Ijumaa, 29 Machi 2024

HAZINA ZA MBINGU:

 



Moja ya kitu kinacholeta changamoto kwa watu wengi ni kuwa na hazina ‘ akiba’ na hili jambo sio changamoto kwa watu tu bali hata kwa nchi, baadhi ya nchi zinapitia wakati mgumu katika majanga yanayo wakabili kwa kukosa hazina au kuto kuwa na hazina ya kutosha.

-          Kuna hazina ya mtu,nchi, bara na dunia! Zote hizo zipo kwa ajili ya kuhakikisha mwanadamu anakuwa salama na amani katika dunia aliyopo.

Moja ya sababu ya utumwa kwa familia au kwa nchi ni pale anapokutana na majanga na kushindwa kupata njia ya kutoka hapo, hivyo ujikuta ana anaingia katika gharama kubwa inayoweza kumgharimu maisha yake yote kwa sababu ya kutokuwa na hazina ya kujikim wakati wa uhitaji na wakati mwingine anaweza fanya mambo yatakato athiri maisha yake yote.

Baadhi ya mambo unayoambiwa kufanya kwasababu ya kukosa kukidhi uhitaji ulionao unaweza kukuacha katika mazingira mabaya hata kuliko maisha yako ya awali kabla uja upokea huo msaada.

Dunia inavyobadilika na akili za binadamu zinabadilika watu wanaishi kwa kutegemea watu wapate majanga ili wao waweze kunufaidika, japo majanga hayachagui mtu wa kumpata ( majanga ya asili )!

Katika biblia kuna kijana aliyeitwa yusufu huyu kijana aliweza kuitangaza nchi ya misri katika ulimwengu wote, kwa kuhakikisha kuwa na hifadhi ya kutosha ya chakula wakati wote hata pale hata wakati mgumu ulipoikumba dunia, bado misri iliweza kujilisha yenyewe na kufanyika msaada mkubwa kwa dunia kwa kuuza chakula chake.

Ni kweli kila jambo kuna majira yake na kama usipoenda sawa na majira yake hakika majuto yanaweza kuwa maisha yako.

Bila shaka kama kuna hazina za mbingu basi kuna hazina za ulimwengu/dunia , na kila miliki inautaratibu wake wa kutoa hizo hazina zake.

Sifa moja kubwa ili upate hazina za mbingu au za dunia ni lazima uzipendee/ uzifurahishe hizo falme zinazo toa hazina.

Japo mbingu na dunia ni mali ya Mungu lakini Mungu ametoa uhuru kwa mwanadamu apate hazina zinazotoka kwake au kwingineko ( shetani )!

Torati 30:15 Angalia, nimekuwekea leo mbele yako uzima na mema, na mauti na mabaya;

Hakuna maana ya kuwa na matumaini ambayo hayapo! Mathalani unapoamua kuitumikia dunia na ukategemea hazina za mbingu ni sawa na kulima maharage ukategemea kuvuna mahindi,

-          Japo kwa kiasi kikubwa mtu uweza kujitambua madhabahu anayoitumikia ndio itakayompa hazina yake, ila wako watu waliokatikati huku wapo na kule wapo wanategemea kupata popote kama bahati nasibu ikitiki kwa Mungu sawa au kwa shetani sawa!

Moja ya hazina njema iliyobeba utajiri  ambao hauwezi kuyaharibu maisha yako ni hazina za mbingu japo kuupata kwake hautegemea kuyaishi matakwa yako bali matakwa yake.

Maana ndiye anayejua kwa nini amekuweka hapo/ amekupa hicho na hajakupa kile,

-          Uwa anafanya akitegemea mwendelezo wa furaha yako  na ustawi wako wa kudumu,

Unapoishi kwa kuitumikia mbingu haijalishi unapitia nini na nani anakuelewa na nani akuelewi bali matumaini ya uhakika yatakuwa katika moyo wako ukiambatana na furaha na amani,

Ayubu “ Namjua Mungu………………………..”

Ayubu 19:25 Lakini mimi najua ya kuwa Mteteaji wangu yu hai, Na ya kuwa hatimaye atasimama juu ya nchi.

Ni muhimu ujue katika mbingu ndio sehemu sahihi ambayo unapaswa kuweka hazina zako kwakuwa wewe asili yako katika mbingu basi kwa hapo hazina yako itakuwa salama,

Unahitaji kuokoka ili uweze kupata kibali kuweka hazina yako mbinguni na kama vile unapotaka kuweka pesa kwenye benki ni lazima uwe na akaunti au ufungue akaunti ndipo mengine yaendelee.

-          Usije ukawa unaweka pesa ukafikiri ni akaunti yako kumbe unaweka kwenye akaunti nyingine na pindi mwenye akaunti anapoamua kuzitumia hizo pesa hivyo wewe unakuwa huna hazina.

Moja na changamoto inayo wakumba watu wanaoweka hazina zao katika mbingu ni kukosa subira kuchelewa kufaidi matunda ya hazina yake.

Wagalatia 6:9 Tena tusichoke katika kutenda mema; maana tutavuna kwa wakati wake, tusipozimia roho.

Tambua unapoweka hazina katika mbingu jua uratibishaji utendaji wake wote unakuwa ni kwa ajili ya faida yako haijalishi utaona inachelewa au kuwahi  bado yote yatakuwa kwa ajili yako na sio kitu kingine.

Ni vema kutulia hata wakati wa njaa ukifika utaona mbingu inavyohusika katika kuyatunza maisha yako kwa namna yake.

INAITWA SIKU! BARIKIWA SANA

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson……………………………………………………………………………………….0764 018535

 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni