya kufariki ( kuachana mwili na roho)!

“ pumzi ya mwisho” kwa maana katika somo hili….ni mjumuhisho wa akili, hisia na maneno ya mtu ya kihusisha mwisho wa hatua ya kwanza na kuingia hatua ya pili inaweza kuwa katika hali njema au mbaya!

-          Siku zote mwisho wa kitu kimoja ndio mwanzo wa kitu kingine!

Na siku zote mwisho wa kitu uwa una lenga kukuingiza katika hali nyingine haijalishi uko tayari au hauko tayari!

Wakati mwingi unapofikia katika hatua ya mwisho kwa asilimia kubwa unaweza kosa uhakika/ nuru katika hatua unayoingia, mathalani unaweza kukuta mama mjamzito kuna wakati anaweza pata changamoto katika kujifungua hata kupoteza matumaini kabisa katika kupakata kichanga chake au kupoteza maisha yake binafsi na inapotokea Mungu amemsaidia amekuwa salama yeye na mtoto/kichanga chake hapo anakuwa kama ameingia katika dunia anayoipenda japo hapo awali alikuwa amepoteza matumaini au uhakika wake.

Katika hali ya pumzi ya mwisho inaweza ikatokea mtu kufanya shughuli ambayo haina uhusika wa moja kwa moja na kutekeleza ndoto yake mathalani una wazo la biashara ambalo inahitaji kila mwezi uingize million mia tano ( 500,000,000 ) ili mwisho uweze kufanikisha jambo lililo katika ndoto yako, lakini ikatokea mtu huyohuyo hata laki moja huingizi kwa mwezi lakini ukaendelea kufanya ukitegemea ipo siku ndoto yako itatimia , bila shaka kuna wakati unaweza kuchoka na hata kupelekea kuhisi ni kama una hamisha bahari kwenda nchi kavu kwa kijiko, ila usikate tama!

Tambua  lile wazo linaweza kuzalisha njia ambayo ikazalisha mambo mbalimbali na kukamilisha ndoto yako,

Wakati mwingine pumzi ya mwisho inaweza kuonekana kwa mgonjwa katika hali yake ya ndani hata watu wanampenda kiasi gani hali ya ndani inaweza isimpe jicho/ kuona kwa jicho hilo na kujiona amekuwa mzigo kwa watu na kutaka kufariki ili asiendelee kuwa teso kwa wengine, lakini hapo ni lazima pumzi ya mwisho ichukue nafasi inayopoteza muungamaniko na ardhi, inahitaji mbingu ili iweze kuunganisha matarajio yake tena na hatimaye kuwa mzima tena.

Unapaswa kujua ili mradi una pumzi basi ujue kuna muda utafikia na kuwa katika hali ya pumzi ya mwisho,

Pumzi ya mwisho mahala ambapo akili yako inapoteza nguvu ya kujisimamia hata marafiki unaweza kuwaona marafiki sio marafiki tena wala sio maadui ila wapo kama hawapo,

Katika hali hiyo unahitaji kujua kuna kitu kipya kinazaliwa au kuna dunia unaingizwa ambayo hukuwahi kuiona wala kuwa na ndoto kufika hapo.

Unapaswa kujua pumzi ya mwisho sio mwisho wa maisha yako!

INAITWA SIKU! BARIKIWA SANA

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson……………………………………………………………..0764 018535