Moja ya maisha mazuri unapokuwa hapa duniani ni maisha ya maombi!
Matendo 10:1 Palikuwa na mtu Kaisaria, jina lake Kornelio, akida wa kikosi kilichoitwa Kiitalia,
2 mtu mtauwa, mchaji wa Mungu, yeye na nyumba yake yote, naye alikuwa akiwapa watu sadaka nyingi, na kumwomba Mungu daima.
3 Akaona katika maono waziwazi, kama saa tisa ya mchana, malaika wa Mungu, akimjia na kumwambia, Kornelio!
4 Akamtazama sana, akaogopa akasema, Kuna nini, Bwana? Akamwambia, Sala zako na sadaka zako zimefika juu na kuwa ukumbusho mbele za Mungu.
Ukijua siri iliyo katika maombi hauwezi kuwa mtu wa lawama! Huu ulimwengu unakutambulisha na kupa kuishi katika nafasi yako.
Ayubu 1:1 Palikuwa na mtu katika nchi ya Usi, jina lake alikuwa akiitwa Ayubu; mtu huyo alikuwa mkamilifu na mwelekevu, ni mmoja aliyemcha Mungu, na kuepukana na uovu.
2 Kisha walizaliwa kwake wana saba, na binti watatu.
3 Mali yake nayo yalikuwa ni kondoo elfu saba, na ngamia elfu tatu, na jozi za ng'ombe mia tano, na punda wake mia tano, na watu wa nyumbani wengi sana; basi hivi mtu huyo alikuwa ni mkuu sana kuliko watu wote wa upande wa mashariki.
4 Nao wanawe huenda na kufanya karamu katika nyumba ya kila mmoja wao kwa siku yake; nao wakatuma na kuwaita maumbu yao watatu ili waje kula na kunywa pamoja nao.
5 Basi ilikuwa, hapo hizo siku za karamu zao zilipokuwa zimetimia, Ayubu hutuma kwao akawatakasa, kisha akaamka asubuhi na mapema, na kusongeza sadaka za kuteketezwa kama hesabu yao wote ilivyokuwa; kwani Ayubu alisema, Yumkini kwamba hawa wanangu wamefanya dhambi, na kumkufuru Mungu mioyoni mwao. Ndivyo alivyofanya Ayubu sikuzote.
- Kuwa na mali nyingi hakuondoi nafasi ya wewe kuomba, maana kuomba ndio ustawi wa yale/ shughuli unayoifanya.
Maombi sio ghasia au makele! Bali ni tendo linaloonekana katika mwili bali linatafsiri na nguvu katika ulimwengu wa roho,
Yohana 17:1 Maneno hayo aliyasema Yesu; akainua macho yake kuelekea mbinguni, akasema, Baba, saa imekwisha kufika. Mtukuze Mwanao, ili Mwana wako naye akutukuze wewe;
2 kama vile ulivyompa mamlaka juu ya wote wenye mwili, ili kwamba wote uliompa awape uzima wa milele.
3 Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma.
4 Mimi nimekutukuza duniani, hali nimeimaliza kazi ile uliyonipa niifanye.
5 Na sasa, Baba, unitukuze mimi pamoja nawe, kwa utukufu ule niliokuwa nao pamoja nawe kabla ya ulimwengu kuwako.
6 Jina lako nimewadhihirishia watu wale ulionipa katika ulimwengu; walikuwa wako, ukanipa mimi, na neno lako wamelishika.
7 Sasa wamejua ya kuwa yote uliyonipa yatoka kwako.
8 Kwa kuwa maneno uliyonipa nimewapa wao; nao wakayapokea, wakajua hakika ya kuwa nalitoka kwako, wakasadiki ya kwamba wewe ndiwe uliyenituma.
9 Mimi nawaombea hao; siuombei ulimwengu; bali hao ulionipa, kwa kuwa hao ni wako;
Kama vile uchoki kumuazia mema kwa mtu unaye mpenda ndivyo hivyo upaswi kuchoka kuomba kwa kuwa unampenda,
Yakobo 5:16 Ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana, mpate kuponywa. Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana, akiomba kwa bidii.
17 Eliya alikuwa mwanadamu mwenye tabia moja na sisi, akaomba kwa bidii mvua isinyeshe, na mvua haikunyesha juu ya nchi muda wa miaka mitatu na miezi sita.
Mtu unayempenda unamshirikisha magumu na mazuri unayaopata katika mwenendo wenu wote, maana unajua atakusikiliza na kukupa mwanga katika yale unayoyaendea.
Isaya 1:18 Haya, njoni, tusemezane, asema Bwana. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu.
Wafilipi 4:6 Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu.
Upaswi kuanza kuwa serious na kuomba pale unapokutana na mambo kisha ukakosa jibu huo sio msingi mzuri kuwa endelevu katika maisha yako,
- Hali hiyo itapelekea kuto kujua yule unaye muomba na hali hiyo upelekea kuomba vibaya,
Yakobo 4:3 Hata mwaomba, wala hampati kwa sababu mwaomba vibaya, ili mvitumie kwa tamaa zenu.
Kama hakuna kitu kinaenda pasipo mazungumzo basi hakuna kitu kinaenda pasipo maombi, na ndio kitu kimojawapo kinachoweza kufanya kuufurahia wokovu wako,
Yohana 16:24 Hata sasa hamkuomba neno kwa jina langu; ombeni, nanyi mtapata; furaha yenu iwe timilifu.
Nyumba ya watu wasiozungumza anguko lake ni kubwa, ndivyo ilivyo wokovu bila maombi huwezi kushamiri,
Hauhitaji kusimamiwa ili uombe unahitaji kujua umuhimu/faida za maombi ili uombe:
Unahitaji kujua umebeba nini ili maombi yawe mazuri, ukibeba hazina njema utaomba vyema ila ukibeba hazina mbaya utaomba vibaya,
Maombi yana nguvu pindi utakapojua nini unafanya! Shetani haogopi maneno yako anaogopa maarifa yako unayo yatumia sio yaliyo kichwani pasipo faida yoyote.
Matendo 19:13 Baadhi ya Wayahudi wenye kutanga-tanga, nao ni wapunga pepo, wakajaribu kutaja jina la Bwana Yesu juu yao waliopagawa na pepo wachafu, wakisema, Nawaapisha kwa Yesu, yule anayehubiriwa na Paulo.
14 Walikuwako wana saba wa mtu mmoja Skewa, Myahudi, kuhani mkuu, waliofanya hivyo.
15 Yule pepo mchafu akawajibu, akawaambia, Yesu namjua na Paulo namfahamu, lakini ninyi ni nani?
16 Na yule mtu aliyepagawa na pepo mchafu akawarukia wawili, akawaweza, akawashinda, hata wakatoka mbio katika nyumba ile hali wa uchi na kujeruhiwa.
Ndani ya maombi kunazaliwa:
a) Kunazaliwa njia kutoka pale ulipo:
- Na hali hii inakupa amani na utulivu hata kama ujatoka katika mazingira hayo,
- Mungu ujifunua katika ulimwengu wa maombi na kukupa mwangaza wako,
Zaburi 16:11 Utanijulisha njia ya uzima; Mbele za uso wako ziko furaha tele; Na katika mkono wako wa kuume Mna mema ya milele.
Zaburi 18:30 Mungu, njia yake ni kamilifu, Ahadi ya Bwana imehakikishwa, Yeye ndiye ngao yao. Wote wanaomkimbilia.
b) Kunazaliwa hali ya kuweza au kushinda,
- Kuna kuimarishwa au kutiwa nguvu unapokuwepo katika maombi pale unapoona moyo wako umezidiwa au kuelemewa.
“ ikiwezekana kikombe hiki kiniepuka “
Luka 22:39 Akatoka akaenda mpaka mlima wa Mizeituni kama ilivyokuwa desturi yake; wanafunzi wake nao wakafuatana naye.
40 Alipofika mahali pale aliwaambia, Ombeni kwamba msiingie majaribuni.
41 Mwenyewe akajitenga nao kama kiasi cha kutupa jiwe, akapiga magoti akaomba,
42 akisema, Ee Baba, ikiwa ni mapenzi yako, uniondolee kikombe hiki; walakini si mapenzi yangu, bali yako yatendeke.
43 Malaika kutoka mbinguni akamtokea akamtia nguvu.
44 Naye kwa vile alivyokuwa katika dhiki, akazidi sana kuomba; hari yake ikawa kama matone ya damu yakidondoka nchini.
c) Hayumbishwi/ kutoyumbishwa
- Mtu anayeomba anajua kwanini anafanya hiki na kwa nini afanyi kile, kwa sababu katika maombi kunazaliwa maongozi,
d) Hauwezi kuchoka/ kutochoka
- Katika maombi kuna kuimarishwa katika utu wa nje na utu wa ndani ila hautukuwa katika hali hii ya uzuri kama tu utaomba vibaya,
Unapokuwa mwana maombi kwa Mungu inakuwa:
i. Ni kitu anachohitaji kusikia
- Mzazi mwenye mapenzi na familia yake upenda kusikia sauti za watoto wake anapokuwa nyumbani, na sio sauti za majirani.
“ njooni tusemezane “
Isaya 1:18 Haya, njoni, tusemezane, asema Bwana. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu.
ii. Ni kitu anachotegemea
Yohana 10:27 Kondoo wangu waisikia sauti yangu; nami nawajua, nao wanifuata.
- Ashtuki kusikia sauti yako.
- Unapoishi katika himaya yake na haumuombi yeye unampa maswali mzazi kuwa yeye ndio baba yako au kuna mtu mwingine anakuhudumia: mathalani unasoma secondary wewe umuombi kitu chochote kwa mzazi, sio nguo za shule, vifaa vya shule au kumkumbusha ada!
Maombi kwa lugha nyepesi ni mazungumzo/ mawasiliano kati ya wewe na unaye muomba,
- Hauwezi kuwa salama nje ya maombi, kwa kuwa kupitia maombi Mungu atajua hitaji lako na kukupatia,
Hakuna maombi yenye majibu halisi nje ya kupendwa!
- Kuna majibu ya haraka na sahihi zaidi pindi utakapo muomba Mungu anayetambua unampenda,
Maombi yasiyobebwa na upendo yanakuwa ni maombi ya msimu namatukio pamoja na mazoea,
Mahali pekee unatakiwa kuwa na furaha na shauku ni mahali pa maombi maana ni mahali ambapo unakwenda kuzungumza na unayempenda na sio adui,
- Kuna maandalizi ya kuzungumza na adui pia kuna maandalizi ya kuzungumza na upendaye!
- Mawasiliano na unayempenda ( maombi ) uongeza pendo: kila mtu anajisikia kwanini leo sijaongea naye na Mungu anasema leo sijamsikia mwanangu/rafiki.
Ili maombi yawe na matokeo:
i. Ni lazima ukiishi kile unachokiomba
- Usiombe kitu ambacho ukielewi wala hauna namna ya kukifanya kuishi kupitia hilo ombi,
- Ni lazima ukiri wako uhusishe moyo wako, usiongee kitu ambacho umeona wengine wanaongea tu, pasipo kujua kwa nini huyu anaongea hivi,
Mathayo 6:7 Nanyi mkiwa katika kusali, msipayuke-payuke, kama watu wa mataifa; maana wao hudhani ya kuwa watasikiwa kwa sababu ya maneno yao kuwa mengi.
ii. Lazima ukiamini kile unachokiomba
- Lazima imani yako iwe katika kile unachokiomba, na ujue maombi ni tendo la kuamisha kitu toka katika ulimwengu war oho na kuingiza katika ulimwengu wa mwili,
- Unahitaji nguvu na maarifa ili kuyafanya hayo na kuamini,
Marko 11:24 Kwa sababu hiyo nawaambia, Yo yote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu.
Waebrania 11:6 Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao.
iii. Maongozi ya Roho mtakatifu
- Huu ndio msingi wa maombi, bila Roho mtakatifu maombi bado hayajaanza,
- Hata kama uliomba kwa miaka 10 ujue bado ujaanza kuomba
- Maombi bila ya Roho mtakatifu ni sawa na kumpigia simu mtu huku simu yako imezima, hakuna muunganiko!
Warumi 8:26 Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa.
INAITWA SIKU! BARIKIWA SANA
Imeandaliwa na:
Cothey Nelson……………………………………………………………0764 018535
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni