Neno “ mwisho” uwa linaleta tahaluki miongoni mwa watu wengi…….wengine wakihuzunika na wengine wakipata faraja na wengine wakifurahi kama sio kulia japo inategemea ni mwisho wa nini? Na baada ya huo mwisho maisha gani yataendelea,
Katika dunia tuliyopo na kwa asilimia kubwa ya jamii yetu hasa jamii ya kiafrika neno la mwisho linakuwa na nguvu sana maana linaweza kuwa limebeba hitimisho ya mambo mbalimbali na wakati mwingine hili neno linaweza kubeba matamanio halisi ya mtu husika,
Unaweza kukuta mtu anaongea sana lakini mwisho atakavyo malizia ndivyo hasa mtajua nini nia yake au mategemeo yake kama sio matarajio yake.
Neno la mwisho linakuwa na maana kwa mtu mzima au kwa marehemu neno analolitoa kabla ya kufariki ( kuachana mwili na roho)!
“ pumzi ya mwisho” kwa maana katika somo hili….ni mjumuhisho wa akili, hisia na maneno ya mtu ya kihusisha mwisho wa hatua ya kwanza na kuingia hatua ya pili inaweza kuwa katika hali njema au mbaya!
- Siku zote mwisho wa kitu kimoja ndio mwanzo wa kitu kingine!
Na siku zote mwisho wa kitu uwa una lenga kukuingiza katika hali nyingine haijalishi uko tayari au hauko tayari!
Wakati mwingi unapofikia katika hatua ya mwisho kwa asilimia kubwa unaweza kosa uhakika/ nuru katika hatua unayoingia, mathalani unaweza kukuta mama mjamzito kuna wakati anaweza pata changamoto katika kujifungua hata kupoteza matumaini kabisa katika kupakata kichanga chake au kupoteza maisha yake binafsi na inapotokea Mungu amemsaidia amekuwa salama yeye na mtoto/kichanga chake hapo anakuwa kama ameingia katika dunia anayoipenda japo hapo awali alikuwa amepoteza matumaini au uhakika wake.
Katika hali ya pumzi ya mwisho inaweza ikatokea mtu kufanya shughuli ambayo haina uhusika wa moja kwa moja na kutekeleza ndoto yake mathalani una wazo la biashara ambalo inahitaji kila mwezi uingize million mia tano ( 500,000,000 ) ili mwisho uweze kufanikisha jambo lililo katika ndoto yako, lakini ikatokea mtu huyohuyo hata laki moja huingizi kwa mwezi lakini ukaendelea kufanya ukitegemea ipo siku ndoto yako itatimia , bila shaka kuna wakati unaweza kuchoka na hata kupelekea kuhisi ni kama una hamisha bahari kwenda nchi kavu kwa kijiko, ila usikate tama!
Tambua lile wazo linaweza kuzalisha njia ambayo ikazalisha mambo mbalimbali na kukamilisha ndoto yako,
Wakati mwingine pumzi ya mwisho inaweza kuonekana kwa mgonjwa katika hali yake ya ndani hata watu wanampenda kiasi gani hali ya ndani inaweza isimpe jicho/ kuona kwa jicho hilo na kujiona amekuwa mzigo kwa watu na kutaka kufariki ili asiendelee kuwa teso kwa wengine, lakini hapo ni lazima pumzi ya mwisho ichukue nafasi inayopoteza muungamaniko na ardhi, inahitaji mbingu ili iweze kuunganisha matarajio yake tena na hatimaye kuwa mzima tena.
Unapaswa kujua ili mradi una pumzi basi ujue kuna muda utafikia na kuwa katika hali ya pumzi ya mwisho,
Pumzi ya mwisho mahala ambapo akili yako inapoteza nguvu ya kujisimamia hata marafiki unaweza kuwaona marafiki sio marafiki tena wala sio maadui ila wapo kama hawapo,
Katika hali hiyo unahitaji kujua kuna kitu kipya kinazaliwa au kuna dunia unaingizwa ambayo hukuwahi kuiona wala kuwa na ndoto kufika hapo.
Unapaswa kujua pumzi ya mwisho sio mwisho wa maisha yako!
INAITWA SIKU! BARIKIWA SANA
Imeandaliwa na:
Cothey Nelson……………………………………………………………..0764 018535
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni